Wasafi TV

Wasafi TV Official page For Wasafitv Channel
(11)

22/07/2025

KAMPUNI ya Selcom kupitia Huduma yake ya kifedha ya kidigitali -Selcom Pesa imezindua kampeni ya Huduma ya Mabando ya Miamala, ijulikanayo k**a "Tumia Bando la miamala, k**a Bure,okoa gharama" ikiwa ni muendelezo wa dhamira yake ya kutoa Huduma za kifedha zenye gharama nafuu kwa watanzania.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo Mkuu wa kitengo Cha Masoko wa Selcom Shumbana Walwa amesema kampeni hiyo imekuja baada ya mafanikio ya kampeni ya kwanza ya 5 kwa jero iliyoanzisha ajenda ya upatikanaji wa Huduma nafuu Zaidi kwa Kila Mtanzania

Aidha ameeleza kwamba Mabando ya Miamala ya Selcom pesa ni ya kwanza Tanzania yakilera SULUHISHO jipya linalomwezesha watumiaji kufanya miamala kwa makato madogo kuliko huku wakijipangia matumizi Yao kwa ufanisu bila kutozwa ada ya Kila muamala.

Kampeni hiyo inalenga siyo tu kupunguza gharama kwa watumiaji Bali pia KUWAJENGEA tabia ya kupanga matumizi ya kifedha kwa unafuu Zaidi

20/07/2025

WAZIRI ULEGA ATUMIA SAA MBILI NA MTOTO MWENYE KIPAJI KUTIMIZA NDOTO ZAKE

Waziri wa Ujenzi, Abdallah Ulega, leo ametumia zaidi ya saa mbili kuzungumza na kumtembeza mtoto mwenye kipaji kutoka Dodoma kwenye maeneo aliyotamani kuyaona jijini Dar es Salaam.

Wiki hii, picha mjongeo za mtoto huyo, Ridhiwani Asheri mwenye umri wa miaka 13 zilisambaa kwenye mitandao ya kijamii zikiionyesha uwezo wake mkubwa wa kubuni ujenzi wa barabara na madaraja akiwa kijijini kwao Kibaigwa, Dodoma.

Baada ya Ulega ambaye ana dhamana ya masuala ya ujenzi nchini kuona picha hizo, aliagiza wataalamu wa wizara yake kwenda kumwona na kuangalia namna ya kumsaidia.

Baada ya kumwona na kuzungumza na familia, waziri aliomba mkutano nao ili kuangalia namna bora ambayo serikali inaweza kufanikisha ndoto zake.

Baada ya mkutano wa jana katika ofisi ndogo za Wizara ya Ujenzi jijini Dar es Salaam, Ulega alisema serikali ya Tanzania ina historia, uwezo na dhamira ya kusaidia watoto wenye uwezo mkubwa kimaarifa kwa maslahi ya taifa.

Baada ya mazungumzo hayo Waziri Ulega ameahidi kumsaidia kijana huyo kuhakikisha anatimiza ndoto zake za kuwa Mhandisi mkubwa hapo baadaye.

Waziri Ulega amesema atakaa na Wizara ya Elimu kuona ni sehemu gani sahihi kijana huyo apelekwe ili kuweza kumsaidia kielimu hasa kwenye maswala ya ujenzi.

Pia Waziri Ulega amemtembeza mtoto huyo katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam ili aweze kujionea kwa macho yale ambayo alikuwa anayatengeneza akiwa nyumbani kwao kwa kuyaona tu kwenye TV.

Miongoni mwa maeneo hayo ni Daraja la Kijazi lililopo Ubungo, Daraja la Tanzanite na kituo cha Treni ya Mwendokasi (SGR) Posta

20/07/2025

Teknolojia huko Amerika, Ulaya na mataifa makubwa imefikia kiwango cha kutengeneza binadamu halisi kwa kutumia DNA pekee.

TAYARI SIMULIZI HII MPYA IPO YOUTUBE KATIKA CHANNEL YETU YA .

Cc.
Co-Producer
Graphics / VFX
Editor
Videographers &

19/07/2025

USHIRIKA VILLAGE YAWAKARIBISHA WADAU MBALIMBALI WA MAENDELEO, MASHIRIKA YOTE NCHINI NA NJE YA NCHI.
Fursa ya kipekee ya kushiriki kwenye Maonyesho ya Kimataifa ya Kilimo ya Nane Nane 2025 imewadia!
Kuanzia tarehe 1 hadi 8 Agosti 2025, Dodoma, Kwenye Viwanja vya 8 8 (Nane Nane) jiunge na Ushirika Village Kupata eneo maalum lenye mabanda 100+ ya maonyesho kutoka kwa:

-Mashirika ya Ushirika na Kilimo
-Wadau wa Masoko na Mitaji
-Sekta ya Mifugo, Lishe, Chakula na Mashine
-Watoa Teknolojia, Ubunifu na Uwekezaji
-Wadau wa Madini,Uvuvi na Saccos
- Wadau wote mnakaribishwa kwenye Ushirika Village.

Onesha bidhaa zako, panua mtandao wa kibiashara, fikia wateja wapya na shiriki midahalo ya kitaalamu.

Nafasi ni chache! Wahi nafasi yako ya kushiriki leo!

Tupigie +255789856246
Barua pepe [email protected]

Ccfederation




19/07/2025

Usiruhusu kabisa Weekend yako kuwa kinyonge, mizigo hii hapa ya kibabe alafu mipyaaaaa. 🎬🍿🔥

Usikose kutazama kila siku ya Jumatatu Alhamisi na Jumamosi saa 07:45 jioni

Cc


13/07/2025

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewahimiza wafanyabiashara wa kimataifa kuwahamasisha wawekezaji wengine kuja kuwekeza Tanzania ili kutumia fursa zilizopo katika sekta mbalimbali kwa ajili ya uzalishaji wa bidhaa ndani ya nchi.

Akizungumza wakati wa hafla ya kufunga Maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba), Waziri Mkuu amesema Tanzania ina fursa nyingi katika kila sekta na ni wakati muafaka kwa wawekezaji kuzichanganua na kuzalisha bidhaa.

Waziri Mkuu amesisitiza umuhimu wa kuendelea kutangaza maonesho ya Sabasaba ili kuvutia wafanyabiashara na wawekezaji ambao watajenga viwanda na kuongeza thamani ya rasilimali zilizopo nchini, na kuuza bidhaa kwenye masoko ya kimataifa.

Ameiagiza Wizara ya Viwanda na Biashara kushirikiana na wafanyabiashara ili kuelewa namna bora ya kutangaza fursa za uwekezaji nchini, kwa lengo la kukuza uchumi wa Taifa.

Aidha, Waziri Mkuu ameitaka
Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) kutafuta masoko ya bidhaa za Tanzania nje ya nchi, ili kila mzalishaji aweze kufahamu mahitaji ya bidhaa yake kwenye nchi mbalimbali na ubora unaotakiwa katika soko husika.

✍️ 🎥

13/07/2025

📺: - Raul 🔥🔥

08/07/2025

“Safari ya Mwanamke kuelekea Uchaguzi 2025” ni jukwaa la kitaifa la uhamasishaji, elimu ya uraia, na mazungumzo ya kimaendeleo linalolenga kuongeza ushiriki wa wanawake na vijana, hasa wa k**e, katika mchakato wa uchaguzi na uongozi wa nchi kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Tanzania mwaka 2025.

Tukio hili ni safari ya kipekee ya mafunzo, hamasa, na mshik**ano. Linaibua ari ya wanawake kuelewa haki zao za kiraia, kujiamini kugombea, kushiriki kwenye meza za maamuzi, na kutoa sauti kwa ndoto na dira ya kizazi kipya kuhusu uongozi, haki, na maendeleo ya taifa.

Lengo Kuu ni Kuhamasisha wanawake na vijana kushiriki kwa ujasiri na maarifa katika mchakato wa kidemokrasia k**a wapiga kura, wagombea wa nafasi za uongozi, waangalizi wa uchaguzi, waelimishaji rika, na viongozi wa mabadiliko katika jamii zao.

Anakaribisha kila mwanamke, kila kikundi, kila taasisi, na kila mdau kujiunga na Safari hii tukio litakalofanyika julai 9 mwaka huu pale SUPER DOME Masaki Jijini Dar Es Salaam

03/07/2025

AFISA Tawala Mkuu kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Flora Mgonja amewataka Waajili kuweka mazingira rafiki makazini ili wafanyakazi wapende kazi na kushawishika kwenda kazini.

Pia amewataka kutoa motisha mahali pa kazi ili wafanyakazi hao wazidi kujituma katika kazi na kuhakikisha wanavutiwa nayo.

Akizugumza hayo leo jijini Dar es Salaam,Afisa huyo Tawala ,Mgonja wakati wa kikao kazi kati ya Chama Cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa (TALGWU) pamoja na Waajili waliopo katika Mamlaka ya Serikali za Mitaa.

Mgonja amesema waajiri waliopo katika mamlaka mbalimbali wanatakiwa kuwakumbusha maafisa utumishi na wakurugenzi kuhusu kuwafuatilia na kuwafahamu wafanyakazi wao ili wajue jinsi ya kuwasiliana nao na kutatua matatizo yao.

"Maafisa utumishi na wakurugenzi jambo kubwa sana la umuhimu ni kuwafahamu watumishi wetu unaweza ukamuona mtu kila siku anachelewa kazini kumbe ana matatizo ambayo anapaswa kusikilizwa.

"Tunatakiwa kujua ni namna gani tunaweza kuweka mazingira bora ya watu,wapo watumishi ambao wanaamka asubuhi hawatamani kwenda kazini kwa sababu ya maafisa rasilimali watu,wakurugenzi ipo sehemu anaitwa Mungu mtu hii inamfanya mtu achukie kazi,"amesema Mgonja.

Amesema ni muhimu kwa kila ofisi kuweka mazingira mazuri ya kazi ili mtumishi akiamka atamani kufanya kazi na kuja kazi.

Awali Naibu Katibu Mkuu TALGWU Wandiba Ngocho amesema chama chao ndiyo chama ambacho kinatetea wafanyakazi waliopo chini ya mamlaka ya serikali za mitaa ukiacha walimu kuna kundi kubwa la tunaowatetea.

"Kitu muhimu kinafanywa na chama ni kuwafanya wafanyakazi kuwa karibu sana na wanachama wake,ni utaratibu wetu k**a chama tunakutana na wadau hawa kila mwaka mwisho wa siku hii ni k**a kioo tunajitathimini kila mwaka.

"Tumefanya hii kila mikoa lakini leo ni zamu ya mkoa wa Dar es Salaam,tunawashukuru waajiri pamoja na changamoto nyingi lakini tuna uhusiano mzuri,"amesema Ngocho.

Amesema chama huwa kina utaratibu wa mazungumzo wanakaa wanaongea na waajiri pia kuna watendaji wa mitaa vijiji
tunataka wafanye kazi kwakutumia kanuni na utaratibu.

16/06/2025

K**a wewe ni mpenzi wa movies kali Obvious umeshapita na hii mizigo STRAW & ACRIMONY ambazo Director na mwandishi ni mmoja pia main character ni mmoja Taraji P Henson na upande wa story line ni k**a inashabihiana.

Tuambie kwenye Comment ni movie gani kati ya hizi ni kali kuzidi nyingine?.

Usikose kutazama W-Movies kila siku ya jumatatu, alhamisi na jumamosi saa 1:45 usiku kupitia

Cc


12/06/2025

Leo kwenye W-Movies tupo na movie ya Jahari, Movie ambayo ilimfanya mwanadada kung'aa zaidi kwa kipindi kile, Ila cha kushangaza baada ya hapo akawa kimya kwa muda mrefu sana.

Kupitia WMovies amefunguka ni kitu gani kilisababisha ukimya huo

USIKOSE Kutazama W-Movies kila Jumatatu, Alhamis Na Jumamosi Saa 1:45 Usiku Kupitia 📺

With

Address


Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Wasafi TV posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Shortcuts

  • Address
  • Alerts
  • Claim ownership or report listing
  • Want your business to be the top-listed Media Company?

Share