Clouds TV

Clouds TV Kituo namba moja cha burudani kwa vijana kikisogeza kila taarifa ya entertainment mbele yako na kuhakikisha hupitwi na yanayojiri ndani na nje ya nchi.

SACP, Muliro Jumanne - K**anda wa Polisi, Kanda Maalumu ya DSM leo Julai 22 kwenye Clouds 360 ya Clouds TV.
22/07/2025

SACP, Muliro Jumanne - K**anda wa Polisi, Kanda Maalumu ya DSM leo Julai 22 kwenye Clouds 360 ya Clouds TV.


SACP, Muliro Jumanne - K**anda wa Polisi, Kanda Maalumu ya DSM akiwa na Timu ya Clouds 360 mara baada ya kumaliza mahoji...
22/07/2025

SACP, Muliro Jumanne - K**anda wa Polisi, Kanda Maalumu ya DSM akiwa na Timu ya Clouds 360 mara baada ya kumaliza mahojiano maalum aliyoyafanya asubuhi ya leo kupitia kipindi hicho.

Cc: .samsasali360 .h.a.g.i.l.e na


"Dar es salaam lazima iwe shwari. Sio k**a nchi zingine ikifika kipindi cha uchaguzi watu wanaondoka halafu wanarudi baa...
22/07/2025

"Dar es salaam lazima iwe shwari. Sio k**a nchi zingine ikifika kipindi cha uchaguzi watu wanaondoka halafu wanarudi baada ya uchaguzi hapana, Kariakoo lazima iendelee kufanya kazi, airport ifanye kazi na shughuli ziendelee. Na siku ya uchaguzi lazima watu wapate haki yao ya kupiga kura.

"Na baada ya uchaguzi kuna watu huwa wanajitoa ufahamu. K**a haujaridhika mahak**a ipo! Kila kitu kwa mujibu wa sheria. Huwezi kutengeneza sheria yako ya kichwani ukaamua kutekeleza kwa jinsi unajisikia wewe!

"Unasukumwa na hisia zako unafanya vitu ambavyo ni kinyume na sheria"- SACP, Muliro Jumanne - K**anda wa Polisi, Kanda Maalumu ya DSM.


"Unakumbuka power window mtu anachukuliwa power window yake Tegeta lakini anaambiwa aende Gerezani, Kariakoo ataipata na...
22/07/2025

"Unakumbuka power window mtu anachukuliwa power window yake Tegeta lakini anaambiwa aende Gerezani, Kariakoo ataipata na akifika anaikuta. Na ule ujinga ujinga wote umeshughulikiwa"-SACP, Muliro Jumanne - K**anda wa Polisi, Kanda Maalumu ya DSM.


"Wananchi wawe na imani na jeshi lao, na Mkuu wa Jeshi la Polisi, IGP Camilius Wambura anafuatilia sana suala la nidhamu...
22/07/2025

"Wananchi wawe na imani na jeshi lao, na Mkuu wa Jeshi la Polisi, IGP Camilius Wambura anafuatilia sana suala la nidhamu, uweledi, uadilifu na haki za wananchi kuliko watu wanavyofuatilia na sisi mak**anda tuna wajibu wa kuhakikisha maaskari wetu wanafanya kazi kwa mujibu wa sheria lakini pia ikitokea watu wanafanya makosa tunarudi kwenye katiba kunakuwa na usawa mbele ya sheria. Neno langu wananchi wa Dar es Salaam tuendelee kushirikiana na wadau wengine"- SACP, Muliro Jumanne - K**anda wa Polisi, Kanda Maalumu ya DSM.


"Kulinganisha jeshi letu la polisi na Marekani ni makosa makubwa wakati unakuta kuna CCTV camera kuanzia ndani. Kuna foo...
22/07/2025

"Kulinganisha jeshi letu la polisi na Marekani ni makosa makubwa wakati unakuta kuna CCTV camera kuanzia ndani. Kuna footage kwenye gari, barabara, ofisini.

"Sasa uchunguzi wake utalinganisha na Mtanzania ambaye anatumia akili yake. Ni kweli kuna mabadiliko makubwa kwenye uchunguzi, tunasoma vizuri lakini pia nadhani ni makosa makosa makubwa kusema kwamba sehemu fulani siku Tano tu kesi imekwisha.

"Nadhani wapelelezi wa Tanzania wana akili kubwa sana wanachunguza hadi kumk**ata mhalifu. Hawa wana akili kuliko hata wa nchi zingine ambao vyombo vyao viko wazi, mtu anangalia na kumuonyesha muhalifu"- SACP, Muliro Jumanne - K**anda wa Polisi, Kanda Maalumu ya DSM.


"Nashangaa watu wanasema askari hajajitambulisha anapokwenda kumk**ata mhalifu. Inategemea na mazingira k**a mhalifu ana...
22/07/2025

"Nashangaa watu wanasema askari hajajitambulisha anapokwenda kumk**ata mhalifu. Inategemea na mazingira k**a mhalifu ana silaha?

"Au alipomuona askari anakimbia! Atajitambulisha vipi? Au wanasema askari hajamwambia mhalifu kosa lake. Atamwambiaje wakati yeye ni mkata mapanga?

"Hajamaliza kumwambia kosa lake si atakuwa ameshamkata mkono? Wakati mwingine askari anaanza kujitambulisha mhalifu anafoka na hampi nafasi askari ya kujitambulisha anafika kituoni anasema hajaambiwa kosa lake.

"Tunakumbana na changamoto k**a hizo. Ni kweli ukisoma sheria inasema ujitambulishe jina lako unapotoka kwenye kituo aelezwe na kosa lake halafu waelekee kituoni. Sasa ustaarabu wa namna hiyo unatakiwa uwe pande zote mbili"- SACP, Muliro Jumanne - K**anda wa Polisi, Kanda Maalumu ya DSM.


"Kwenye sheria hakuna sehemu ambapo pameandikwa kwamba uchaguzi utazuiwa labda kwa kitu kinaitwa au sheria inaitwa No re...
22/07/2025

"Kwenye sheria hakuna sehemu ambapo pameandikwa kwamba uchaguzi utazuiwa labda kwa kitu kinaitwa au sheria inaitwa No reform no election.

"Sisi ni wasimamizi wa sheria. Ukisema utazuia uchaguzi kwa sheria ipi? Kwa slogan hiyo? Mimi ni msimamizi wa sheria, wewe inasema no reform no election, nakushangaa!

"K**a mwanasiasa labda ni slogan unajifurahisha! Nachukulia k**a maoni yako. Hiyo no reform no election ipo kwenye sheria ipi?- SACP, Muliro Jumanne - K**anda wa Polisi, Kanda Maalumu ya DSM.


"Jeshi la Polisi Tanzania lina hati ya maboresho. Na jeshi hili linapitishwa katika awamu tofauti tofauti za kimaboresho...
22/07/2025

"Jeshi la Polisi Tanzania lina hati ya maboresho. Na jeshi hili linapitishwa katika awamu tofauti tofauti za kimaboresho kuhakikisha kwamba linakuwa bora kabisa na linatimiza majukumu yake katika mifumo ya kisheria lakini katika mazingira ambayo ni mazuri.

"Utekelezaji wake mkubwa kwenye miaka ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan. Tunakwenda kwenye utekelezaji na ile hati bado ipo.

"Na utekelezaji wake unaonekana kwa macho na unaweza kuona mabadiliko makubwa sana kwenye jeshi la polisi kwenye Awamu ya Sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan pamoja na IGP Camilius Wambura ni formula iliyokutana na inatekelezeka.

"Kitu kikubwa na cha gharama ni mtu kufanya majukumu yake katika mazingira mazuri ya kisheria. Na pia maarifa ambayo ni elimu.

"Askari wengi na maafisa wengi wa Polisi wanapata maarifa na elimu katika vyuo vya ndani na nje ya nchi kulingana na mazingira na aina ya makosa ambayo yamekuwa yakitokea hapa"- SACP, Muliro Jumanne - K**anda wa Polisi, Kanda Maalumu ya DSM.


"Unakumbuka eneo la Kibamba kulikuwa na shauri la Tarimo alitekwa na watu walijifanya ni askari polisi na ukiwaangalia w...
22/07/2025

"Unakumbuka eneo la Kibamba kulikuwa na shauri la Tarimo alitekwa na watu walijifanya ni askari polisi na ukiwaangalia wapo k**a polisi.

" Na wanasema wampeleke Gogoni au Osterbay polisi na watu wanabaki na kumbukumbu kwamba wale walikuwa ni polisi.

" Lakini baadae tulifanya kazi ya ziada na wale jamaa walik**atwa. Walikuwa ni wahalifu tu"-SACP, Muliro Jumanne - K**anda wa Polisi, Kanda Maalumu ya DSM.


SACP, Muliro Jumanne - K**anda wa Polisi, Kanda Maalumu ya DSM akiingia Mjengoni muda mfupi kabla ya kuingia kwenye maho...
22/07/2025

SACP, Muliro Jumanne - K**anda wa Polisi, Kanda Maalumu ya DSM akiingia Mjengoni muda mfupi kabla ya kuingia kwenye mahojiano maalum kwenye kipindi cha Clouds 360 cha Clouds TV. Amepokelewa na Mkuu wa Maudhui Clouds Media Group, na Producer wa kipindi cha Clouds 360,


Sauti ya K**anda kusikika kesho ndani ya  ! Ni sauti yenye majibu ya maswali yote yanayohusu Usalama ndani ya jiji letu ...
21/07/2025

Sauti ya K**anda kusikika kesho ndani ya !

Ni sauti yenye majibu ya maswali yote yanayohusu Usalama ndani ya jiji letu la Dar-Es-Salaam,

Kwako mwana Kanda Maalumu, una swali lipi kwenda kwa SACP: Muliro Jumanne - K**anda wa Polisi, Kanda Maalumu ya DSM.

Usikose kuanzia 12:00 asubuhi kesho live on !

Address


Opening Hours

Monday 08:00 - 17:00
Tuesday 08:00 - 17:00
Wednesday 08:00 - 17:00
Thursday 08:00 - 17:00
Friday 08:00 - 17:00

Telephone

+255222781445

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Clouds TV posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to Clouds TV:

Shortcuts

  • Address
  • Telephone
  • Opening Hours
  • Alerts
  • Contact The Business
  • Claim ownership or report listing
  • Want your business to be the top-listed Media Company?

Share