Jamhuri Digital

  • Home
  • Jamhuri Digital

Jamhuri Digital The official page of Jamhuri Media Company
Wanapoishia Wengine

23/07/2025

UJENZI WA DARAJA LA MTO ITEMBE, MEATU WAFIKIA ASILIMIA 85

Na Berensi China, JamhuriMedia – Meatu

Ujenzi wa daraja kubwa la Mto Itembe, linalounganisha Wilaya ya Meatu mkoani Simiyu na Mkalama mkoani Singida, umefikia asilimia 85 na umeleta faraja kwa wananchi walioteseka kwa muda mrefu kutokana na changamoto za usafiri hasa wakati wa mvua.

Wananchi wa maeneo hayo wamesema wamekuwa wakikumbana na kero kubwa ya kutoweza kuvuka mto kwa siku kadhaa, hali iliyosababisha vifo vya watu, mifugo na uharibifu wa mali. Wameishukuru serikali na Wakala wa Barabara (TANROADS) kwa kusimamia ujenzi huo, huku wakifurahishwa na ukweli kuwa kazi hiyo inatekelezwa na mkandarasi mzawa.

Mkandarasi anayejenga daraja hilo ni kampuni ya RockTronick, ambapo msimamizi wa mradi huo, Eng. Emanuel Kisanga, amesema ujenzi huo wenye urefu wa mita 150 ulisimama kwa miezi saba kutokana na ukosefu wa fedha, lakini hivi karibuni malipo yamepatikana na wanatarajia kumaliza kazi hiyo ifikapo Septemba mwaka huu.

Kwa upande wake, Mhandisi Raphael Chasama kutoka TANROADS Simiyu amesema mradi huo umegharimu Shilingi bilioni 8.4 na utakamilika kwa viwango vya juu. Aidha, daraja hilo litaunganisha mikoa ya Singida, Simiyu, Manyara, Arusha na Mwanza, hivyo kurahisisha usafiri na uchumi wa wananchi.

“Tunaipongeza serikali kwa kutoa fedha na kutuwezesha kutumia wakandarasi wazawa wenye uwezo mkubwa wa kufanya kazi bora nchini,” alisema Chasama.

Bodaboda, Bajaji Wamlilia Mkuu wa Mkoa ArushaNa Zulfa Mfinanga, JamhuriMedia – ArushaJiji la Arusha linakumbwa na changa...
23/07/2025

Bodaboda, Bajaji Wamlilia Mkuu wa Mkoa Arusha
Na Zulfa Mfinanga, JamhuriMedia – Arusha

Jiji la Arusha linakumbwa na changamoto ya msongamano wa vyombo vya moto k**a bodaboda, bajaji na guta, hali inayozua changamoto za usalama na mazingira ya kazi kwa madereva wake.

Wakizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Kenan Kihongosi, katika mkutano uliofanyika uwanja wa Sheikh Amri Abeid, madereva hao walieleza masikitiko yao kuhusu ukosefu wa vituo vya kudumu vya maegesho na mazingira duni ya kazi.

Katibu wa Umoja wa Waendesha Bodaboda Mkoa wa Arusha, Hakimu Msemo, alisema idadi kubwa ya bodaboda haina leseni, hali inayochangia ajali na kuharibu taswira ya sekta hiyo.

“Tuna zaidi ya bodaboda 24,000, lakini wengi hawana elimu ya udereva. Tunaomba serikali itoe tamko dhidi ya wanaofanya kazi bila leseni na pia kutoa mafunzo kwao,” alisema Msemo.

Kwa upande wake, Katibu wa Waendesha Bajaji Mkoa wa Arusha, Salim Lyimo, alieleza kuwa vituo walivyopewa vipo mbali na huduma muhimu k**a masoko na hospitali, jambo linalowapunguzia wateja.

"Tunazo bajaji zaidi ya 3,500 lakini maeneo ya kupaki ni machache na hayafai kibiashara. Tunaiomba serikali itupatie vituo bora na kutoa kipaumbele kwa wenye leseni na makundi maalum," alisema.

Hata hivyo, wadau wa maendeleo na utalii wameendelea kuishauri serikali kudhibiti ongezeko la vyombo vidogo vya usafiri katikati ya jiji kwa madai kuwa vimepunguza mvuto wa Arusha k**a lango la utalii.

Wakizungumza na Jamhuri, wadau hao walipendekeza kupunguza bajaji na bodaboda k**a ilivyofanyika Dar es Salaam ili kupunguza msongamano na uchafu.

Meneja wa LATRA Mkoa wa Arusha, Omary Ayoub, alisema kwa mujibu wa kanuni, ni bajaji 800 tu zinazotakiwa kuwepo katikati ya jiji, lakini hadi sasa zipo zaidi ya 3,000.

Alieleza ongezeko hilo linachangiwa na bajaji kutoka mikoa jirani k**a Kilimanjaro, Dodoma na Manyara.

Kutatua hilo, LATRA imeanzisha mchakato wa kuondoa hiace na kusajili mabasi makubwa yenye uwezo wa kubeba abiria wengi. Lengo ni hadi 2026, asilimia 80 ya daladala ndogo ziwe zimeondolewa katikati ya jiji.

“Tayari coaster zimeanza kuchukua nafasi ya hiace kwenye barabara ya Moshi-Arusha. Tunataka Arusha iwe jiji lenye usafiri wa kisasa,”

Mtoto wa Darasa la Pili Ajinyonga Baada ya Kuiga Maudhui ya Chaneli ya KIX Jijini ArushaMwanafunzi wa darasa la pili kat...
22/07/2025

Mtoto wa Darasa la Pili Ajinyonga Baada ya Kuiga Maudhui ya Chaneli ya KIX Jijini Arusha

Mwanafunzi wa darasa la pili katika Shule ya Msingi Imani na mkazi wa Kata ya Osunyai, Jijini Arusha, aitwaye Karim Rahim (9), amefariki dunia kwa madai ya kujinyonga kwa kutumia kipisi cha kitambaa cha dera, baada ya kutazama maudhui ya chaneli ya KIX na kujaribu kuyaiga akiwa nyumbani kwao.

Kwa mujibu wa taarifa, tukio hilo lilitokea majira ya saa tisa alasiri Julai 20, 2025, ambapo inaelezwa kuwa Karim alimaliza kutazama chaneli hiyo kisha kuingia chumbani akiwa amebeba kashata – vitafunwa ambavyo hupendwa sana na watoto.

Baada ya kuingia chumbani, Karim alifungua dirisha na kuwaona watoto wa jirani, akaanza kuwagawia kashata huku wakiendelea kuzungumza. Dirisha hilo linaelezwa kuwa lilikuwa limefungwa kwa kutumia kipisi cha kitambaa cha dera kutokana na kitasa chake kuwa kimeharibika.

Mama mkubwa wa Karim, Bi. Amina Daudi, amesema kuwa alisikia sauti ya mtoto huyo akiwa anaongea na wenzake, lakini ghafla alipokuwa akimwaga maji ya kudekia, alimuona Karim akiwa amenasa shingoni na kuning’inia pembezoni mwa dirisha.

Amina alipiga yowe, akaingia ndani na kukata kipande cha kitambaa hicho, kisha Karim alikimbizwa katika Hospitali ya Levolosi, lakini madaktari walithibitisha kuwa tayari alikuwa amefariki dunia.

Watoto waliokuwa wakizungumza na Karim walieleza kwa mshangao kuwa walimuona tu "kageukia huko", ishara kuwa tukio hilo lilitokea kwa ghafla bila wao kuelewa kilichokuwa kinaendelea.

Familia ya Karim imekiri kuwa mtoto huyo alikuwa na tabia ya kutazama chaneli ya KIX kwa muda mrefu, na huenda alijaribu kuiga baadhi ya maudhui yanayoonyeshwa kwenye chaneli hiyo, ambayo hulenga watu wenye umri wa miaka 18 hadi 45, na huhusisha mapigano, mashindano ya nguvu, na matukio ya kihatarishi.

Kwa sasa, tunasubiri taarifa rasmi kutoka kwa Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha kuhusu uchunguzi wa kina wa tukio hilo ili kubaini k**a kuna maelezo zaidi au tofauti na yaliyotolewa.

---

Chanzo: GADI TV

19/07/2025
Wanaume watatu wa Nigeria walik**atwa katika uwanja wa ndege nchini Algeria baada ya kujaribu kupanda ndege kuelekea Dub...
17/07/2025

Wanaume watatu wa Nigeria walik**atwa katika uwanja wa ndege nchini Algeria baada ya kujaribu kupanda ndege kuelekea Dubai wakiwa wamejigeuza kuwa wanawake wa Kiarabu.

Kundi hilo lilivalia mavazi ya kitamaduni, hijabu na vipodozi vizito katika juhudi za kupita katika usalama bila kutambuliwa. Maafisa walishuku na kufichua udanganyifu huo haraka wakati wa uchunguzi wa kawaida.

Ingawa sababu kamili za kujaribu kusafiri kwa siri hazikuwahi kufichuliwa hadharani, tukio hilo lilizua taharuki katika vyombo vya habari vya Afrika Kaskazini-na kuwaacha wengi wakihoji ni umbali gani watu wako tayari kutoroka au kuanza upya.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akisikiliza maelezo kuhusu habari za uchunguzi...
15/07/2025

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akisikiliza maelezo kuhusu habari za uchunguzi kutoka kwa Mhariri Mtendaji wa Gazeti la JAMHURI ambaye pia ni Mkurugenzi Mwenza wa JAMHURI Media Ltd., Bw. Deodatus Balile wakati akikagua mabanda ya maonesho katika Mkutano wa Mabaraza Huru ya Habari Afrika unaofanyika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC). Tarehe 15 Julai 2025.

Tukio hilo ni sehemu ya Mkutano wa Mabazara Huru ya Habari Afrika (NIMCA), ambao umewaleta pamoja wadau mbalimbali wa se...
15/07/2025

Tukio hilo ni sehemu ya Mkutano wa Mabazara Huru ya Habari Afrika (NIMCA), ambao umewaleta pamoja wadau mbalimbali wa sekta ya habari kutoka pembe zote za bara hili.

Polepole Ajiuzulu Ubalozi: Aeleza Sababu, CCM YajibuAliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Cuba, Humphrey Polepole, ametang...
13/07/2025

Polepole Ajiuzulu Ubalozi: Aeleza Sababu, CCM Yajibu

Aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Cuba, Humphrey Polepole, ametangaza kujiuzulu nafasi yake rasmi tarehe 13 Julai 2025, hatua iliyozua mjadala mkubwa ndani na nje ya Chama Cha Mapinduzi (CCM). Kupitia barua yake ya kujiuzulu iliyosambaa mitandaoni, Polepole ameeleza kuwa amepoteza amani ya moyo na imani kwa uongozi wa sasa, akitaja sababu kuu kuwa ni kuzorota kwa maadili ya uongozi, upungufu wa uwajibikaji na ukiukwaji wa haki za watu.

Kulingana na Polepole, baadhi ya misingi ya chama k**a “Chama Kwanza, Mtu Baadaye” imekuwa ikitumiwa vibaya, jambo linalodhoofisha misingi ya demokrasia na utawala bora. Amewataka viongozi walioko madarakani kurejea kwenye misingi ya uadilifu, uwazi na kuheshimu katiba ya chama na nchi kwa ujumla.

Kwa upande wake, CCM kupitia kwa Katibu wa Itikadi na Uenezi, imethibitisha kupokea taarifa za barua hiyo ya kujiuzulu na imeahidi kufanya uchunguzi ili kujiridhisha kuhusu uhalisia wa nyaraka hizo. Chama pia kimetoa wito kwa wanachama kuwa watulivu na kuacha kutoa maneno yenye kuleta migawanyiko hadi ukweli utakapobainika.

Sakata hili limekuja wakati taifa linaelekea katika kipindi cha uteuzi na mchakato wa kuelekea uchaguzi mkuu ujao, hali inayoongeza uzito wa hoja za Polepole kuhusu misingi ya kidemokrasia na haki za wagombea ndani ya chama.

Hadi sasa, wananchi na wachambuzi wa siasa wanafuatilia kwa karibu hatua zitakazochukuliwa na CCM na serikali kufuatia sakata hili, huku Polepole akibaki na msimamo wake wa kusimamia ukweli kwa mujibu wa barua yake.

Kipindi Cha kwanzaChelsea Funny 🤣 woyee
13/07/2025

Kipindi Cha kwanza
Chelsea Funny 🤣 woyee

Mrisho Gambo ameondolewa kwenye mchujo wa ubunge Arusha Mjini kupitia CCM.Paul Makoda ameibuka kidedea na jina lake lime...
12/07/2025

Mrisho Gambo ameondolewa kwenye mchujo wa ubunge Arusha Mjini kupitia CCM.
Paul Makoda ameibuka kidedea na jina lake limepitishwa kuendelea mbele.

Wengi wameshangaa kuona Gambo, mwanasiasa maarufu na mwenye ushawishi, akiachwa nje hatua za awali.
Wafuasi wa Makoda wanasema ni muda wa kizazi kipya chenye maono mapya!

Macho sasa kwa Kamati ya Siasa ya Mkoa na Kamati Kuu ya CCM kwa uamuzi wa mwisho!

Je, unalionaje hili? 👀✨

Wananchi wa jijini Dar es Salaam wakielimishwa kuhusu suluhisho la mapishi kwa kutumia nishati ya umeme, ikiwa ni muende...
09/07/2025

Wananchi wa jijini Dar es Salaam wakielimishwa kuhusu suluhisho la mapishi kwa kutumia nishati ya umeme, ikiwa ni muendelezo wa uzinduzi rasmi wa Kampeni ya Kitaifa ya Uhamasishaji wa Upishi wa Umeme (eCooking) uliofanyika tarehe 13 Juni 2025 jijini Dar es Salaam. Kampeni hii inaendeshwa na Wizara ya Nishati kwa kushirikiana na Programu ya huduma za nishati za kisasa za kupikia (MECS) na Shirika la Maendeleo la Uingereza (UK International Development). Lengo kuu ni kuhamasisha mabadiliko ya tabia na kusaidia kaya za Kitanzania kuachana na kuni na mkaa kuepusha athari za afya na mazingira.

Wakulima wa pamba walipewa pikipiki na waziri  Bashe waahidi kuongeza uzalishaji.Na Berensi china  Bariadi Siku chache b...
04/07/2025

Wakulima wa pamba walipewa pikipiki na waziri Bashe waahidi kuongeza uzalishaji.
Na Berensi china Bariadi

Siku chache baada ya waziri wa kilimo.Husein Bashe kuwazawadia pikipiki wakulima bora wa pamba katika kata ya Dutwa wilayani Bariani mkoani.Simiyu wskulima hao wameahidi kuongeza uzalishaji zaidi ili mwakani waweze pia kupewa zawadi.

Wakiongea na waandishi wa habari za pamba waliotembelea wakulima hao wamesema wamepokea kwa furaha kubwa zawadi hiyo ambayo wamepewa na waziri kwa kutambua juhudi zao

"Siku moja waziri Bashe alipita hapa tukaongea naye na akutuahidi kuwa wakulima watakaozalisha kilo.nyingi atatoa zawadi ingawaje hakuitaja sisi hatukuamini lakini tulishangaa tulipoitwa na kupewa pikipiki hizi ambazo tuliambiwa kuwa ndiyo ahadi ya waziri wa kilimo.aliyotuahidi .kwakweli tumefarijika sana"alisema Saimon Malugu mkulima bora kijiji cha Igaganulwa

Wakulima hao wamesema.mwakani.wamejinga ipasavyo kuhakikisha wanaongeza uzalishaji kwani bodi ya pamba imewaletea maafisa kilimo.wa BBT ambao wamewasaidia kuwapa elimu ya kilimo hicho.

Kwakweli tumeona ambavyo bodi ya pamba imejipanga kutusaidia mwaka Jana tumeona hadi ndege nyuki ambazo zimeletwa kunyunyuzia pamba jambo.tulikuwa hatujaona tangia nchi ipate uhuru hakika haya ni .mapinduzi makubwa katika kilimo hiki maana dawa .pembejeo tumeletewa kwa muda ",,alisema Joshua Malongo mkulima bora wa kijiji cha isenge .
Kwa upande wake mkaguzi wa pamba toka bodi ya pamba wilaya Bariadi Ndinda Anthony.amesema wanahakikisha wakulims wanauza pamba iliyo na ubora ambapo amewataka wakulima kuchsmbua pamba yao kabla hawajaiuza sambamba na kitoweka maji na mchanga kwani kufanya hivyo ni kosa na pia wanaharibu pamba na inachangia kukosa soko kwenye soko la dunia.

Address


Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Jamhuri Digital posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to Jamhuri Digital:

Shortcuts

  • Address
  • Alerts
  • Contact The Business
  • Claim ownership or report listing
  • Want your business to be the top-listed Media Company?

Share