Watetezitv

Watetezitv WATETEZI TV is a Not-For-Profit online Tv under the Tanzania Human Rights Defenders Coalition(THRDC). Watetezi Tv operates in lieu of all applicable laws.

It will not be responsible to any subscriber who will post anything contrary to the applicable laws

Mahak**a ya Hakimu Mkazi Wilaya ya Lindi, imemhukumu kifungo cha miaka 30 jela Alli Ibrahimu Malinda (30), mkazi wa Kiji...
23/07/2025

Mahak**a ya Hakimu Mkazi Wilaya ya Lindi, imemhukumu kifungo cha miaka 30 jela Alli Ibrahimu Malinda (30), mkazi wa Kijiji cha Ng’apa, baada ya kupatikana na hatia ya kumbaka mtoto wake wa kumzaa mwenye umri wa miaka 10. Hukumu hiyo imetolewa Julai 23, 2025 na Hakimu Mkazi Delphina Kimathi, baada ya ushahidi wa upande wa mashtaka kuthibitisha kosa hilo pasipo shaka yoyote.

Kwa mujibu wa hati ya mashtaka, tukio hilo lilitokea Januari 6, 2025, usiku katika kijiji cha Ng’apa, wakati mtoto huyo akiwa usingizini. Malinda alitumia nafasi yake k**a mzazi vibaya na kutenda kitendo hicho cha unyama ndani ya nyumba yao ya familia.

Akisoma hukumu hiyo, Hakimu Kimathi alisema kuwa ushahidi uliotolewa mahak**ani ulionyesha wazi kuwa mshtakiwa alitenda kosa hilo la ukatili wa kingono dhidi ya mtoto wake, na kwamba mahak**a haiwezi kuvumilia matendo k**a hayo yanayohatarisha ustawi na haki za watoto.

Upande wa Jamhuri ukiongozwa na Wakili wa Serikali Denis Nguvu, uliiomba mahak**a kutoa adhabu kali kwa mshtakiwa ili iwe fundisho kwa watu wengine wenye tabia k**a hizo. Katika uamuzi wake, mahak**a ilisema adhabu hiyo ni sahihi kwa kuzingatia uzito wa kosa na madhara aliyoyapata mtoto huyo.

"Wananchi wawe na imani na jeshi lao, na Mkuu wa Jeshi la Polisi, IGP Camilius Wambura anafuatilia sana suala la nidhamu...
22/07/2025

"Wananchi wawe na imani na jeshi lao, na Mkuu wa Jeshi la Polisi, IGP Camilius Wambura anafuatilia sana suala la nidhamu, uweledi, uadilifu na haki za wananchi kuliko watu wanavyofuatilia na sisi mak**anda tuna wajibu wa kuhakikisha maaskari wetu wanafanya kazi kwa mujibu wa sheria lakini pia ikitokea watu wanafanya makosa tunarudi kwenye katiba kunakuwa na usawa mbele ya sheria. Neno langu wananchi wa Dar es Salaam tuendelee kushirikiana na wadau wengine"-

SACP, Muliro Jumanne - Kamanda wa Polisi, Kanda Maalumu ya DSM alipozungumza na kituo cha Clouds Tv leo Julai 22,2025.

Dodoma, Julai 21, 2025 Jeshi la Polisi mkoani Dodoma linawashikilia askari wake wawili kwa tuhuma za kumuua kwa risasi r...
21/07/2025

Dodoma, Julai 21, 2025
Jeshi la Polisi mkoani Dodoma linawashikilia askari wake wawili kwa tuhuma za kumuua kwa risasi raia mmoja aitwaye Frank Sanga, aliyefariki dunia Julai 19, 2025, katika eneo la Ntyuka, jijini Dodoma.

Tukio hilo lililotokea majira ya saa 8:00 mchana limeelezwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, ACP Agathon Hyrera, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari leo. Kamanda Hyrera amesema kuwa Frank Sanga alik**atwa na askari hao akiwa anaendesha pikipiki bila leseni, bila kuvaa kofia ya usalama, huku akiwa amebeba magunia matatu ya mkaa.

Baada ya kuk**atwa, marehemu alidai kuwa hawezi kwenda kituoni bila uwepo wa ndugu zake. Ndugu hao walipofika kwa pikipiki tatu zilizobeba abiria zaidi ya wawili kila moja, walidai kukabidhiwa funguo ya pikipiki na kuachiwa Frank.

Mvutano ulizuka kati yao na askari, na hali hiyo iligeuka kuwa ya mvutano baada ya baadhi ya ndugu hao kuwashambulia askari. Kamanda Hyrera amesema kuwa askari mmoja alifyatua risasi hewani kwa lengo la kuwatisha, lakini alipodondoka chini baada ya kushambuliwa kwa fimbo, mzozo uliendelea na ndipo risasi ikamfikia Frank Sanga na kusababisha kifo chake.

Jeshi la Polisi limesema kuwa uchunguzi wa kina unaendelea na limeahidi kuwajibisha wote watakaobainika kwenda kinyume cha sheria.

Idara ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) nchini Kenya imeondoa rasmi mash*taka ya ugaidi dhidi ya mwanaharakati maaru...
21/07/2025

Idara ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) nchini Kenya imeondoa rasmi mash*taka ya ugaidi dhidi ya mwanaharakati maarufu wa haki za binadamu, Boniface Mwangi, ambaye sasa anakabiliwa na shtaka moja la kumiliki risasi kinyume cha sheria.

Kwa mujibu wa taarifa za mahak**a, Mwangi amechiwa kwa dhamana baada ya kufikishwa mbele ya hakimu jijini Nairobi leo, kufuatia kuk**atwa kwake Jumamosi iliyopita katika makazi yake ya Lukenya, Kaunti ya Machakos. Awali, DCI ilimshutumu kwa kusaidia shughuli za kigaidi wakati wa maandamano ya kitaifa ya kupinga serikali ya Rais William Ruto yaliyofanyika tarehe 25 Juni 2025.

Katika hati ya mashtaka mpya, DCI inadai kuwa uchunguzi wa awali ulibaini Mwangi alikuwa na ganda la risasi kinyume cha sheria, lililokutwa katika ofisi yake eneo la Kilimani, Nairobi, wakati wa upekuzi uliofanyika mara baada ya kuk**atwa kwake.

Wakili wa Mwangi, James Kamau, amesema kuwa mashtaka haya mapya yanaonyesha kuwa hakuna ushahidi wa kutosha uliounganisha mteja wake na madai ya ugaidi, na kwamba hatua ya kuondoa shtaka hilo ni ushindi wa haki na ushahidi wa shinikizo la umma.

Mashirika ya haki za binadamu yamepongeza uamuzi huo wa kuondoa shtaka la ugaidi, lakini bado yanaitaka serikali ya Kenya kuhakikisha kuwa inazingatia sheria na due process wakati wa kushughulikia wanaharakati na wapinzani wa kisera.

Kwa sasa, Mwangi yupo huru kwa dhamana akisubiri tarehe ya usikilizwaji wa kesi ya umiliki haramu wa risasi, huku mashirika mbalimbali ya kiraia yakiendelea kufuatilia mwenendo wa kesi hiyo kwa karibu.

Na Herrieth Molla, IringaWatu watatu wamefariki dunia na wengine sita kujeruhiwa katika ajali mbaya ya barabarani iliyot...
18/07/2025

Na Herrieth Molla, Iringa

Watu watatu wamefariki dunia na wengine sita kujeruhiwa katika ajali mbaya ya barabarani iliyotokea asubuhi ya Julai 18, 2025 katika Kijiji cha Imalutwa, Kata ya Lugalo, Tarafa ya Mazombe, Wilaya ya Kilolo mkoani Iringa.

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Iringa, (SACP) Allan Bukumbi, amesema ajali hiyo ilihusisha basi dogo la abiria aina ya Fuso Mini Bus lenye namba za usajili T 562 EBK linalomilikiwa na Khatibu Kihwelo. Gari hilo lilikuwa likiendeshwa na dereva Akhan Mpagile (45), mkazi wa Njombe, ambaye ni miongoni mwa waliopoteza maisha.

Kwa mujibu wa SACP Bukumbi, watu wengine waliopoteza maisha ni Alfred Mgaya, mkazi wa Njombe ambaye alikuwa utingo wa basi hilo, pamoja na Feleschina Masigati (36), mkazi wa Imalutwa aliyekuwa abiria.

Kamanda Bukumbi alieleza kuwa ajali hiyo ilitokea baada ya basi hilo kugonga kwa nyuma lori lenye namba T 857 DVZ na Trela T 460 EAM aina ya Howo, mali ya kampuni ya Glenrich Transportation Co. Ltd, ambalo lilikuwa likitokea Dar es Salaam kuelekea Iringa likibeba mzigo wa unga.

Aidha, chanzo cha ajali hiyo kimeelezwa kuwa ni uzembe wa dereva wa basi, ambaye alishindwa kulimudu gari na kugonga lori lililokuwa limesimama mbele yake.

Majeruhi sita wa ajali hiyo wamepelekwa katika vituo vya afya kwa ajili ya matibabu, huku uchunguzi zaidi ukiendelea.

Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) imewafungia kuendelea na kazi za kihabari watangazaji wa kituo cha redio c...
18/07/2025

Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) imewafungia kuendelea na kazi za kihabari watangazaji wa kituo cha redio cha Mjini FM baada ya kubainika kuvunja Sheria na Kanuni za taaluma ya habari.

JAB imewataja watangazaji Deodatha William, M***a Crispin Mgenge(Perfect Crispin ) na Iddy Bakari Iddy ambao waliongoza kipindi cha GENGE LA GEN wakimhoji dogo Patern kupitia kipindi hicho kilichorushwa Julai 16, 2025.

Katika sababu zake Bodi hiyo kupitia taarifa yake imesema waliotajwa hapo juu hawajasajiliwa kisheria kufanya kazi za kihabari na walikiuka maadili kwa kutumia lugha za kudhalilisha na kumlazimisha mgeni kutoa taarifa binafsi.

Bodi hiyo imeandika kuwa kuanzia leo 18 Julai 2025, watangazaji hao wamefungiwa kushiriki shughuli yoyote ya kihabari hadi pale watakapopata ithibati na kuzingatia maadili ya taaluma ya habari.

Bodi imeonya vyombo vyote vya habari kuhakikisha waandishi na watangazaji wao wanakuwa na Ithibati kabla ya kuruhusiwa kuendesha vipindi.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, ametoa wito kwa Mahak**a na taasisi zote zinazohusika na u...
17/07/2025

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, ametoa wito kwa Mahak**a na taasisi zote zinazohusika na utoaji wa haki nchini kutekeleza majukumu yao kwa uadilifu, usawa na bila upendeleo, sambamba na maelekezo mapya ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025-2050.

Akihutubia leo Alhamisi Julai 17,2028 katika Ukumbi wa Jakaya Kikwete, Dodoma, wakati wa uzinduzi rasmi wa Dira hiyo, Rais Samia amesema mwelekeo mpya wa taifa unasisitiza kwa kina kulinda haki, maadili na utamaduni wa Mtanzania k**a misingi ya maendeleo endelevu.

“Dira imeweka msisitizo wa kipekee katika suala la haki, na vilevile katika kulinda maadili na utamaduni wa Tanzania. Haya ni maeneo muhimu kwa ustawi wetu k**a taifa,” amesema Rais Samia.

Aidha, amekumbusha kuwa Mahak**a na taasisi nyingine za utoaji haki zina jukumu la kuhakikisha haki inatendeka bila huba, chuki, wala upendeleo, kwa mujibu wa viapo vyao vya kiutumishi.

“Nitoe wito kwa Mahak**a na taasisi zote husika katika utoaji haki kutimiza wajibu wao bila upendeleo, huba wala chuki – au uonevu wa mtu yoyote,” amesisitiza.

Dira hii mpya ya Maendeleo 2025-2050 imekuja kufuatia kutimia kwa Dira ya awali ya Maendeleo ya Taifa 2025, na inalenga kuweka msingi imara wa maendeleo ya kijamii, kiuchumi na kimaadili kwa miongo ijayo.

Baada ya kipindi kirefu cha ukimya na kutojitokeza katika matukio makuu ya kitaifa na shughuli za kisiasa nchini, aliyek...
17/07/2025

Baada ya kipindi kirefu cha ukimya na kutojitokeza katika matukio makuu ya kitaifa na shughuli za kisiasa nchini, aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mheshimiwa Freeman Mbowe, ameonekana hadharani leo Alhamisi, Julai 17, 2025 jijini Dodoma katika Uzinduzi wa Dira ya taifa ya maendeleo 2050.

Mbowe ni miongoni mwa Watanzania na wageni mashuhuri wanaohudhuria uzinduzi unaofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete, jijini Dodoma.

Tukio hili ni la kihistoria na hufanyika kila baada ya miaka 25.

Mgeni rasmi katika hafla hiyo ya kitaifa ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, anatarajiwa kuandika historia leo, Alhamisi Julai 17,...
17/07/2025

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, anatarajiwa kuandika historia leo, Alhamisi Julai 17, 2025, kwa kuzindua rasmi Dira Mpya ya Maendeleo ya Taifa ya Mwaka 2050, katika Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete, jijini Dodoma.

Uzinduzi huo utamfanya Rais Samia kuwa Rais wa Pili wa Tanzania kuzindua Dira ya Maendeleo ya Taifa, baada ya Hayati Benjamin William Mkapa aliyezindua Dira ya Taifa ya 2025 mnamo mwaka 2000.

Kwa mujibu wa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Mipango na Uwekezaji, Prof. Kitila Mkumbo, Dira ya Maendeleo ya 2050 ni ya aina yake kwa kuwa imeandaliwa kwa ushirikishwaji mpana zaidi wa wananchi, ambapo takribani wananchi milioni 1.17 walihusishwa moja kwa moja, zaidi ya 20,000 walishiriki katika makongamano ya kitaaluma na mikutano ya wadau, na wengine wengi walitoa maoni yao kupitia tovuti maalum ya Tume ya Taifa ya Mipango.

Aidha, Dira hii imeidhinishwa na Baraza la Mawaziri, na kwa mara ya kwanza katika historia ya nchi, Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limeridhia dira hiyo k**a hatua ya kuiwekea kinga ya utekelezaji wake kwa kipindi chote cha miaka 25 ijayo, bila kujali mabadiliko ya serikali au itikadi za vyama vya siasa.

“Kwa mara ya pili, nchi yetu inapata Dira ya Maendeleo ya Taifa isiyoegemea upande wowote wa kiitikadi ya chama cha siasa. Rais Samia Suluhu Hassan anakuwa Rais wa Pili kuandika na kuzindua Dira ya Taifa,” amesema Prof. Kitila.

Takwimu zinaonesha kuwa asilimia 81 ya waliotoa maoni kuhusu Dira hii ni vijana wenye umri kati ya miaka 15 hadi 35, jambo linaloashiria hamasa kubwa ya kizazi kipya katika mustakabali wa taifa.

Akizungumzia tathmini ya Dira ya Taifa ya 2025, Prof. Mkumbo ameeleza kuwa:
• Asilimia 69 ya Watanzania wanaamini nchi iko katika mwelekeo sahihi,
• Na asilimia 76 wana imani kuwa Tanzania ya mwaka 2050 itakuwa na ustawi mkubwa katika sekta mbalimbali.

Tume ya Taifa ya Mipango imesema kuwa zaidi ya wageni 5,000 kutoka ndani na nje ya nchi wakiwemo viongozi wa serikali, taasisi binafsi, wadau wa maendeleo, na mashirika ya kimataifa wanatarajiwa kushuhudia tukio hilo la kihistoria.

The European Union Ambassador to Tanzania, Christine Grau, has firmly rejected accusations that the EU has remained sile...
17/07/2025

The European Union Ambassador to Tanzania, Christine Grau, has firmly rejected accusations that the EU has remained silent as democratic space in the East African country continues to shrink.

Speaking with Watetezi TV, Grau insisted that the EU delegation in Tanzania has been consistently engaging the government on issues related to human rights and the rule of law, including the controversial arrest and treason charges against opposition figure Tundu Lissu.

“The European Union ambassador and the ambassadors of EU Member States remain actively engaged and have been clearly expressing their concern to the government on all questions of respect of Human Rights and rule of law, including on the arrest and ongoing trial of Tundu Lissu,” Grau said.

Her comments come days after members of the European Parliament sharply criticized the EU’s perceived inaction in Tanzania, accusing the delegation in Dar es Salaam of failing to publicly denounce escalating repression under President Samia Suluhu Hassan’s government.

Onesmo Ole Ngurumwa, the National Coordinator of the Tanzania Human Rights Defenders Coalition (THRDC), welcomed Grau’s statement as a “sign of meaningful solidarity at a critical moment for democracy.”

“We sincerely appreciate the role of the European Union in standing with the people of Tanzania and with human rights defenders across Africa,” Ngurumwa said. “Their expression of concern over shrinking democratic space, and their insistence on the rule of law, shows that they are not silent partners—they are truly engaged.”

Ngurumwa further acknowledged the quiet but strategic diplomacy at play. “Despite criticism from MPs, I understand that the EU mission and some few other EU member states with presence in Tanzania have been closely and strategically engaging the government on the current trends of human rights and democracy in Tanzania, including some of them attending Tundu Lissu court cases,” he said.

During a heated parliamentary session in May, German MEP Michael Gahler, a member of the European People's Party and a long-time advocate for democratic governance in Africa, took the EU delegation to task for what he described as "calm and silent" diplomacy in the face of blatant human rights abuses.

“In an election where the main contestants are not allowed to stand, we cannot finance it, and we should not send an election observation mission because we know the result in advance,” Gahler said on the Parliament floor.

“Our ambassador on the ground must take the floor and speak out publicly. It’s not about our standards — it’s about their own standards, their own legislation.”

Gahler went further to express frustration over the EU’s failure to respond when a European foreign minister visited Tanzania and praised the situation, despite the imprisonment of opposition leaders and the stifling of civil society.

“That is not acceptable,” he said. “Then we should stop pretending that we have any values at all if we watch African countries violate their own laws and remain silent.”

On May 8, 2025, the European Parliament passed a resolution condemning Tanzania’s political environment and specifically calling for the immediate release of Chadema opposition leader Tundu Lissu. The resolution, adopted with cross-party support, labeled the treason charges against Lissu as politically motivated and called on the Tanzanian authorities to allow all opposition parties to freely participate in the upcoming October 2025 elections.

The European Parliament’s message was unequivocal: no EU funding should be released — including the €8 million in support for the electoral process — unless all candidates are allowed to contest freely.

“We are the European Union,” Gahler said. “We must act like it.”

Ngurumwa underscored the importance of this principled approach.

“The EU has consistently supported different initiatives—be it through strengthening civil society, advising on governance reforms, or backing the rule of law,” he noted. “This kind of partnership matters deeply, especially now, when the political atmosphere in Tanzania is tense and democratic values are being tested.”

President Samia’s government has pointed to the recent formation of the Independent National Electoral Commission, revived political dialogue, and expanded media freedoms as evidence of progress.

But human rights observers and opposition groups argue that these measures are cosmetic at best. They note that while political rhetoric has shifted, repressive laws remain intact and opposition parties continue to face systematic harassment.

Ambassador Grau’s defense highlights the EU’s struggle to walk a fine line between quiet diplomacy and public condemnation. While the EU has traditionally avoided direct confrontation with African governments, the growing outcry from the European Parliament suggests that patience is wearing thin.

Analysts say the latest developments could force the EU to recalibrate its engagement with Tanzania.

“We appreciate that the EU, through its institutions and ambassador, has chosen to speak out while also continuing to engage the government constructively,” says Ole Ngurumwa.

The EU Parliament’s resolution also placed Tanzania’s situation within a broader African context, citing an “alarming decline of democracy” across the continent.

“An even more corrosive threat is emerging — the systematic breakdown of democratic institutions and values,” said one lawmaker. “Opposition politicians are being excluded from elections, critics jailed, and civil society space is shrinking.”

Tanzania was listed alongside Côte d’Ivoire as a country where opposition politicians have been unfairly sidelined and democratic processes manipulated.

The EU Parliament emphasized that such trends have severe implications not only for governance but also for regional stability and youth engagement.

“Citizens, especially the youth, face disillusionment as promises of democratic governance crumble,” the resolution warned.

With Tundu Lissu’s treason trial expected to resume later this month, the stakes are high for Tanzania’s image abroad. The government’s handling of the case could either validate claims of political persecution or offer a chance for genuine reconciliation.

Meanwhile, the EU will be closely monitoring developments — not just as a donor, but as a stakeholder in Tanzania’s democratic future.

“What pains me most is that we often wait until the pressure comes from outside before we act,” Ole Ngurumwa said. “We must build a culture where we confront our challenges openly and honestly as a nation. Let’s come together and forge a national consensus—for the sake of our people, our democracy, and the peaceful future we all deserve, especially with elections around the corner.”

*Watetezi Analysts*
*16/07/2025*

Mahak**a Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo ya Dar es Salaam, imepanga kutoa uamuzi tarehe Agosti 12, 2025 kuhusu maombi ya ...
16/07/2025

Mahak**a Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo ya Dar es Salaam, imepanga kutoa uamuzi tarehe Agosti 12, 2025 kuhusu maombi ya mapitio yaliyowasilishwa na Mwenyekiti wa Chadema, Tundu Lissu.

Uamuzi huo umetangazwa leo Jumatano, Julai 16, 2025 na Jaji Elizabeth Mkwizu, baada ya kusikiliza hoja za mawakili wa Lissu na majibu kutoka upande wa Serikali.

Katika maombi hayo, Lissu anapinga uamuzi wa Mahak**a ya Kisutu ulioruhusu baadhi ya mashahidi wa Jamhuri katika kesi yake ya uchapishaji wa taarifa za uongo mtandaoni kulindwa majina na utambulisho wao. Lissu anadai kuwa uamuzi huo unakandamiza haki yake ya kujitetea kikamilifu.

Pia, Jaji Mkwizu ametangaza kuwa siku hiyo hiyo ya Agosti 12 atatoa uamuzi juu ya malalamiko ya Lissu dhidi ya Magereza, ambapo analalamikia kudhibitiwa kwa kunyimwa mawasiliano huru na mawakili wake, pamoja na kuzuiwa kupewa nyaraka muhimu kutoka kwa mawakili hao.

Mahak**a Kuu Kanda ya Dar es Salaam leo Julai 16,2025  inatarajiwa kusikiliza maombi ya Mwenyekiti wa Chama cha Demokras...
16/07/2025

Mahak**a Kuu Kanda ya Dar es Salaam leo Julai 16,2025 inatarajiwa kusikiliza maombi ya Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Taifa, Tundu Antiphas Lissu, ya kutaka kufanyika kwa marejeo dhidi ya uamuzi wa Mahak**a ya Hakimu Mkazi Kisutu, kuhusu ombi la Jamhuri la kutaka mashahidi wa kesi ya uchochezi kufichwa.

Katika maombi hayo, Lissu kupitia kwa mawakili wake, anapinga uamuzi wa Mahak**a ya Kisutu kuruhusu Jamhuri kuficha majina na sura za mashahidi wake, akidai kuwa hatua hiyo inakiuka haki zake za msingi k**a mshtakiwa, ikiwemo haki ya kujua ushahidi unaomkabili na haki ya kupata utetezi wa haki.

Kesi ya uchochezi inayomkabili Lissu inaendelea katika Mahak**a ya Hakimu Mkazi Kisutu, ambapo Jamhuri ilieleza kuwa ipo haja ya kuwaficha mashahidi wake kwa sababu za kiusalama. Hata hivyo, upande wa utetezi umepinga vikali hoja hizo, na hivyo kupeleka hoja ya marejeo Mahak**a Kuu.

Mahak**a Kuu inatarajiwa kusikiliza hoja hizo leo na kutoa mwelekeo wa iwapo uamuzi wa Mahak**a ya Kisutu utapaswa kupitiwa upya au kuendelea k**a ulivyotolewa.

Uamuzi wa Mahak**a Kuu katika maombi haya unaweza kuwa na athari kubwa, si tu kwa kesi hii ya Mheshimiwa Lissu, bali pia kwa mwenendo wa kesi nyingine za jinai zinazohusisha masuala ya haki za kiraia na kisiasa nchini.

Address


Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Watetezitv posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to Watetezitv:

Shortcuts

  • Address
  • Telephone
  • Alerts
  • Contact The Business
  • Claim ownership or report listing
  • Want your business to be the top-listed Media Company?

Share