13/01/2024
Kocha wa zamani wa timu ya Taifa ya England Sven-Goran Eriksson (75), ameeleza baadhi ya mambo ambayo anatamani kuyafanya katika siku zake za maisha zilizobakia.
Mapema jana Kocha huyo mkongwe ameeleza kusumbuliwa na ugonjwa wa saratani ya kongosho (pancreas) iliyofikia hatua za mwisho.
Akizungumza na Sky News, Sven amesema mpango wake ni kusafiri na kuhudhuria mechi nyingi.
Aidha anayotamani zaidi awe na nafuu ya afya aweze kuiona ni kati ya kati ya England na Brazil itakayofanyika mwezi Machi huko Wembley.
"Natamani nisiwe na maumivu makali sana, ili niweze kwenda Uingereza kutizama mechi hiyo itakayochezwa Machi 23".
"Kuamka bila maumivu ni zawadi kubwa sana ambayo watu tunaichukulia kirahisi pale tunapokuwa na afya, lakini tukiugua ndio tunaelewa umuhimu wake".
Alipoulizwa ikiwa kuna nafasi kwenye soka ambayo aliwahi kuitamani bila mafanikio, alijibu,
"Kuwa Meneja wa Liverpool, sikufanikiwa, mimi bado ni shabiki wa Liverpool".
"Nakumbuka nilikuwa nikipishana sana maneno na Sir Alex Fergusson, kuna wakati tulihitaji wachezaji wengi kutoka Manchester United, hii ni kawaida, ile ilikuwa klabu bora sana"