13/11/2024
Mimi na mke wangu hatukua na maelewano usiku wa jana, na hata asubuhi ya leo kabla ya kuondoka kwenda kazini, Kila mmoja bado alikua kamkasirikia mwenzie.
Mimi na yeye wote tunafanya kazi mjini, na ni kawaida yetu kila siku kutoka pamoja kwenda kazini, tumekua ni watu wa kutaniana wakati wa kujiandaa na tunapotoka ndani anaechelewa kutoka ndo hua anatakiwa kufunga mlango, kuna wakati hua namfichia mafuta yake ya kupaka ili tu achelewe kumaliza kujiandaa na afunge mlango, utani na kuchezeana hapa na pale mda huo hua ni jadi yetu.
ila leo mambo yalikua tofauti kidogo kutokana na kutokua na maelewano.
Leo baada ya kujiandaa nilitoka nje tofauti na ilivyozoeleka na yeye akanifata nyuma, akafunga mlango tukaanza kutembea kwenda stand kupanda gari, kawaida yetu hua tunakaa seat ya pamoja ila leo kila mtu alikaa seat yake, ye alikaa mbele mie nikawa nyuma.
Pembeni ya mke wangu alikua amekaa Askari mmoja..
Asikari yule akamwangalia mke wangu Niliona jinsi alivyoangalia nywele na uso wake kwa kupendeza sana. Kisha akamwambia amependeza. Mke wangu alitabasamu na kumwambia asante.
Alimuuliza mke wangu anaenda wapi akamwambia anaenda job
Wakati wote huu, nilikuwa nimeiketi nyuma na kusikiliza mazungumzo yao.
"Naitwa Hemed" Mimi ni askari k**a unavyoniona kwenye sare zangu, nimetoka depo mwezi uliopita na sasa naelekea kwenye kituo changu cha kazi nilichopangiwa, Mke wangu alitikisa kichwa.
Kondakta alipoomba nauli kwa mke wangu, afande alijitolea kulipa, akatoa noti ya 2000 alafu akasema wawili inamaana yeye pamoja na mke wangu.
Mke wangu akamshukuru na akatabasamu
Basi afande akaendelea
"Mie nitashuka hapo mbele kituo kinachofata, hivyo naomba ukipata nafasi unawezapita hapo unisalimie nitakuepo katika kituo kidogo cha police hicho hapo mbele, lakini pia naomba nipate namba yako kwa mawasiliano zaidi”
Mie kwakua nilikua nyuma ya mke wangu niliyasikia maongezi yao yote, baada ya kusikia mke wangu kuombwa namba na afande Sikupoteza muda wowote tena. Nilimpiga mke wangu mabega yake mara moja.
Kageuka
Kisha nikamwambia
"I hope ulikumbuka kuweka kijiko ndani ya lunch box ya Gift? Unajua huwa unasahau.”
Mke wangu alichanganyikiwa Pengine alikuwa anajiuliza Gift ni nani, na kwanini nimeamua kuzungumza naye. Kabla hajaniuliza maswali yoyote zaidi niliongeza.
"Jaribu kumchukua kutoka shuleni mapema leo. Mie Nitachelewa kurudi nyumbani. Pia itapendeza leo upike chapati na nyama rost kwa ajili ya chakula cha usuku "
Mke wangu alizidi kuchanganyikiwa
Kisha akamtazama askari na kunirudishia macho yake. Alielewa kile nilikuwa najaribu kufanya.
"Sawa honey" Alitabasamu.
Askari aligeuka na kunitazama kisha akanisalimia sana Kisha akamuuliza mke wangu.
"Huyu ni mume wako?"
Mke wangu alitabasamu. Askari kaniangalia tena na tena
Kisha akatazama kwa mara ya mwisho na akatabasamu kwangu.
Mie Sikutabasamu hata kidogo
Tulipofika kwenye kituo tunachoshukia ili tupate kupanda basi lingine nilishuka kutoka kwenye basi na kumvuta mke wangu kwa nguvu.
Mke wangu alishindwa kujizuia kuacha kucheka. Tukiwa tunatembea huku nimemshika mkono nikamsikia akiuliza.
"Honey Gift ni nani? "
"Gift ni binti yetu wa baadae. Nilimjibu huku nimemkazia macho"
Mke wangu akacheka sana.
Tulipanda basi lingine na safari hii sikutaka tena kukaa mbali na mke wangu, na konda alipoomba nauli nilitoa chapu na kusema “wawili” tulitazamana na mke wangu tukajikuta tunacheka wote kwa pamoja, na jioni ilipofika tulilejea nyumbani na nambo yalikua bam bam na ugomvi wetu ukawa umeishia hapo.
NB: Unapompa mpenzi wako umbali, kiroho na kimwili, unampa shetani akae kwenye nafasi hiyo.
Anachukua nafasi yako bila ruhusa yako na anajijengea makao kwako.
Usiruhusu shetani awe na nafasi nyumbani kwako. funga njia zote za shetani kuweza kupitia.
Fanya uwepo wako ujulikane
Mungu aibariki ndoa yako na mahusiano yako Sing'ongo Tz