AWR Tanzania

AWR Tanzania Sikiliza Sauti ya Matumaini AWR Tanzania (Morning Star Radio zamani). ujumbe wa matumaini kwa watu wote.

Njozi za kuanzishwa kwa Radio hii, zilianza mnamo miaka ya tisini, ambapo mwaka 2000 viongozi wa makanisa ya Dar es salaam walikutana na kuweka mkakati madhubuti ya kuanzisha radio,kwa wakati huo ikijulikana k**a TAWR (Tanzania Adventist World Radio). Mwaka 2001, uchunguzi yakinifu wa kuanzishwa kwa Kituo hiki ulianza chini ya kitengo cha mawasiliano cha Makao makuu ya Kanisa Tanzania kijulikanach

o k**a TAMC (Tanzania Adventist Media Center). Baada ya mikakati madhubuti kukamilika, ujenzi wa kituo cha radio ulianza rasmi mnamo mwaka 2002, katika eneo la Mikocheni B, jijini Dar es salaam, ujenzi ambao uliendelea na kukamilika kwa sehemu kubwa mnamo mwaka 2003. Mnamo tarehe moja mwezi wa kumi mwaka 2003, kituo kilirusha matangazo yake kwa mara ya kwanza k**a
majaribio, kwa kutumia mtambo wa kurushia matangazo wenye uwezo wa watt 500, na tangu hapo safari ya
matangazo kusikika hewani iliendelea! Mwezi wa kumi na moja mwaka wa 2003, kituo kilifunguliwa rasmi na Mgeni aliyehudhuria
shughuli hiyo, Mchungaji Jan Paulsen, akija k**a Rais wa kanisa la Waadventista wasabato
Duniani, akitoea Nchini Marekani ambako ndiko makao makuu ya Kanisa Duniani, yalipo. Majuma mawili baada ya kufunguliwa rasmi kwa kituo, Mtambo wa kurushia matangazo
uliokuwa umefungwa mikocheni B mahali zilipo studio, ulishindwa kufanya kazi
kutokana na hitilafu iliyosababishwa na umeme, tatizo lililojitokeza baada ya mvua kali kunyesha. Jitihada za kujaribu kuirejesha katika hali ya kuendelea kufanya kazi zilishindikana,
jambo lililopelekea muingiliano na vyombo vingine vya habari, na kituo kufungwa kwa muda
na tume ya mawasilianona, ili kutoa nafasi ya kufanyika kwa marekebisho. Kituo kilirejea
tena katika hali yake na kuendelea na matangazo baada ya miaka miwili baadae. Mwaka 2005 mwezi wa tano,vifaa vipya vya kurushia matangazo viliagizwa ili kurejesha matangazo tena. Uagizaji huo
ulichukua muda wa miezi mitatu, na mwezi wa nane vifaa viliwasili na ufungaji ukaanza mara moja, wakati huu mtambo
ukiwa umehamishiwa eneo la kisarawe, mkoa wa Pwani. Baada ya ufungaji mtambo kukamilika, mnamo mwezi wa nane mwaka 2005, urushaji wa matangazo ya majaribio
ulianza mara moja, ambapo majaribio hayo yalichukua takribani mwezi mmoja, hadi mnamo mwezi wa tisa! Ilipofika tarehe 26, mwezi wa tano mwaka 2006, saa 11:00 jioni, kituo kilirusha
matangazo moja kwa moja kwa mara ya kwanza, baada ya matangazo ya majaribio
kukamilika! Tangu hapo, Morning Star Radio imeendelea kurusha matangazo yake hadi hivi sasa,
ambapo watu mbali mbali wamekuwa wakibarikiwa sana na matangazo haya, na kwa
hakika kituo hiki kimekuwa ni mbaraka sana kwa ma elfu ya wakaazi wa Tanzania
na dunia kwa ujumla ambapo matangazo
ya Redio hii yanasikika!

Taarifa namba 7 ya k**ati ya uchaguzi katika Mkutano Mkuu wa 62 wa Konferensi Kuu ya Kanisa la Waadventista wa Sabato Du...
07/07/2025

Taarifa namba 7 ya k**ati ya uchaguzi katika Mkutano Mkuu wa 62 wa Konferensi Kuu ya Kanisa la Waadventista wa Sabato Duniani, imechagua wenyeviti 13 wa Divisheni za Kanisa hilo, ikiwemo Divisheni ya Mashariki Kati mwa Afrika ECD, ambapo Mchungaji na Daktari Blasious Ruguri amechaguliwa kwa mara nyingine kuiongoza Divisheni hiyo kwa kipindi cha miaka mitano.

Tangu kuanza kwa Mkutano Mkuu tarehe 03 Julai 2025, k**ati ya Uchaguzi imekuwa ikitoa taarifa zake katikati ya vipindi vya mjadala, ambapo taarifa ya Kwanza ilikuwa ya uchaguzi wa Mwenyekiti wa Konferensi Kuu ya Kanisa la Waadventista wa Sabato Duniani.

Viongozi hawa wa Divisheni wamechaguliwa kwa kura za ndio 1720 kati ya kura 1833 zilizopigwa.

Paul Douglas amechaguliwa tena kuhudumu katika nafasi Mweka Hazina na Afisa Mkuu wa fedha wa Makao Makuu ya Kanisa la Wa...
07/07/2025

Paul Douglas amechaguliwa tena kuhudumu katika nafasi Mweka Hazina na Afisa Mkuu wa fedha wa Makao Makuu ya Kanisa la Waadventista Wasabato Duniani yaliyoko Silver Spring, Maryland. Anasimama katika nafasi ya ofisa akihusika na maswala yote ya kifedha kimataifa kwa Kanisa na familia ya taasisi za kanisa. Paul amechaguliwa tena katika nafasi hii akiwa na uzoefu wa zaidi ya miaka 30.

Richard E. McEdward amechaguliwa kuwa Katibu Mkuu wa Kanisa la Waadventista wa Sabato Ulimwenguni. Wajumbe walimpigia ku...
07/07/2025

Richard E. McEdward amechaguliwa kuwa Katibu Mkuu wa Kanisa la Waadventista wa Sabato Ulimwenguni. Wajumbe walimpigia kura McEdward katika Mkutano Mkuu wa 62 wa Konferensi Kuu (GC) unaofanyika St. Louis, Missouri.

Akiwa mmoja wa maafisa watatu wakuu wa uongozi wa kanisa hilo lenye zaidi ya waumini milioni 23 katika zaidi ya nchi 200, McEdward atasimamia uratibu wa shughuli za kimataifa za kanisa hilo. Majukumu yake yanajumuisha kusaidia miundo ya utawala, kuongoza mabadiliko ya uongozi, na kuwezesha taasisi za kanisa kutekeleza huduma yao kwa ufanisi katika maeneo na tamaduni mbalimbali.

Jina la McEdward liliwasilishwa na Kamati ya Uteuzi ya Mkutano Mkuu na uteuzi wake uliwasilishwa kwa wajumbe wote na kuthibitishwa kwa kura kutoka kwa wajumbe waliowakilisha kila eneo la kanisa duniani ambapo kura za kuthibitisha jina lake zilikuwa 1,630 za ndio dhidi ya 153.

Kabla ya kuchaguliwa, alikuwa ni Kiongozi wa Kanisa la Waadventista wa Sabato katika Unioni Misheni ya Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini (MENAUM), ambako aliongoza juhudi za kimkakati katika moja ya maeneo magumu zaidi kwa huduma ya injili duniani.

McEdward ambaye anakuwa Katibu Mkuu wa 25 katika historia ya kanisa hilo alizaliwa Seattle, Washington, na alitumia miaka ya utotoni Jeddah, Saudi Arabia, ambako familia yake iliishi k**a wageni. Uzoefu huo wa awali wa kuishi kati ya jamii mbalimbali unaelezwa kuwa ulimjengea huruma ya kina na kusudi la kushiriki upendo wa Kristo katika mipaka ya kitamaduni na kidini.

Ana shahada ya kwanza kutoka Chuo Kikuu cha Walla Walla, Shahada ya Uzamili ya Uungu kutoka Chuo Kikuu cha Andrews, na Shahada ya Uzamivu ya Uinjilisti wa Kimataifa kutoka Chuo Kikuu cha Theolojia cha Fuller. Huduma yake ya kikazi inajumuisha kuwa mchungaji, Mratibu wa uanzishaji wa makanisa huko Sri Lanka na Divisheni ya Asia-Pasifiki Kusini, na Mkurugenzi msaidizi wa Taasisi ya Utume wa Ulimwenguni ya Chuo Kikuu cha Andrews.

Baadaye alijiunga na Konferensi Kuu (GC), ambako alihudumu k**a Mkurugenzi msaidizi wa Ofisi ya Utume wa Waadventista na Mkurugenzi wa Vituo vya Utume wa Duniani kwa Dini mbalimbali. Mwaka 2016, alichaguliwa kuongoza MENAUM, makao yake yakiwa Beirut, Lebanon, ambako alisaidia wafanyakazi wa utume na kupanua uwepo wa utume wa kanisa hilo katika maeneo ya mijini na yasiyofikiwa.

McEdward amemuoa Marcia McEdward, muuguzi wa aliyesajiliwa, Wana watoto wawili wakubwa, Julia na Joshua.

Katibu Mkuu wa Kanisa hilo ulimwenguni ana jukumu muhimu katika uratibu wa kimataifa wa Kanisa la Waadventista wa Sabato. Likihusisha kusimamia shughuli za kiutawala, kusaidia mabadiliko ya uongozi, kudumisha kumbukumbu sahihi za uanachama na sera, na kuwaongoza viongozi wa kikanda katika kupanga na kutekeleza utume. Pia hufanya kazi kwa karibu na idara zinazolenga utume, zikiwemo Ofisi ya Utume wa Waadventista, Taasisi ya Utume wa Dunia, na Ofisi ya Kumbukumbu na utafiti.

Katika jiji la St. Louis, Missouri, Marekani, Mkutano Mkuu wa 62 wa Konferensi Kuu ya Kanisa la Waadventista wa Sabato U...
05/07/2025

Katika jiji la St. Louis, Missouri, Marekani, Mkutano Mkuu wa 62 wa Konferensi Kuu ya Kanisa la Waadventista wa Sabato Ulimwenguni umemchagua Erton Köhler kuwa Kiongozi Mkuu wa Kanisa hilo Ulimwenguni kwa kipindi cha miaka mitano.

Ni utaratibu wa kawaida kwa Kanisa la Waadventista wa Sabato Duniani kufanya mkutano wa Konferensi Kuu kila baada ya miaka mitano. Mkutano huu huwaleta pamoja wajumbe kutoka mataifa mbalimbali duniani kote, ambapo miongoni mwa shughuli zake kuu ni uchaguzi wa viongozi wa Kanisa kwa ngazi ya Konferensi Kuu yenye makao yake makuu Marekani, pamoja na viongozi wa Divisheni 13 duniani.

Kabla ya kuchaguliwa kwake, Erton Köhler alikuwa Katibu Mtendaji wa Kanisa la Waadventista wa Sabato Duniani nafasi aliyoianza rasmi Aprili 14, 2021. Kabla ya hapo, aliwahi kuwa Kiongozi wa Divisheni ya Amerika ya Kusini, akihudumu katika eneo hilo lenye nchi nane tangu mwaka 2007, alipochaguliwa akiwa na umri wa miaka 36 na kuwa mmoja wa viongozi vijana zaidi kwa jukumu hilo katika historia ya Divisheni hiyo.

Köhler alizaliwa kusini mwa Brazil na tangu utotoni alitamani kufuata nyayo za baba yake ambaye alikuwa mchungaji wa Waadventista. Alipata Shahada ya Kwanza ya Theolojia mwaka 1989 katika Taasisi ya Mafunzo ya Waadventista, ambayo sasa ni Chuo Kikuu cha Waadventista cha Brazil. Mwaka 2008, alihitimu tena kutoka chuo hicho akiwa na Shahada ya Uzamili katika Theolojia ya Kichungaji. Kwa sasa, anaendelea na masomo ya Shahada ya Udaktari wa Huduma ya Kichungaji katika Chuo Kikuu cha Andrews nchini Marekani.

Kati ya mwaka 1990 hadi 1994, alikuwa mchungaji wa kanisa mahalia huko São Paulo. Baadaye, mwaka 1995, alichaguliwa kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Vijana wa Konferensi ya Rio Grande do Sul, kisha mwaka 1998 akawa Mkurugenzi wa Huduma za Vijana wa Unioni ya Kaskazini-Mashariki mwa Brazil. Mwaka 2002, alirejea katika Konferensi ya Rio Grande do Sul k**a Katibu Mtendaji, na mwaka uliofuata akachaguliwa kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Vijana kwa nchi nane za Divisheni ya Amerika ya Kusini (SAD) kabla ya kuwa Kiongozi wa Divisheni hiyo mwaka 2007.

Köhler amemuoa Adriene Marques, ambaye ni muuguzi, na wamejaliwa watoto wawili. Pamoja, wamekuwa mstari wa mbele katika huduma ya kanisa, wakihudumu bega kwa bega na kutembelea waumini duniani kote. Amekuwa akisisitiza mitazamo thabiti kuhusu athari za michezo ya kompyuta kwa vijana, upendeleo wa muziki unaojenga imani, na umuhimu wa kushikilia imani kuliko kuhusika kisiasa.

Katika nafasi yake mpya, Köhler ataongoza Kanisa la Waadventista wa Sabato Duniani akiwa ni kiongozi mkuu wa kiutawala. Atasaidia kuunda maono ya kimkakati ya utume wa Kanisa hilo lililoko katika nchi zaidi ya 200 duniani, kutoa mwongozo wa mafundisho, na kuunganisha maeneo mbalimbali kupitia utume wa pamoja. Atakuwa mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Utendaji ya Konferensi Kuu, mabaraza kadhaa ya kanisa, na atashirikiana kwa karibu na viongozi wa Divisheni, akiwakilisha kanisa katika matukio makubwa ya kimataifa.

Pia anatarajiwa kuhamasisha mipango ya utume wa dunia, kuhakikisha uthabiti wa mafundisho ya Waadventista, na kuimarisha taasisi za elimu, afya, na vyombo vya habari vya kanisa hilo.

Kanisa la Waadventista wa Sabato limekuwa dhehebu la Kiprotestanti la kimataifa tangu mwaka 1863, likiwa na zaidi ya waumini milioni 23 kote duniani. Biblia inatambuliwa kuwa mamlaka kuu ya mafundisho ya kanisa, na ujumbe wake ni kuwasaidia watu kupata uhuru, uponyaji, na tumaini katika Yesu Kristo.

31/05/2025

Yesu anakuja upesi, una nafasi ya kuchagua upande, nakupendekezea sasa umchague Yesu, siku anaporudi uwe kati ya watakaomlaki mawinguni, vinginevyo nni kilio na kusaga meno.

21/05/2025

....Sikiliza kwa makini, elewa, Chukua hatua...


05/05/2025

DARNETEVENT 2025 | N U R U Y A M A T U M A I N I
Tukiwa tumebakiwa na siku 5 pekee, Mch. DR BLASIOUS RUGURI anakualika katika mkutano huu wa kipekee, usipange kukosa.

Alika jirani zako, Ndugu na Jamaa kushiriki mbaraka huu wa kipekee, na kuwa sehemu ya kupeleka Nuru yenye Tumaini kupitia Mahubiri makuu, Mafundisho ya Afya, Familia pamoja na Elimu juu ya Sheria.

📺>> Hope Channel Tz || Azam 466, Zuku 870
📻>> AWR Tanzania || 105.30 FM Dar es salaam // Rock FM Mbeya
🤳>> Youtube / Tiktok / Instagram

Mkutano huu unadhaminiwa na Kanisa la Waadventista wa Sabato Tanzania, Chama cha Wanataaluma na Wajasiriamali wa Kiadventista Tanzania ATAPE na Jumuia ya Watanzania waishio Marekani na Canada TAUS.


DARNETEVENT 2025 | N U R U Y A M A T U M A I N I______________________________________________siku 11 pekee zimebaki ili...
30/04/2025

DARNETEVENT 2025 | N U R U Y A M A T U M A I N I

______________________________________________siku 11 pekee zimebaki ili kuanza kwa Mahubiri ya Kipekee kutokea Jiji la Dar es Salaam, N U R U Y A MA T U M A I N I, mahubiri ya kipekee yakiruka kutokea kuanzia Tar 10 - 31 Mei 2025 Saa 11.00 Jioni hadi 02.00 Usiku.
Mahubiri haya yatakuwa live kupitia na .radio

Alika jirani zako, Ndugu na Jamaa kushiriki mbaraka huu wa kipekee, na kuwa sehemu ya kupeleka Nuru yenye Tumaini kupitia Mahubiri makuu, Mafundisho ya Afya, Familia pamoja na Elimu juu ya Sheria.

📺>> Hope Channel Tz || Azam 466, Zuku 870
📻>> AWR Tanzania || 105.30 FM Dar es salaam // Rock FM Mbeya
🤳>> Youtube / Tiktok / Instagram

Mkutano huu unadhaminiwa na Kanisa la Waadventista wa Sabato Tanzania, Chama cha Wanataaluma na Wajasiriamali wa Kiadventista Tanzania ATAPE na Jumuia ya Watanzania waishio Marekani na Canada TAUS.



2d
1m

DARNETEVENT 2025 | N U R U  Y A  M A T U M A I N I _____________________________________________________________________...
21/04/2025

DARNETEVENT 2025 | N U R U Y A M A T U M A I N I

______________________________________________________________________________________________
N U R U Y A MA T U M A I N I, mahubiri ya kipekee yakiruka kutokea kuanzia Tar 10 - 31 Mei 2025 Saa 11.00 Jioni hadi 02.00 Usiku.
Mahubiri haya yatakuwa live kupitia na .radio

Alika jirani zako, Ndugu na Jamaa kushiriki mbaraka huu wa kipekee, na kuwa sehemu ya kupeleka Nuru yenye Tumaini kupitia Mahubiri makuu, Mafundisho ya Afya, Familia pamoja na Elimu juu ya Sheria.

📺>> Hope Channel Tz || Azam 466, Zuku 870
📻>> AWR Tanzania || 105.30 FM Dar es salaam // Rock FM Mbeya
🤳>> Youtube / Tiktok / Instagram

Mkutano huu unadhaminiwa na Kanisa la Waadventista wa Sabato Tanzania, Chama cha Wanataaluma na Wajasiriamali wa Kiadventista Tanzania ATAPE na Jumuia ya Watanzania waishio Marekani na Canada TAUS.


DARNETEVENT 2025 | N U R U  Y A  M A T U M A I N I______________________________________________________________________...
20/04/2025

DARNETEVENT 2025 | N U R U Y A M A T U M A I N I

______________________________________________________________________________________________
Ni siku 20 pekee zimebaki ili kuanza kwa Mahubiri ya Kipekee kutokea Jiji la Dar es Salaam, N U R U Y A MA T U M A I N I, mahubiri ya kipekee yakiruka kutokea kuanzia Tar 10 - 31 Mei 2025 Saa 11.00 Jioni hadi 02.00 Usiku.
Mahubiri haya yatakuwa live kupitia na .radio

Alika jirani zako, Ndugu na Jamaa kushiriki mbaraka huu wa kipekee, na kuwa sehemu ya kupeleka Nuru yenye Tumaini kupitia Mahubiri makuu, Mafundisho ya Afya, Familia pamoja na Elimu juu ya Sheria.

📺>> Hope Channel Tz || Azam 466, Zuku 870
📻>> AWR Tanzania || 105.30 FM Dar es salaam // Rock FM Mbeya
🤳>> Youtube / Tiktok / Instagram

Mkutano huu unadhaminiwa na Kanisa la Waadventista wa Sabato Tanzania, Chama cha Wanataaluma na Wajasiriamali wa Kiadventista Tanzania ATAPE na Jumuia ya Watanzania waishio Marekani na Canada TAUS.


Sabato Njema kwako na Familia yako, chukua nafasi kuwatakia rafiki na ndugu Sabato Njema. Ni wakati wa kufurahi na kusha...
21/02/2025

Sabato Njema kwako na Familia yako, chukua nafasi kuwatakia rafiki na ndugu Sabato Njema. Ni wakati wa kufurahi na kushangilia Bwana ametukirimu sabato nyingine.




Kamati Kuu Tendaji ya Divisheni ya Afrika Mashariki na Kati, Kanisa la Waadventista wa Sabato, imemteua Ndg. Shabatu Nic...
14/02/2025

Kamati Kuu Tendaji ya Divisheni ya Afrika Mashariki na Kati, Kanisa la Waadventista wa Sabato, imemteua Ndg. Shabatu Nicholas Msaki, kuwa Mhazini Mkuu wa Unioni Misheni ya Kusini mwa Tanzania. Mabadiliko haya yanakuja baada ya kikao kilichokaa siku ya 13 mwezi Febduari mwaka huu

Address


Alerts

Be the first to know and let us send you an email when AWR Tanzania posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Shortcuts

  • Address
  • Alerts
  • Claim ownership or report listing
  • Want your business to be the top-listed Media Company?

Share