Nkungu Fm

Nkungu Fm Nkungu FM radio ni radio ya kijamii inayopatikana katika wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma nchini Tanzania. Karibu kutusikiliza kupitia95.7 MHz

Usisahau ku-subscribe,  Ku-share na ku-comment
10/02/2025

Usisahau ku-subscribe, Ku-share na ku-comment

Endelea kuhabarika na N-FM katika platform zetu kwa mitandao ya kijamii.......Coming soon kwa 95.7MHz
23/04/2022

Endelea kuhabarika na N-FM katika platform zetu kwa mitandao ya kijamii.......Coming soon kwa 95.7MHz

N-FM KARIBU YAKO..............
23/04/2022

N-FM KARIBU YAKO..............

MUNGU ni mwema kwetu coming soon......
16/04/2022

MUNGU ni mwema kwetu coming soon......

TAARIFA: Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amewataka Viongozi kufanya kazi kwa kuzingatia...
02/04/2022

TAARIFA: Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amewataka Viongozi kufanya kazi kwa kuzingatia Mipango, Sheria, Miongozo, pamoja na Dira ya Maendeleo ya nchi ili kukuza ustawi wa taifa.
Mhe. Rais Samia amesema hayo leo mara baada ya kuwaapisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Bunge, Sera na Uratibu, Waziri wa Katiba na Sheria, Waziri wa Maliasili na Utalii, Mwenyekiti wa Baraza la Maadili pamoja na Wajumbe wake wawili na viongozi wengine pia katika hafla iliyofanyika Ikulu Chamwino, Mkoani Dodoma.
Aidha, Rais Samia amesema Serikali imedhamiria kukuza uchumi wa nchi baada ya kuathiriwa na UVIKO 19, hivyo ili kufikia azma hiyo ni wajibu kila Kiongozi kwenye kila sekta kutekeleza wajibu na majukumu yake ipasavyo.
Rais Samia amewataka Viongozi hao kusimamia na kutekeleza majukumu waliyopangiwa kikamilifu kwa kushirikiana, kuheshimiana na kuzingatia viapo vyao.
Kwa upande wa Baraza la Maadili, Rais Samia amewataka viongozi aliowaapisha kuanza kazi mara moja kwa kuzifanyia kazi kesi za maadili ndani ya Utumishi wa Umma zinazowasilishwa katika Baraza hilo.
Hafla hiyo ya Uapisho imehudhuriwa na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa. Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Tulia Ackson, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Liberata Mulamula, Katibu Mkuu Kiongozi Mhe. Balozi Hussein Katanga pamoja na viongozi wengine wa Serikali.

Mapema, Umoja wa Ulaya ulikuwa ukiangazia namna ya kuishawishi China kutoiunga mkono kwa namna yoyote Urusi katika mzozo...
02/04/2022

Mapema, Umoja wa Ulaya ulikuwa ukiangazia namna ya kuishawishi China kutoiunga mkono kwa namna yoyote Urusi katika mzozo huo unaotishia kuathiri mahusiano ya kibiashara baina ya mataifa yenye nguvu kubwa ya kiuchumi ulimwenguni.

Michel na von der Leyen kabla ya kuzungumza na rais Jinping, walikutana kwanza na waziri mkuu wa China Li Keqiang, na kulingana na taarifa mazungumzo yao yalikuwa ni ya kuangazia masuala ya bishara na mabadiliko ya tabianchi, ingawa hata hivyo yaligubikwa na wasiwasi wa magharibi kuhusiana na uungaji mkono wa China kwa Urusi katika mzozo huo wa Ukraine.

Soma Zaidi: Marekani, washirika wazidisha shinikizo la kiuchumi kwa Urusi

China yasema itatumia njia zake kusaka amani nchini Ukraine.

Msemaji wa wizara ya mambo ya kigeni wa China, Zhao Lijian aliwaambia waandishi wa habari kwamba kwenye mazungumzo hayo, Keqiang aliwaambia viongozi hao wa Ulaya kwamba China itaamua njia zake yenyewe za kusaka amani nchini Ukraine baada ya Brussels kuishinikiza kutoa uhakikisho kwamba haitaisaidia Urusi kwa kuipatia silaha ama kuvikwepa vikwazo vya magharibi.

"Kuhusiana na suala la Ukraine, ningependa kusisitiza dhamira ya China ya kuwa na sera huru ya mambo ya nje ya amani na itatoa uamuzi wake kwa kuzingatia umuhimu wa suala hilo. Mbali na hayo, nchi zote zina haki zao za kujitegemea kuamua sera zao za kigeni. Hazipaswi kuwalazimisha wengine kuchukua upande au kuchukua mtazamo rahisi wa 'rafiki au adui' au 'mweusi au nyeupe'. China na nchi nyingine ikiwa ni pamoja na zinazoendelea, zina msimamo sawa kuhusu suala hili." alisema Lijian.

Umoja wa Ulaya unahofia kwamba kushindwa kwa China kulaani uvamizi wa Urusi nchini Ukraine, kunamaanisha kwamba huenda iko tayari kuisaidia Urusi na mzozo wa kibinaadamu nchini humo.

Soma Zaidi: Viongozi wa dunia wailaani Urusi kuhusu Ukraine

Balozi Lutong ambaye pia ni mkuu wa mahusiano ya Ulaya katika wizara hiyo ya mambo ya nje ya China amesema pande hizo mbili zimekubaliana kushirikiana ili kurejesha amani, utulivu

Chama Cha Waajiri  nchini  (ATE) kimeahidi kuendelea kufanya kazi bega kwa bega na wadau wake ambao ni Mashirika binafsi...
02/04/2022

Chama Cha Waajiri nchini
(ATE) kimeahidi kuendelea kufanya kazi bega kwa bega na wadau wake ambao ni Mashirika binafsi, watu wenye ulemavu pamoja na Serikali katika kusimamia masuala ya ajira .

Akizungumza leo katika Ofisi za ATE zilizopo Mikocheni Dar Es Salaam Meneja wa ATE Kanda ya Kati Dodoma Leonard Selestini alisema hayo katika mkutano uliowakutanisha na Jumuia ya watu wenye Ulemavu nchini ambao ni TASI,TLB na CHAVITA.

Wakizungunza kwa nyakati tofauti watu wenye ulemavu wamesema kuwa bado kunachangamoto nyingi katika utekelezwaji wa sheria ya kupata ajira.

Katibu wa Tanzania Albinism Society (TASI) M***a Kabimba alisema kuwa "Tuko hapa kujadili sheria inayoihusu utekelezwaji wa upatikanaji wa ajira kwa watu wenye ulemavu nchini sababu bado kunachangamoto nyingi ambazo watu wenye ulemavu wanakumbana nazo katika upatikanaji wa ajira hivyo tuko hapa kujadili ili nao waweze kunufaika" alisema Kabimba.

Katika mkutano huo watu hao wenye ulemavu waliweza kutoa maoni mbalimbali na kuishauri ATE iweze kuweka utaratibu wa kufanya ufuatiliaji kwa watu wenye ulemavu pindi wanapoajiriwa hii itasaidia kung'amua changamoto wanazokumbana nazo.

Serikali imesema itaendelea kuratibu na kusimamia sera zinazohusu masuala ya lishe k**a hatua ya kukabiliana na utapiaml...
02/04/2022

Serikali imesema itaendelea kuratibu na kusimamia sera zinazohusu masuala ya lishe k**a hatua ya kukabiliana na utapiamlo na udumavu ndani ya jamii kuhakikisha inakuwa salama na yenye afya bora.

Kauli hiyo ilitolewa na Mkurugenzi wa Idara ya Mipango na Bajeti Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Eleuter Kihwele mara baada ya semina ya kuijengea uelewa Menejimenti ya Ofisi hiyo kuhusu Utekelezaji wa Mpango wa Pili Jumuishi wa Masuala ya Lishe nchini iliyotolewa na Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania (TFNC) katika Ukumbi wa Ofisi hiyo Jijini Dodoma.

Mkurugenzi huyo alisema kulingana na Mpango wa Taifa wa Lishe wa miaka mitano umesisitiza ushirikishwaji wa sekta binafsi kushiriki katika hatua zote za kupanga na kutekeleza mipango inayohusiana na lishe pamoja na ushirikishwaji wa wananchi.

“Lishe ni suala mtambuka linalohusisha wadau wote na wananchi hasa katika muktadha mzima wa kubadili tabia ya ulaji wa vyakula unaozingatia misingi ya lishe kuwe na nyaraka hizi za mpango wa miaka mitano ambazo zitakuwa ni rahisi kueleweka kwa wananchi na kutekeleza. Pia ni lazima tuimarishe uratibu na ugharamiaji wa utekelezaji wa mpango ili yote yatekelezwe kikamilifu ifikapo 2025/2026,” alisema Mkurugenzi huyo.

Pia aliongeza kuwa Ofisi ya Waziri Mkuu ina jukumu la kuratibu shughuli za lishe nchini kwa kuzingatia kuwa k**a nchi imeandaa mpango wa miaka mitano wa kuratibu masuala ya lishe baada ya kumalizika kwa mpango wa kwanza wa masuala hayo ambao umetekelezwa kwa miaka mitano.

“Mkutano huu umekuwa na manufaa makubwa kwa washiriki na wadau waliohudhuria kufahamu ni wadau gani wanaopasawa kusimamia masuala haya hivyo imekuwa ni fursa muhimu kwa Menejimenti ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa maana ya uongozi na wakuu wa Idara ambao wanasamamia masuala haya kuelewa na kwenda kusimamia utekelezaji wake,” alieleza Bw. Kihwele.

Kwa upande wake Mtafiti Mwandamizi kutoka Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania (TFNC) Bw. Luitfrid Peter akiwasilisha taarifa ya hali ya lishe nchini alibainisha kwam

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama akizungumza na Mene...
02/04/2022

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama akizungumza na Menejimenti ya Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma alipokutana na Menejimenti hiyo kwa lengo la kuhimiza uwajibikaji na kukagua ujenzi wa Ofisi za makao makuu ya Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma jijini Dodoma. Kulia kwake ni Kamishna wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Mhe. Jaji Sivangilwa Mwangesi na kushoto kwake ni Mkurugenzi Idara ya Ujenzi Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) Mhandisi Loishorwa Likimaitare.

Kamishna wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi, Mhe. Jaji Sivangilwa Mwangesi akitoa neno la utangulizi kabla ya kumkaribisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama kuzungumza na Menejimenti hiyo kwa lengo la kuhimiza uwajibikaji na kukagua ujenzi wa Ofisi za makao makuu ya Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma jijini Dodoma.

Muonekano wa jengo la ofisi za makao makuu ya Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma linaloendelea kujengwa jijini Dodoma na Mkandarasi ambaye ni Wakala wa Majengo Tanzania (TBA)

Na James K. Mwanamyoto-Dodoma
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama ameielekeza Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma kushughulikia malalamiko na tuhuma zinazowasilishwa na wananchi kuhusu Viongozi wa Umma wanaokiuka maadili ili kuwa na viongozi waadilifu wanaotekeleza majukumu yao kwa maendeleo ya taifa.

Mhe. Jenista ameyasema hayo leo alipokutana na Menejimenti ya Sekretarieti hiyo kwa lengo la kuhimiza uwajibikaji na kukagua ujenzi wa Ofisi za makao makuu ya Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma jijini Dodoma.

Mhe. Jenista amesema, kumekuwa na malalamiko kutoka kwa wananchi kuhusu mwenendo wa baadhi ya Viongozi wa Umma kwenye eneo la uadilifu, hivyo Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi ina jukumu kubwa la kuyapokea malalamiko hayo na kuyafanyia kazi ili viongozi wawe

Tupe maoni yako kuhusu operation hii......
02/04/2022

Tupe maoni yako kuhusu operation hii......

Mkutano mkuu Wa CCM ulihudhuriwa na wakuu Wa idara mbalimbali na marais wastaafu akiwemo mzee Jakaya Mrisho Kikwete rais...
02/04/2022

Mkutano mkuu Wa CCM ulihudhuriwa na wakuu Wa idara mbalimbali na marais wastaafu akiwemo mzee Jakaya Mrisho Kikwete rais Wa awamu NNE Wa JMT.....

Tarehe moja mwezi Wa NNE ni ilikuwa ni siku muhimu kwa wana-CCM walipokutana Dodoma kwa lengo LA kujadili mambo mbalimba...
02/04/2022

Tarehe moja mwezi Wa NNE ni ilikuwa ni siku muhimu kwa wana-CCM walipokutana Dodoma kwa lengo LA kujadili mambo mbalimbali ili kuimarisha chama chini ya Mwenyekiti Wa chama Mh. Samia Suluhu Hasan.
Kikao hicho kilifanikisha kupatikana kwa makamu Mwenyekiti Wa chama Comred Abdulahman Kinana na kurejeshewa kadi za uanachama wanachama waliovuliwa uanachama akiwemo aliyekuwa waziri Wa mambo ya nje Ndg. Bernard Camilius Membe.
Pamoja na mambo mengine mengi yaliyofanyika ya kichama ambapo mkutano huo ulihudhuriwa na wajumbe kutoka katika mikoa mbalimbali, viongozi Wa taasisi mbalimbali za Chama ikiwemo UVCCM na UWT.

Address


Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Nkungu Fm posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to Nkungu Fm:

Shortcuts

  • Address
  • Alerts
  • Contact The Business
  • Claim ownership or report listing
  • Want your business to be the top-listed Media Company?

Share