06/05/2025
Nimeshindwa kujizuia. Natanguliza kukuombeni radhi kwa lolote nitakaloliandika ambalo bila ya kukusudia litakukwazeni. Nisameheni bure tu.
1. Simba waliiambia Bodi ya Ligi *hawachezi* na ndani ya saa 24 Bodi wakakubakiana nao.
2. Yanga wakaiambia Bodi hiyo hiyo hawachezi kwa sababu za Kanuni kukiukwa, leo ni miezi miwili Bodi haijawajibu Yanga
3. Siyo tu kwamba Bodi haijawajibu Yanga juu ya hoja yao; lakini Bodi ilisema inafanya uchunguzi ambao hadi leo haijatoa taarifa juu ya matokeo ya uchunguzi wao
4. Bodi badala ya kujibu hoja za Yanga, na badala ya kuweka hadharani taarifa ya uchunguzi wao, Bodi wamepanga tarehe ya mechi namba 184.
5. Mwenendo wa Bodi dhidi ya Yanga unaashiria chuki, dharau, kiburi na dhuluma iliyo uchi bila kuvikwa nguo.
6. Tulitaraji TFF waingie kuja kuleta suluhu lakini kumbe Bodi ni petroli na TFF ni kiberiti.
7. Katika mazingira haya ni unyonge usiyo na kifani chake kwa Yanga kukubali kuicheza mechi hii.
8. Kusikilizwa ni haki ya msingi hivyo Bodi na TFF kukataa kuisikiliza Yanga ni dharau ambayo haipendezi, haivumiliki na haikubaliki.
Naunga mkono msimamo wa HATUCHEZIhadi Kanuni zitakapozingatiwa.