Mzawaonline

Mzawaonline Ukurasa Rasmi wa Mzawa Online

24/07/2025

Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Suleman Jafo, ashiriki hafla ya Uzinduzi wa Mkakati wa Kitaifa wa Utekelezaji wa Eneo Huru la Biashara la Afrika (AfCFTA), leo Julai 24, 2025, jijini Dar es Salaam.

17/07/2025

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Akizindua Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050, Dodoma Tanzania leo tarehe 17 Julai, 2025.

15/07/2025

Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt. Seleman Jafo Ashiriki Mkutano Wamiliki wa Viwanda Tanzania l, leo tarehe Julai 15, 2025.

Mkuu wa  Mkoa  wa Manyara Mhe. Queen  Sendiga  leo Julai 11,2025 wilayani Hanang amezindua rasmi mradi wa usambazaji wa ...
11/07/2025

Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe. Queen Sendiga leo Julai 11,2025 wilayani Hanang amezindua rasmi mradi wa usambazaji wa mitungi ya gesi ya kilo sita kwa bei ya ruzuku mkoa wa Manyara. uzinduzi huo umeongozwa na mkuu wa mkoa pamoja na viongozi wengine wa mkoa, wilaya, kata pamoja na vijiji na vitongoji vyake.

Mhe. Sendiga amesema lengo la uzinduzi mradi ni kuutambulisha rasmi mradi kwa wananchi wa mkoa wa Manyara ambao ndio walengwa na wanufaika wa mradi.

Mhe. Sendiga, amepongeza juhudi za Serikali na REA katika kufanikisha utekelezaji wa mradi na kuongeza kuwa lengo la Mkakati wa Nishati Safi ya Kupikia ni kuwa ifikapo mwaka 2034, asilimia 80 ya Watanzania wawe wanatumia nishati safi ya kupikia, jambo ambalo litasaidia kutunza na kuhifadhi mazingira.

“Serikali, imeweka ruzuku ya asilimia 50, kwa hiyo wakina Baba na kina Mama wa mkoa wa Manyara, wajiandae kutumia gesi, tuwapunguzie wakina Mama kushika masizi, kutumia kuni na mikaa, kwetu sisi Mradi huu ni neema”. Alisema, Mhe. Sendiga.

Kwa upande wake, Msimamizi wa mradi kutoka REA, ndugu Abdulrazack Mkomi amesema kwa nchi nzima Mradi huo wa kusambaza mitungi ya gesi ya kilo 6 kwa Wananchi utagharimu shilingi bilioni 8 ambapo kwa mkoa wa Manyara zaidi ya shilingi milioni 284 zitatumika kugharamia mitungi 16,275 kwa mkoa mzima na kila wilaya mitungi 3,255 itasambazwa

“Kampuni ya MANJIS imeshinda, tenda ya kusambaza mitungi hiyo, ilitangaza ofa ya kusambaza mtungi mmoja kwa shilingi 35,000 kwa kutambua hilo, Serikali italipia asilimia 50 ya bei hiyo, ambayo itakuwa shilingi 17,500.” Alifafanua, Mkomi.

Mkomi, amesema ili kupata mtungi huo wenye ruzuku ya Serikali kila Mwananchi anapaswa kuwa na kitambulisho cha NIDA.

Aidha Mhe. Sendiga amewaomba wananchi kutoa ushirikiano wakutosha kwa mtoa huduma (MANJIS LOGISTICS LTD) ili kufanikisha utekelezaji wa mradi na kuwasihi wananchi kutumia fursa ya upatikanaji wa mitungi ya gesi kwa bei ya ruzuku kuweza kuachana na matumizi ya nishati zisizo salama za kupikia ili kuweza kutunza na kuboresha afya zao ,mazingira pamoja na kuimarisha usawa wa kijinsia.

Mkoa wa Manyara una jumla ya wilaya 5 ambazo Wananchi wake watanufaika na mitungi ya gesi ni pamoja na wilaya ya Babati, Hanang, Simanjiro, Mbulu na Kiteto.

08/07/2025

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji Prof.Kitila Mkumbo, ashiriki Kikao cha Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), kuhusu uzinduzi wa Dira ya Taifa, unaofanyika ukumbi wa Serena Hoteli, jijin Dar Es Salaam leo tarehe 08 Julai, 2025.

30/06/2025

Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt. Seleman Jafo Ashiriki Mkutano wa Maafisa Biashara wa Mkoa, Wakuu wa Idara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Morogoro, leo tarehe Juni 30,, 2025.

Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Kisarawe, Dk. Selemani Jafo, amechukua fomu ya kuwania nafasi ya Ubunge kwa mara nyingine t...
29/06/2025

Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Kisarawe, Dk. Selemani Jafo, amechukua fomu ya kuwania nafasi ya Ubunge kwa mara nyingine tena kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Dk. Jafo amejaza fomu hiyo na kuirejesha kwa Katibu wa Chama hicho wa Wilaya ya Kisarawe, Ndugu Josephine Mwanga.

26/06/2025

BUNGE LA KUMI NA MBILI, MKUTANO WA KUMI NA TISA, KIKAO CHA 54, 26 JUNI 2025

20/06/2025

Naibu Waziri wa Viwand ana Biashara Mhe. Exaud Kigahe Ashiriki maathimisho ya CBE CAREEA FAIR 2025 JUNI 20 2025 Dar Es Salaam

06/06/2025

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mhe. Mohamed Mchengerwa, anazungumza na waandishi wa habari leo, Juni 6, 2025, jijini Dodoma

04/06/2025

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa, ashiriki katika uwekaji wa jiwe la msingi la Viwango House, leo Juni 4, 2025, eneo la Njendengwa, jijini Dodoma.

Wakala wa Nishati Vijijini (REA) umeitambulisha kampuni ya Lake Gas Limited ambayo imepewa jukumu la kusambaza mitungi y...
02/06/2025

Wakala wa Nishati Vijijini (REA) umeitambulisha kampuni ya Lake Gas Limited ambayo imepewa jukumu la kusambaza mitungi ya gesi 13,020 itakayouzwa kwa bei ya ruzuku ya asilimia 50 katika Mkoa wa Shinyanga.

Hayo yamebainishwa leo Juni 2, 2025 katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga na Mhandisi wa Miradi kutoka REA, Bi. Annet Ndyanabo wakati wa uwasilishwaji wa taarifa ya utekelezaji wa mradi wa usambazaji mitungi ya gesi yenye ujazo wa kilo sita mkoani humo.

Mha. Ndyanabo amesema kuwa mitungi ya gesi 13,020 itakayosambazwa mkoani Shinyanga ni utekelezaji wa Mkakati wa Kitaifa wa Nishati Safi ya Kupikia ambao una lengo la kuongeza matumizi ya nishati safi kufikia asilimia 80 ifikapo 2034.

"Utekelezaji wa mradi huu unaenda sambamba na malengo ya Mkakati wa Kitaifa wa Matumizi ya Nishati Safi ya kupikia (2024-2034) ambao unalenga kuongeza matumizi ya nishati safi ya kupikia kufikia asilimia 80 ya watanzania wanaotumia nishati hiyo ifikapo mwaka 2034," Amesema Mha. Ndyanabo.

Ameongeza kuwa, lengo la mradi ni kuongeza upatikanaji wa huduma za nishati safi ya kupikia kwa kuwawezesha wananchi wengi kumudu gharama za bidhaa za nishati safi ili kutunza mazingira.

"Mradi huu utapunguza umaskini kwa kuwapa muda zaidi wanawake kushiriki katika shughuli za kiuchumi pindi wanapotumia mitungi ya gesi k**a njia mbadala ya kupikia badala ya kuni na mkaa," Ameongeza Mha. Ndyanabo.

Kwa upande wake, Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga, CP Salum Hamduni ameipongeza REA kwa kuja na mradi huo na kuiomba iwe endelevu ili iweze kuwasambazia wananchi wengi nishati hiyo muhimu.

Naye, Mratibu wa nishati safi kutoka kampuni ya Lake Gas Limited, Bw. Ramadhan Siasa amesema watatekeleza mradi huo kwa kuzingatia makubaliano ya Mkataba wa kusambaza mitungi ya gesi ya kupikia pamoja na kutoa elimu kwa wananchi ili kuchochea matumizi ya nishati hiyo.

Gharama ya Mradi huo ni shilingi 272,769,000 na wilaya zitakazonufaika ni pamoja na Wilaya ya Shinyanga, Kishapu, Ushetu na Msalala na kila wilaya itapata mitungi 3,255.

Address


Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Mzawaonline posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Shortcuts

  • Address
  • Telephone
  • Alerts
  • Claim ownership or report listing
  • Want your business to be the top-listed Media Company?

Share