29/04/2024
Je wajua?
PG, SPG, R na X ni alama zinazoonyeshwa kwenye filamu na tamthiliya katika runinga (TV) humaanisha usimamizi kwa watoto na watu wazima pia?
Kwa kawaida filamu na tamthiliya huwa na maudhui na muonekano tofauti tofauti, ukiachana na maonyesho ya kawaida yanayofaa kutazamwa na mtu yeyote ila wakati mwingne kuna maonyesho huchagua umri na jamii kutokana na maudhui yaliyopo, kwa mfano maonyesho mengine huwa na maudhui ya ngono, maudhui ya kimapenzi, maudhui ya watoto tu, maudhui ya wakubwa tu, maudhui ya matusi, matumizi ya madawa ya kulevya na ulevi, au maudhui ya dharau, jeuri au madhui yasiyo na heshima au maudhui ya kutisha ambayo kuna baadhi ya jamii ya watu yanaweza kuwaathiri hivyo hawafai kuitazama.
Baadhi ya alama hizo ni k**a zifuatazo na maana zake;
G. Humaanisha GENERAL GUIDANCE maonyesho haya yanaruhusiwa kutazamwa na watu wote.
PG. Humaanisha PARENTAL GUIDANCE hii humaanisha onyesho hilo linahitaji watoto wasiangalie bila ya uongozi wa wazazi, alama hii huonekana ikiwa na namba k**a vile PG-13 humaanisha watoto wenye umri chini ya miaka 13 wasitazame bila ya uongozi wa wazazi, nyingne ni PG-16 humaanisha watoto wenye umri chini ya miaka 16 wasitazame bila ya uongozi wa wazazi, nyingne PG-18 humaanisha watoto wenye umri chini ya miaka 18 wasitazame bila ya uongozi wa wazazi n.k.
SPG. humaanisha STRONG PARENTAL GUIDANCE hii pia humaanisha onyesho hilo linahitaji uangalizi mkubwa sana kutoka kwa wazazi hivyo wazazi wahakikishe wanakuwa makini sana na watoto wao kwenye onyesho hilo.
R. Humaanisha RESTRICTED humaanisha onyesho hilo lisitazamwe kabisa kwa watu maalum, na hii pia huwa inaonekana ikiwa na namba k**a vile R-13 humaanisha watoto wenye umri chini ya miaka 13 wasitazame kabisa, nyingne R-16 humaanisha watoto wenye umri chini ya miaka 16 wasitazame kabisa, nyingne R-18 humaanisha watoto wenye umri chini ya miaka 18 wasitazame kabisa n.k.
X. Humaanisha NOT FOR PUBLIC EXHIBITION humaanisha onyesho hilo lisitazamwe mbele ya jamii ya watu wengi badala yake litazamwe na watu wachache au mmoja na wawe faragha, hii mara nyingi hutumika kwenye maonyesho ya ngono n.k.
Ahsanteni