Chakushangaza

  • Home
  • Chakushangaza

Chakushangaza Njoo tukujuze TUJUZANE

MJ Records 2010 - MJ, Millard Ayo na Marco Chali.Enzi hizo 15 years back📸 Master J
13/04/2025

MJ Records 2010 - MJ, Millard Ayo na Marco Chali.
Enzi hizo 15 years back

📸 Master J

MAGIC , WITCHCRAFT, SORCERYKatika vitu hivyo vitatu katika kiswahili hakuna maneno ya kutosha kuweza kutofautisha maana ...
11/04/2025

MAGIC , WITCHCRAFT, SORCERY

Katika vitu hivyo vitatu katika kiswahili hakuna maneno ya kutosha kuweza kutofautisha maana lakini , maneno yote matatu katika kiswahili yanamaanisha UCHAWI.

🤙Lakini MAGIC WITCHCRAFT na SORCERY ni tofauti

Sasa kwa uelewa wa haraka haraka
Magic ni uchawi lakini ni tofauti na Witchcreft na Sorcery

Magician akitaka kumuita kiumbe ni tofauti na SORCERY au WITCHES wakitaka kuwaita viumbe.

MAGICIAN anatumia sana nguvu zake mwenyewe (analazimika sana kutunza nguvu zake za ngono au sexual energy ili kuifadhi na kuongeza nguvu zake), magician anategemea sana nguvu asilia yenyewe moja kwa moja ni mtu asiye pendelea connection au kuunganishiwa na viumbe au mapepo. Magician anaongea moja kwa moja na Ulimwengu na kupitia kanuni za magic , magician anaweza kuongea na viumbe wa juu zaidi kutoka nje ya sayari ya Dunia. Lakini WASHIRIKINA (WITCHCRAFT na SORCERERS) wanaishia kuongea na majini na mapepo pamoja na mizimu.

Magician anategemea sana power of mind nguvu ya akili na fikra, Kwahiyo maditation ni muhimu mno kwa magician ni amri kuu. Lakini msgirikina anategemea sana vizimba, majini, mizimu na mapepo pamoja na madawa k**a chanzo cha nguvu zake na hawaitaji meditation labda k**a wameiga kutoka kwa magician.

Washirikina wanaweza pia kuwa magician. Lakini Magician ni ngumu mno kuchanganya na ush*tikina

🤙Magicians wanategemea sana PASSWORD (Nemo siri), PATTER (Miundo siri), RUNES, SIGIL (Mihuri ya siri inayotamka jambo), CODES (Namba siri), na Lugha ya Kuchonga (Hieroglyphs).

🤙Washirikina wanategemea sana damu na sadaka ndogo ndogo ili wapate kukubalika kwa viumbe wanao watumikia.

WASHIRIKINA lazima wawe chini ya viumbe hatimaye wanatumikishwa na viumbe wengine hasa Mizimu, majini, Mapepo. Lakini Magician hatumikishwi na kiumbe kwahiyo hana masharti.

🤙Magicians hana makorokoro mengi hana vibuyu haitaji dawa nyeusi wala haitaji shanga au makorokoro kibao mnayo yaona kwa WASHIRIKINA..Lakini washirikina wanahotaji vikorokoro k**a vyote na

Mpwampwa Sec. School,1969.
25/11/2024

Mpwampwa Sec. School,1969.

  MR METHANE ⠀👉Huyu👆 ni mtalamu  wa kujamba nchini UINGEREZA anaweza kujamba sauti mbalimbali akifatisha midundo ya muzi...
25/11/2024


MR METHANE ⠀
👉Huyu👆 ni mtalamu wa kujamba nchini UINGEREZA anaweza kujamba sauti mbalimbali akifatisha midundo ya muziki ⠀
👉Amekua akitumika na makampuni mengi ya biashara kupitia kipaji chake hicho ⠀
👉Pia amekua akifanya matamasha na anajiita THE ONLY PROFESSIONAL FARTER IN THE WORLD

  Pichani ni Kaylee Moats Mwanamke wa Miaka 29 Sasa Raia wa Arizona US. Mwaka 2017 Alikuwa Anahangaika Kuomba Pesa Zimsa...
05/08/2024


Pichani ni Kaylee Moats Mwanamke wa Miaka 29 Sasa Raia wa Arizona US. Mwaka 2017 Alikuwa Anahangaika Kuomba Pesa Zimsaidie Katika Upasuaji wa Kutobolewa Uke, Alizaliwa Bila Via vya Uzazi, Alikuwa Anaweza Kutoa Haja Ndogo Pekee, Njia ya Uzazi Hakuna.

★☆☆☆☆☆☆★★☆☆☆☆☆☆★★★☆☆☆

Mwaka 2017 taarifa kutoka Arizona zilisema kuwa mwanamke Kaylee Moats (22) raia wa mji huo alikuwa anaomba mdaada wa michango ili afanyiwe upasuaji wa uke, alizaliwa bila uke wala mfuko wa uzazi, hali hii inaitwa (MRKH) Mayer-Rokitansky-Küster-Hauser.

Tatizo hili linawakumba sana wanawake, uke anakuwa nao lakini anakua anaweza kukojoa tuu, ile njia maalumu kwa tendo la ndoa inakua haipo.

Mpenzi wake Robbie Limmer alisema kuwa hajali kabisa kuhusu kufanya mapenzi na mpenzi wake huyo, anachojali ni kumsaidia kupatikana kwa kiasi cha pesa US 15,000 ili upasuaji ufanyike apate njia, japo njia hii ya kutengenezwa huwapa maumivu sana wanawake wakati wa tendo.

"Nilikutana na Robbie katika mwaka wangu wa mwisho wa chuo kikuu. Alisema nilikuwa mzuri kwa hivyo alinijia na tukaanza kuongea"

"Ilichukua mwezi mmoja kumwambia kuwa nina MRKH. Alichanganyikiwa mwanzoni lakini aliunga mkono na akasema kwamba hawezi badilisha vile ananipenda. Kwa kweli tuwezi kufanya chochote kwa kuwa sina ufunguzi wa uke."

Kaylee anasema uke wake unaonekana jinsi inavyopaswa isipokuwa hauna ufunguzi, hakuna shimo linalopaswa kuwepo.

February 26, 2020 mtandao wa BBC uliripoti kuwa mwanamke Julian Peters wa miaka 29 raia wa Kenya analo tatizo k**a hili pia. Uke unakwepo kwa haja ndogo pekee, hakuna njia ya uzazi.

  Henry Ford (1863 - 1947) pichani, alikuwa mfanyabiashara Mmarekani, mwaasisi na mmiliki wa kiwanda cha magari aina ya ...
03/08/2024


Henry Ford (1863 - 1947) pichani, alikuwa mfanyabiashara Mmarekani, mwaasisi na mmiliki wa kiwanda cha magari aina ya FORD.

Watu wanasema kuwa hakuwa na elimu kubwa, aliishia darasa la nne tu, bali alikuwa na uwezo mkubwa wa kuendesha biashara na uwekezaji...

Jopo la wasomi walimkalia kitako, kumwaambia kuwa yeye ni mjinga tu na wakambamiza swali gumu la kisayansi kuthibitisha ujinga wake, Mzee Ford akachukuwa simu yake na kumpigia mmoja wa wataalamu wake na wasomi hao wakapewa jibu sahihi...

Wasomi wakapayuka na kusema: "Tuliwaambia kuwa yeye ni mjinga, ona sasa, hawezi hata kujibu maswali tunayomuuliza." Mzee Ford akajibu: "K**a nina wataalamu wa kujibu maswali yenu, kwa nini nipoteze muda kubishana nanyi badala ya kufanyia kazi mawazo yangu ya biashara na kutafakari kwa kina."

Mzee Ford akaendelea na kazi zake muhimu na kuwaacha wasomi kwenye butwaa lao la majungu.

Tunaweza kujifunza nini kupitia hili lililowahi kumkuta gwiji huyu wa biashara na viwanda huko Mmarekani?

  John D. Rockfeller alizaliwa Julai 8, 1839 na kufariki Mei 23, 1937, mwanzilishi wa Standard Oil alikuwa mtu tajiri za...
03/08/2024


John D. Rockfeller alizaliwa Julai 8, 1839 na kufariki Mei 23, 1937, mwanzilishi wa Standard Oil alikuwa mtu tajiri zaidi duniani. Alikuwa bilionea wa kwanza duniani. Alipata utajiri wa dola bilioni 1 mnamo 1916. Wakati Rockefeller alipokufa mnamo 1937, utajiri wake ulikadiriwa kuwa karibu $340 bilioni katika dola za leo. Kufikia umri wa miaka 25, alidhibiti moja ya kiwanda kikubwa zaidi cha kusafisha mafuta huko marekani. Alikuwa na umri wa miaka 31 alipokuwa msafishaji mkubwa zaidi wa mafuta ulimwenguni. Akiwa na miaka 38, aliagiza 90% ya mafuta yaliyosafishwa nchini U.S.

John, katika umri wa miaka hamsini alikuwa mtu tajiri zaidi katika nchi ya Amerika. Akiwa kijana, kila uamuzi, mtazamo, na uhusiano uliundwa ili kuunda nguvu na utajiri wake binafsi.

Lakini akiwa na umri wa miaka 53, aliugua. Mwili wake wote ulipatwa na maumivu na kupoteza nywele zake zote. Kwa uchungu kabisa, bilionea pekee duniani angeweza kununua chochote alichotaka, lakini aliishia tu kuchimba visima na crackers. Mshiriki mwenzie wa karibu aliandika maneno haya , "Hakuweza kulala, hakutabasamu na hakuna kitu maishani cha maana kwake alichofurahia". Madaktari wake kibinafsi, waliobobea sana walitabiri kwamba angekufa ndani ya mwaka mmoja. Mwaka huo ulipita polepole kwa uchungu.

Alipokuwa akikaribia kufa aliamka asubuhi moja na bila kujitambua na kupelekea mpaka kudahau kuzitambua mali zake alikuwa Mtu ambaye angeweza kudhibiti ulimwengu wa biashara ghafla aligundua kuwa hakuwa na udhibiti wa maisha yake mwenyewe. Aliachwa na chaguo moja tu la kifo.

Aliwaita mawakili wake, wahasibu, na wasimamizi na akatangaza kwamba alitaka kuelekeza mali zake kwenye Hospitali zinazofanya maswala ya Utafiti, na Kazi ya Usaidizi. John D. Rockefeller alianzisha Wakfu wake na utajiri wake ukaenda kwenye mahospitali kuanzisha miradi ya utafiti wa matatizo mbalimbali.

Rockefeller Foundation iliunga mkono juhudi za Howard Florey na mwenzake Norman Heatley katika utafiti wao juu ya penicillin mnamo 1941.

Lakini labda sehemu ya kushangaza zaidi ya hadithi ya Rockefeller ni kwamba wakati alipoanza kurudisha sehemu ya yote aliyokuwa amepata, kemia ya mwili wake ilibadilishwa kwa kiasi kikubwa kwamba alipata ubora. Ilionekana kana kwamba angekufa akiwa na miaka 53 lakini aliishi hadi miaka 98.

Rockefeller alijifunza shukrani na akarudisha sehemu kubwa ya utajiri wake. Kufanya hivyo kulimfanya awe mzima. .

Alikuwa Mbaptisti aliyejitolea na alihudhuria Kanisa la Baptist la Euclid Avenue huko Cleveland, Ohio. Kabla ya kifo chake, aliandika hivi katika shajara yake:

“Mungu alinifundisha, kwamba kila kitu ni chake, na mimi ni njia tu ya kutekeleza matakwa Yake. Maisha yangu yamekuwa likizo moja ndefu, yenye furaha baada ya hapo; Nikiwa nimejawa na kazi na mchezo mwingi, niliondoa wasiwasi nikiwa njiani, na Mungu alikuwa mwema kwangu kila siku.”

Unapokuwa mzima jifunze kuwa na shukrani kwa mungu

Hivi karibuni, Instagram itafanya mabadiliko katika sehemu ya Ujumbe wa Moja kwa Moja (DM) na Reels. Instagram itaweka u...
28/04/2024

Hivi karibuni, Instagram itafanya mabadiliko katika sehemu ya Ujumbe wa Moja kwa Moja (DM) na Reels. Instagram itaweka uwezo wa kutuma Reels nyingi kwa pamoja, na zote zitajipanga vizuri na itakuwa rahisi kuona kundi la Reels ambazo zimetumwa kwa pamoja.

Instagram inaendelea kuboresha uzoefu wa kutuma na kushiriki Reels baada ya kugundua kwamba watumiaji wengi wanapenda kutuma Reels kwenye DMs.

Cc: swahili tek

_________

IPE NENI HIIFULL STORY NIMEKUWEKEA TELEGRAM GUSA LINK HAPO KWENYE BIO AU NENDA TELEGRAM KISHA SEARCH CHAKUSHANGAZA KWA W...
28/04/2024

IPE NENI HII
FULL STORY NIMEKUWEKEA TELEGRAM GUSA LINK HAPO KWENYE BIO AU NENDA TELEGRAM KISHA SEARCH CHAKUSHANGAZA KWA WALE WA FB LINK HII t.me/chakushangaza
#0627368679

WhatsApp itaweka sehemu mpya ya "Favourites" - itasaidia kuweka list ya namba zako za karibu na WhatsApp Groups ambazo u...
27/04/2024

WhatsApp itaweka sehemu mpya ya "Favourites" - itasaidia kuweka list ya namba zako za karibu na WhatsApp Groups ambazo unapendelea kuzifuatilia sana.

Sehemu hii itasaidia kuona contacts ambazo unawasiliana nazo mara kwa mara au contacts ambazo unapendelea kuzipata kwa urahisi.

Sehemu hii imeanza kwenye WhatsApp ya Android na itapatikana kwa watumiaji wote.

______________


Cc: swahili tek

  UNAIJUA STORY YA  GEORGE STINNEYSOMA HIIIKAMWE MSIMSAHAU NDUGU YETU,WAFUNDISHENI WATOTO WENU HISTORIA YAKE. 😓George St...
26/04/2024


UNAIJUA STORY YA GEORGE STINNEY

SOMA HIII

KAMWE MSIMSAHAU NDUGU YETU,WAFUNDISHENI WATOTO WENU HISTORIA YAKE.

😓George Stinney Jr alikuwa mtu mdogo zaidi kuhukumiwa kifo katika karne ya 20 nchini Marekani.

Alikuwa na umri wa miaka 14 tu aliponyongwa kwenye kiti cha umeme.

Wakati wa kesi yake, hata siku ya kunyongwa kwake, daima alibeba biblia mikononi mwake, akidai kuwa hana hatia.
Alishtakiwa kwa kuwaua wasichana wawili wa kizungu, Betty mwenye umri wa miaka 11, na Mary wa miaka 7, miili yao ilikutwa karibu na nyumba ambayo kijana huyo aliishi na wazazi wake.

Wakati huo, washiriki wote wa mahak**a walikuwa wazungu.

Kesi hiyo ilidumu kwa saa 2 tu, na hukumu ilitolewa dakika 10 baadaye.

Wazazi wa Mvulana huyo walitishiwa, na kuzuiwa kuwapo katika chumba cha mahak**a, na baadaye kufukuzwa kutoka katika mji huo.

Kabla ya kunyongwa, George alikaa gerezani kwa siku 81 bila kuwaona wazazi wake.

Aliwekwa Katika chumba cha peke yake, maili 80 kutoka mji wake alipokuwa anaishi.

Walimpeleka mahak**ani peke yake bila uwepo wa wazazi wake au wakili.

Walimuuwa na shot ya umeme wa volti 5,380 kichwani mwake, fikiria voltage yote hiyo katika kichwa cha mtoto.😭😭😭😭😭😭😭

Miaka 70 baadaye, KESI yake ilikatwa rufaa na kusikilizwa tena hatimaye mahak**a ilithibitishwa na hakimu huko FULL STORY NIMEKUWEKEA TELEGRAM GUSA LINK HAPO KWENYE BIO AU NENDA TELEGRAM KISHA SEARCH CHAKUSHANGAZA KWA WALE WA FB LINK HII t.me/chakushangaza
#0627368679

Address


Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Chakushangaza posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to Chakushangaza:

Shortcuts

  • Address
  • Telephone
  • Alerts
  • Contact The Business
  • Claim ownership or report listing
  • Want your business to be the top-listed Media Company?

Share