06/08/2025
Mtoto wa Freeman Mbowe, Mwenyekiti mstaafu wa CHADEMA, James Mbowe,amesema anamuuga mkono Freeman Mbowe, kwa kitendo chake cha kutotoa maoni yake juu ya yanayoendelea ndani ya chama hicho pamoja na kesi ya Mwenyekiti wa chama hicho Tundu Lissu.
James, ameyasema hayo wakati akizungumza na wanahabari kuhusu mwenendo wa chama hicho akiwa katika ofisi za CHAUMMA.
"Taasisi inayowekeza kwenye kutukana waasisi wake, imejiua yenyewe, namuunga mkono Freeman Mbowe, kunyamaza, yeye kwenye chama alimaliza wajibu wake, sasa mnataka aseme nini wakati wajibu wake yeye alishamaliza" amesema
Imeandikwa na Elizabeth Zaya
Credit
NipasheDigital