Viola Mtetezi

  • Home
  • Viola Mtetezi

Viola Mtetezi content creator
(1)

🙏
25/06/2025

🙏

Kosa kubwa Tanzania ni kuwa na akili na kufungua macho ya wenzako.Maana yake ni kwamba ukijua ukweli, ukaamua kuufichua,...
21/06/2025

Kosa kubwa Tanzania ni kuwa na akili na kufungua macho ya wenzako.

Maana yake ni kwamba ukijua ukweli, ukaamua kuufichua, na ukawaambia wananchi kuhusu haki zao, mfumo wa hila, au ukiukwaji wa demokrasia — basi unajikuta unalipwa kwa vitisho, kufuatwa usiku, kutekwa, au hata kupotezwa kabisa.

Hii ni ishara ya serikali yenye hofu, inayojua kuwa haiko madarakani kwa ridhaa ya wananchi bali kwa hila, udanganyifu, na nguvu za dola.

Badala ya kusikiliza na kujifunza kutoka kwa wenye maarifa, wao wanachagua kuwanyamazisha. Badala ya kuwalinda wanaosema ukweli, wanawatisha.

Lakini historia inatufundisha hivi:

“Wenye akili waliodhulumiwa ndio wanaoandika historia ya kesho.”


Na siku moja, hata giza nene lina mwisho wake.
Na kila mfumo wa vitisho una mwisho wake.

Waache wanaoogopa akili waendelee kutisha, lakini ukweli haudhibitiwi na risasi wala hofu.
Ukweli ni k**a maji — ukikanyaga, utakuchafua.

Ng'atuka kwenye uchawaNg'atuka kwenye kusifia ujingaNg'atuka kwenye kwenye uongozi mbayaNg'atuka tupambanie katika mpya ...
20/06/2025

Ng'atuka kwenye uchawa
Ng'atuka kwenye kusifia ujinga
Ng'atuka kwenye kwenye uongozi mbaya
Ng'atuka tupambanie katika mpya maana ni msaada kwa Watanzania wote

"Leo hii Tanzania, si kila kiongozi ni mkweli.Wengi wamegeuka kuwa wasemaji wa sifa, hata kwa mambo yasiyofaa.Wanaogopa ...
19/06/2025

"Leo hii Tanzania, si kila kiongozi ni mkweli.
Wengi wamegeuka kuwa wasemaji wa sifa, hata kwa mambo yasiyofaa.
Wanaogopa kusema ukweli kwa sababu mmoja akisemea wananchi, anaweza kupoteza cheo chake.

Wengine wameamua kusifia tu, hata uongo…
Wanapiga makofi, wakijua mioyoni mwao kuna maumivu.
Wananyamaza, wakati wananchi wanalia.

Je, huo ndiyo uongozi tunaoutaka?

Uongozi si cheo cha kuogopwa, ni dhamana ya kuwatumikia watu.
Na kiongozi wa kweli hasifiwi kila siku,
anakosolewa, anasahihisha, na anaheshimu ukweli.

Tanzania inahitaji viongozi wenye ujasiri wa kusema:
'Hili haliko sawa.'
Wenye moyo wa kusema:
'Situmiki kwa maslahi binafsi, natumikia wananchi.'

📢 Ni wakati wa kuamka. Taifa hili ni la wananchi, si la vyeo!

Ee Baba wa mbinguni,Tunakuja mbele zako leo tukiwaweka mikononi mwako watoto wote wa kiume, waliozaliwa na wanaokua kati...
17/06/2025

Ee Baba wa mbinguni,
Tunakuja mbele zako leo tukiwaweka mikononi mwako watoto wote wa kiume, waliozaliwa na wanaokua katika kizazi hiki chenye changamoto.
Tunaomba, Bwana, uwalinde dhidi ya kila shauri ovu, kila mtego wa adui na kila mfumo unaotaka kuwavua utu wao wa kiume.

Wajalie hekima k**a ya Sulemani, moyo wa ujasiri k**a wa Daudi, na utiifu k**a wa Yesu Kristo.
Wafunze kupenda haki, kuwajibika, kuheshimu wanawake, na kuwa viongozi wa kweli katika familia na jamii.

Tunakemea roho ya woga, ya uvivu, ya utegemezi, na ya kujisahau.
Wape maono ya maisha yao, ndoto kubwa, na nguvu ya kuzitimiza kwa juhudi na neema yako.

Tunaomba wazazi na walezi wawalee katika njia impasayo mtoto wa kiume, ili hata atakapokua asiache njia hiyo.
Naomba uwainue wanaume wa kiroho, wa kimwili na wa kiakili kupitia watoto hawa—watoto ambao watazaliwa kuwa baraka, si laana.

Katika jina la Yesu Kristo tunaomba,
Amina. 🙏

Binti ake na Mama angu🤗
17/06/2025

Binti ake na Mama angu🤗

Mungu hahitaji kulindwa, lakini anapaswa kuheshimiwa. Na kati ya vitu vyote duniani, usithubutu kugusa nyumba yake. Leo ...
15/06/2025

Mungu hahitaji kulindwa, lakini anapaswa kuheshimiwa. Na kati ya vitu vyote duniani, usithubutu kugusa nyumba yake. Leo mnaweza kuwa na virungu, silaha, na mamlaka ya muda, lakini kumbukeni: Mamlaka yote hutoka kwa Mungu, na k**a mnaweza kufunga kanisa leo, kesho Mungu anaweza kufunga maisha yenu.

Nyumba ya Bwana ni mahali pa sala, pa rehema, pa uponyaji – na si uwanja wa siasa, si mahali pa hila, wala si pa kebehi. Msidhani kwa kuzuia watu kusali au kufungia ibada kuwa mmezuia kazi ya Mungu. Yeye huja k**a kimbunga kisichozuilika, na mara nyingi huanza kwa wale waliovunja heshima ya madhabahu yake.

Msicheze na moto wa kiroho.

Ukiweza kuchezea serikali, usichezee madhabahu. Mungu anaweza kukuvumilia kwa muda, lakini siku atakapoamka kwa hasira, hakuna atakayemzuia. Si jeshi, si cheo, si hila – maana yeye ni Mungu mwenye wivu.

Acheni watu wasali. Acheni watu wamwabudu Mungu wao. Usiguse nyumba ya Bwana k**a hujataka kuanguka kwa nguvu zake.

"Kwa maana Bwana Mungu ni moto ulao." (Kumbukumbu la Torati 4:24)

Mungu hadhihakiwi – na madhabahu yake ni takatifu.

Address


Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Viola Mtetezi posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Shortcuts

  • Address
  • Alerts
  • Claim ownership or report listing
  • Want your business to be the top-listed Media Company?

Share