
02/07/2025
Ndugu zangu,
Kwa masikitiko napenda kuwajulisha kuwa sintochukua Fomu kuwania nafasi yoyote katika Uchaguzi huu wa mwaka 2025,
Haijawa rahisi kwangu kufanya uamuzi huu kwasababu ni uamuzi unaoleta simanzi kwangu kwasababu dhamiri ya kuwatumikia ndugu zangu ninayo na ndio inayoniumiza zaidi,
Lakini uamuzi huu nimeufanya kutokana na mfumo wa Uchaguzi wa sasa hususani katika suala la Majina matatu,
Nimeheshimu maamuzi ya Chama na ninaamini ya kuwa Chama kilipendekeza mfumo huu huenda ni kwa nia njema kabisa,
Lakini kwa sisi wanachama ambao hatuna wakutusemea kwenye vikao vya maamuzi mfumo huu umekuwa kitanzi kikubwa kwetu,
Naomba nitoe shukrani zangu za dhati kwa wanachama wa CCM Jimbo la Songea Mjini,
Kwa kuniamini na kunipigia kura katika kura za maoni mwaka 2020 hata nikaweza kushika nafasi ya tatu,
Mwenyezi Mungu awalipe kwa Imani yenu mliyoiweka kwangu,
Kwa kaka zangu walionizidi kura
Dkt. Damas Ndumbaro na Eng. Alfred Koyoya Fuko nawaomba shindaneni kwa upendo na amani,
Hamkuwahi kuwa maadui kabla ya kugombea pamoja hivyo msikubali Siasa iue Udugu wenu,
Tushirikiane kuendeleza nyumbani,
Naomba niwatakie heri wanachama wenzangu wa Jimbo la Songea Mjini na Mkoa wa Ruvuma kwa ujumla,
Lakini pia niwatakie heri wanachama wote wa Chama cha Mapinduzi (CCM) nchi nzima,
Wanaogombea na wasiogombea,
Rai yangu kwa wanachama wote naomba na nawasihi sana tuchague Viongozi wenye hofu ya Mungu, wakweli, waaminifu na watu wa haki,
Tuchague Viongozi wenye uwezo wa Kiuongozi, wenye Upendo na wananchi na Upendo wa maeneo tunayotoka, wenye maono makubwa na mikakati dhahiri ya kuyafikia maono hayo,
Mwenyezi Mungu akipenda tutaonana tena wakati mwingine,
Ndimi ndugu yenu
IBRAHIM JEREMIAH