24/06/2024
Kampuni ya Airtel imetangaza kuwasha mkongo wa mawasiliano unaopita baharini wa 2Africa, hatua hii italeta mabadiliko chanya katika huduma ya intaneti Tanzania.
Uzinduzi huo uliongozwa na Rais Dr Samia Suluhu Hassan, Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Africa Segun Ogunsanya, pamoja na Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari mheshimiwa Nape Nnauye.
Mkongo huu wa mawasiliano unaongeza ufanisi katika upatikanaji wa intaneti yenye kasi na hivyo kufungua fursa zaidi katika elimu, biashara na sekta ya mawasiliano kwa watanzania.