Azam TV

Azam TV Azam Media Ltd is a Tanzanian media company owned by the Bakhresa Group.

Under the AzamTV brand | Follow our other accounts AzamTV Burudani AzamSports Sinema Zetu HD

27/07/2025

Mabadiliko ya kasi ya teknolojia yameleta mageuzi makubwa katika mfumo wa malezi ya watoto hapa nchini, hasa kutokana na muingiliano wa tamaduni kupitia vifaa vya kidijitali k**a simu janja. Wazazi na walezi wamesema hali hiyo inaleta athari mseto kwa vijana, ikiwemo kupotea kwa maadili ya kitanzania.

Wakizungumza na , baadhi yao wamehimiza jamii kuchukua hatua madhubuti kwa kuweka mipaka ya matumizi ya teknolojia kwa watoto, sambamba na kuwalea katika misingi bora ya maadili ili teknolojia iwe msaada na si tishio kwa maendeleo ya watoto.


✍Joyce Mwakalinga
Mhariri|

27/07/2025

Mwalimu wa Shule ya Msingi Sinya, Samwel Mlay anadaiwa kujitoa uhai kwa kujichoma moto akiwa nyumbani kwao wilayani Rombo mkoani Kilimanjaro, Julai 25 mwaka huu. Marehemu alikuwa akifundisha katika shule hiyo iliyopo Longido, mkoani Arusha.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Kikosi cha Zimamoto Mkoa wa Kilimanjaro, Jeremiah Mkomagi, inadaiwa kuwa marehemu alikumbwa na msongo wa mawazo uliotokana na mgogoro wa muda mrefu wa ndoa yake jambo linalodhaniwa kuwa chanzo cha tukio hilo la kusikitisha.


Mhariri|

27/07/2025

Wakazi wa kijiji cha Chanoni, Shehia ya Tundauwa, Wilaya ya Chake Chake , Pemba, wameeleza hofu yao kuhusu ukosefu wa daraja la kuunganisha kijiji hicho na chai jirani ambako hupata huduma muhimu k**a afya na elimu.

Wamesema hali huwa mbaya zaidi wakati wa msimu wa mvua, ambapo hulazimika kuvuka mto kwa njia zisizo salama, jambo ambalo linaweka maisha ya wakazi hususani wanafunzi hatarini kila siku. Wanatoa wito kwa mamlaka husika kuchukua hatua haraka kujenga daraja hilo ili kulinda usalama wa jamii.


✍️Aisha Haji
Mhariri|

27/07/2025

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko, amesema kuwa asilimia 80 ya vifo nchini vinaweza kuzuilika endapo Watanzania watachukua hatua ya kubadili mtindo wa maisha, hasa kwa kujenga utamaduni wa kufanya mazoezi mara kwa mara.

Dkt. Biteko ameyasema hayo leo, Jumapili, Julai 27,2025 jijini Dodoma alipomwakilisha Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa katika kilele cha msimu wa sita wa NBC Dodoma Marathon 2025 ambayo imelenga kuchangisha fedha kwaajili ya kuboresha afya ya mama na mtoto.


Mhariri|

27/07/2025

Jumla ya taasisi 88, zikiwemo 76 za ndani na 12 kutoka nje ya nchi, zimepata kibali rasmi cha kuwa waangalizi wa uchaguzi mkuu wa Rais, wabunge na madiwani utakaofanyika Oktoba 29, 2025.

Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Jaji mstaafu Jacobs Mwambegele, ametoa taarifa hiyo leo, Julai 27,2025 katika kikao na wadau wa vyama vya siasa na kufafanua kuwa taasisi hizo zimeidhinishwa baada ya kukidhi vigezo na masharti ya kuwa waangalizi huru wa uchaguzi huo muhimu kwa taifa.


Mhariri|

27/07/2025

Watu wanaokopa katika taasisi za fedha na kukwepa wajibu wa kurejesha mikopo hiyo wameonywa kuacha mwenendo huo kwasababu unafuatiliwa na mfumo maalum uliopo Benki Kuu hivyo wakibainika watajiondolea sifa ya kukopeshwa kabisa.

Rai hiyo imetolewa katika Mkutano Mkuu wa Wanahisa wa Benki ya Mkombozi ambao katika upande mwingine umetangaza kutoa gawio la Shilingi 92.40 kwa kila hisa kuanzia mwezi Agosti owaka huu.

Hatua hiyo ya utoaji gawio ambalo lilikuwa halijaiolewa kwa kipindi kirefu imekuja baada ya benki hiyo kuonesha ukuaji katika kipindi cha miaka 16 ya kuanzishwa kwake huku wananchi wakihimizwa kutunza fedha zao kupitia taasisi za fedha hususani benki ili kuzipa usalama fedha zao na kuzizalisha kupitia mikopo inayotolewa na benki hizo.

Imeandaliwa na

Mhariri

27/07/2025

Katika jitihada za kuunga mkono mkakati wa Serikali wa kuifungua Tanzania kwa dunia kupitia sekta k**a viwanda, kilimo, elimu na afya, vijana wa Kitanzania wameendelea kuhamasishwa kuchangamkia fursa za masomo nje ya nchi ili waweze kuwa sehemu ya maendeleo ya taifa.

Wito huu umetolewa jijini Arusha, kwenye Maonyesho ya 18 ya Elimu ya Juu ya Nje ya Nchi, ambapo Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Global Education Link, Abdumalick Mollel, amesema maonyesho hayo yanalenga kuwapa vijana nafasi ya kuchagua kozi mbalimbali kutoka vyuo vya kimataifa, hatua inayoweza kuwajengea uwezo wa kushindana katika soko la ajira la Afrika na duniani.

✍ Ramadhani Mvungi
Mhariri

27/07/2025

Kijana John Joseph anayeishi na ulemavu, amesema msingi mzuri wa malezi ya wazazi, ni nyezo muhimu ya kumfanya mtoto aishi katika maisha ya uadilifu bila kujali k**a ana hali ya ulemavu au ni mzima.

Anasema anaamini ulemavu ni zawadi na ni mpango wa Mungu.

✍Gideon Paschal
Mhariri |

27/07/2025

Kujikubali ni nyezo muhimu katika kufanikiwa maishani, hivi ndivyo ilivyokuwa kwa Nipaeli Mtana ambaye ni mlemavu wa viungo, ambaye anasema mwanzo aliona aibu hata kupiga picha, lakini baada ya kujikubali na kuona fahari kuishi na ulemavu, ameweza kufika mbali na kipaji chake cha kuimba.Sikiliza shairi lake aliloimba "Je unanipenda? au unanipenda pia"

✍Gideon Paschal
Mhariri |

Michezo ya kimataifa ya kirafiki inaendelea  Karatu, mkoani Arusha.Leo saa 9:00 Alasiri, Taifa Stars kucheza na Senegal....
27/07/2025

Michezo ya kimataifa ya kirafiki inaendelea Karatu, mkoani Arusha.

Leo saa 9:00 Alasiri, Taifa Stars kucheza na Senegal.

Jumanne, Saa 9:00 Alasiri Senegal kucheza na DR Congo

Michezo hii kuruka mbashara kupitia AzamSports1HD.

Kwa kifurushi cha shilingi 28,000 unatazama michezo hii.

27/07/2025

Jumuiya ya Maridhiano na Amani (JMAT) Mkoa wa Morogoro, imetoa wito na kuwaomba viongozi wa dini kuhamasisha amani na utulivu kuelekea kipindi cha uchaguzi, ili kuufanya uchaguzi kuwa wa amani na wenye utulivu.

JMAT imeeleza kuwa vingozi wa dini wana nafasi kubwa katika kuhamasisha amani na utulivu kupitia nyumba za ibada kwa waumini wa dini mbalimbali jambo ambalo litasaidia amani endelevu nchini.

✍️ Theresia Mwanga

Mhariri@claud_jm

27/07/2025

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dkt. Hussein Omar ametoa rai kwa walimu hapa nchini kuendana na mabadiliko ya sayansi na teknolojia, ikiwa ni pamoja na matumizi ya TEHAMA kwa kufundishia, ili kuzalisha wataalamu wanaohitajika katika soko la ajira duniani.

Amesema hayo mkoani Morogoro katika mafunzo ya sayansi, hisabati na TEHAMA kwa walimu wa sekondari, ikiwa kwa awamu ya tatu ya mwaka 2024/2025.

Takribani walimu 1800 wamepatiwa mafunzo hayo ambayo yatakuwa chachu ya kuongeza ubora wa elimu pamoja na kuongeza ubunifu kwa wanafunzi katika elimu.

✍️ Theresia Mwanga

Mhariri|

Address


Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Azam TV posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to Azam TV:

Shortcuts

  • Address
  • Telephone
  • Alerts
  • Contact The Business
  • Claim ownership or report listing
  • Want your business to be the top-listed Media Company?

Share