Radio Kwizera

  • Home
  • Radio Kwizera

Radio Kwizera The Official page of Radio Kwizera
97.7 Kagera, Geita and Mwanza | 93.7 Kigoma | 89.5 Shinyanga.
(202)

Community Radio, seeks to restore hope, peace and development in the North-West Tanzania.

21/07/2025

YALIYOJIRI - RK

AD: Fursa za masomo kwako kijana ambaye ungependa kusoma . Changamkia nafasi hizi upate elimu bora na muongozo mwema wa ...
20/07/2025

AD: Fursa za masomo kwako kijana ambaye ungependa kusoma . Changamkia nafasi hizi upate elimu bora na muongozo mwema wa maisha.

ST. Augustine University of Tanzania-Tabora Centre


20/07/2025

SYNOD & SYNODALITY -RK

DINI: Katika kipindi kilichopita, tulikufahamisha maana ya Sinodi, leo tunakuletea maana ya neno synodality. Tuandikie u...
20/07/2025

DINI: Katika kipindi kilichopita, tulikufahamisha maana ya Sinodi, leo tunakuletea maana ya neno synodality. Tuandikie unachokielewa na mchango wako utasomwa studioni. Kumbuka ni kuanzia saa 4 kamili asubuhi na marudio yake saa 1 kamili jioni.



Amecea Secretariat

MICHEZO: Baada ya kuitumikia kwa miaka 11 akitokea Kagera Sugar, hatimaye nahodha Mohamed Hussein almaarufu Tshabalala a...
19/07/2025

MICHEZO: Baada ya kuitumikia kwa miaka 11 akitokea Kagera Sugar, hatimaye nahodha Mohamed Hussein almaarufu Tshabalala ameipungia mkono wa buriani.

Beki huyo ameandika ujumbe mzito kwenye ukurasa wake kikubwa akiishukuru timu nzima ya Simba. Amesema uamuzi huu ni wa kibinafsi.

Huku tetesi zikitanda mtandaoni kuelekea watani wao Young Africans Sports Club , je, unahisi usajili wake Jangwani utakuwa wa tija?


GEITA: Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa TAKUKURU mkoani Geita imewataka Mawakala wa  Miamala ya simu kuwa makini...
19/07/2025

GEITA: Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa TAKUKURU mkoani Geita imewataka Mawakala wa Miamala ya simu kuwa makini wakati wa kutekeleza majukumu yao ikiwa ni njia ya kuepuka kushiriki vitendo vya rushwa katika kuelekea uchaguzi mkuu.

Katika mwendelezo wa utoaji wa elimu kwa makundi mbalimbali katika jamii, mkuu wa TAKUKURU mkoa wa Geita Bw James Ruge katika mafunzo kwa kundi la Mawakala wa Miamala ya fedha kupitia mitandao ya simu, amesema jukumu la kudhibiti vitendo vya rushwa sio la serikali pekee bali ni jukumu la kila mmoja.

Afisa Uchunguzi TAKUKURU Mkoa wa Geita Bw. Said Lipunjije amesema kundi hili linaweza kuwa sehemu ya kufanikisha nia ovu ya utoaji wa rushwa hasa pale wagombea watakapopita kwenye ofisi za mawakala wa fedha na kutuma fedha kwa walio wakusudia

Noela Lucas ambaye ni mmoja wa washirki wa mafunzo amehoji kuhusu usalama wake baada ya kutoa taarifa ambapo TAKUKURU itahakikisha anakuwa salama kwa kupatiwa ulinzi wakati wa ufuatiliaji wa taarifa hiyo na hatua hiyo inaweza kufikia maamuzi ya ofisi yake kumhamisha kikazi kwenda eneo lingine lenye usalama zaidi.

Nao baadhi ya mameneja na mawakala wa miamala ya kifedha kupitia mitandao ya simu wamesema mafunzo hayo yatawasaidia kutoa taarifa za viashiria vya rushwa kupitia namba ya TAKUKURU ambayo ni 113

✍🏾 Samwel Masunzu- Geita

MICHEZO: Klabu ya  imetangaza kuachana na mchezaji Debora Fernandes MAVAMBO.Raia huyo wa Angola, mwenye umri wa miaka 25...
19/07/2025

MICHEZO: Klabu ya imetangaza kuachana na mchezaji Debora Fernandes MAVAMBO.

Raia huyo wa Angola, mwenye umri wa miaka 25, alisajiliwa Simba Julai, 2024 kwa muda wa miaka mitatu akitokea Mutonda Stars ya Zambia.

Baada ya msimu mmoja tu akivalia jezi ya wekundu wa msimbazi, wametangaza kuvunja ndoa yao baada ya makubaliano ya pande zote mbili.

MAVAMBO anajiunga na Fabrice Ngoma, Kelvin Kijili, Augustine Okejepha, Aishi Manula, Valentin Nouma na Hussein Kazi ambao pia wamevunja uhusiano na Simba.

Je, k**a shabiki sugu wa Simba, hili umelipokeaje?



Young Africans Sports Club

KAGERA: Mkuu wa wilaya ya Biharamulo mkoa wa Kagera  SACP ADVERA BULIMBA amewataka bodaboda kuendelea  kulinda amani, na...
19/07/2025

KAGERA: Mkuu wa wilaya ya Biharamulo mkoa wa Kagera SACP ADVERA BULIMBA amewataka bodaboda kuendelea kulinda amani, na kudhibiti vitendo vya uhalifu katika kipindi hiki kuelekea uchaguzi mkuu wa Rais, wabunge na madiwani unaotarajia kufanyika Oktoba 28, 2025.

Mkuu huyo wa Wilaya amesema hayo baada ya kukutana na viongozi wa Bodaboda katika maegesho mbalimbali ikiwa sehemu ya kutafuta ufumbuzi wa kero na changamoto zinazowakabili hasa wimbi wa wizi pikipiki unaoripotiwa kila mara.

Amesema kuwa ili kudhibiti uhalifu na wizi wa pikipiki, kila bodaboda awe mlinzi wa mwenzake na kwamba watakapoona dalili za uhalifu watoe taarifa kwa jeshi la polisi ili kuzuia kabla ya kutendeka.

Amewataka bodaboda kushirikiana na serikali katika kuchochea maendeleo ya wananchi. Pia, DC ameonya jeshi la polisi wanaofanya kazi bila kuzingatia maadili ya kazi yao hasa kujihusisha na vitendo vya rushwa na kupelekea malalamiko kwa baadhi ya bodaboda huku akiwataka watakaovunja sheria kuwajibishwa kwa mujibu wa sheria.

Naye mwenyekiti wa bodaboda Wilaya ya Biharamulo Bw. Allen Rukala amempongeza mkuu wa Wilaya kwa namna anavyoshirikiana na Bodaboda kwa shughuli mbalimbali za kiserikali na kumhakikishia kuwa wataendelea kumpa taarifa ya viashiria vya uhalifu vitakavyojitokeza katika maeneo Yao.

Na - Biharamulo.


19/07/2025

MICHEZO: Kifaa kipya cha Young Africans Sports Club chatoboa siri. Kwa nini kachagua Jangwani?




18/07/2025

SPORTS CORNER -RK

HABARI SAA 2 USIKU - RK
18/07/2025

HABARI SAA 2 USIKU - RK

HABARI SA 2 USIKU -RK Kwizera Ngara Kagera Tanzania | Unaweza kuisikiliza Radio Kwizera kwa masafa mbalimbali: 97.7 KAGERA...

Address


Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Radio Kwizera posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to Radio Kwizera:

Shortcuts

  • Address
  • Alerts
  • Contact The Business
  • Claim ownership or report listing
  • Want your business to be the top-listed Media Company?

Share