22/07/2025
NABII YA'QUUB KUTAKA KUOA
Wakati Nabii Ya‘qub alipofikia umri wa kuoa, wazazi wake walimshauri asafiri kwenda ardhi ya Harran iliyoko Iraq, na kumposa mmoja wa mabinti wa mjomba wake Laban. Nabii Yakobo alitii ushauri wa wazazi wake, akaelekea kwa mjomba wake huko Iraq, ambako alimkuta na mabinti wawili:
Lia (aliyekuwa binti mkubwa), na
Raheli (binti mdogo), aliyekuwa mrembo zaidi, msafi, na mwerevu kuliko dada yake.
Yaaqub alimuomba Raheli amuoe kwani alimpenda sana. Lakini baba yake Raheli alimwambia kuwa lazima amfanyie kazi kwa kipindi cha miaka saba k**a mahari ya binti yake. Nabii Yaaquub alikubali, na akafanya kazi kwa bidii kwa miaka saba mfululizo.
Lakini ilipofika siku ya harusi, mjomba wake alimwozesha Yaaqub binti mkubwa (Lia) badala ya Raheli.
Asubuhi ya siku iliyofuata, Yaaqub alikwenda kwa hasira kwa mjomba wake na kumkumbusha kuwa alikuwa amemuomba Raheli, si Lia. Mjomba wake akamweleza kuwa desturi ya nchi hiyo hairuhusu binti mdogo kuolewa kabla ya mkubwa.
Nabii Yaaquub hakuwa na budi ila kukubali pendekezo la kufanya kazi tena kwa miaka saba mingine ili apewe Raheli. Na alikubali.
Kumbuka: Katika wakati huo haikuwa haramu kuoa dada wawili kwa wakati mmoja, k**a ilivyokuja kuwa haramu baada ya kuja kwa Uislamu. Baadhi ya wafasiri wa Qur’an wanasema kwamba huenda Yaaqub alimuoa Raheli baada ya kifo cha Lia.
Katika kipindi hicho cha miaka saba, Lia alimzalia Yaaqub watoto kadhaa, lakini Yaaquub aliendelea kumtamani Raheli aliyekuwa akimpenda kwa dhati, mpaka alipomwoa pia.
Mjomba wake, Laban, aliwapa kila binti wake kijakazi:
Lia alipewa kijakazi aitwaye Zilfa,
Raheli alipewa kijakazi aitwaye Bilha.
Baada ya Raheli kuona kuwa dada yake Lia alikuwa ameshamzalia Yaaquub watoto wanne naye hakuwa na mtoto, alimpa Yaaqub kijakazi wake Bilha, ambaye alimzalia watoto.
Lia naye, kwa kuona hilo, alifanya k**a Raheli, akampa Yaaqub kijakazi wake Zilfa, naye akazaa.
Raheli, licha ya kuwa mpendwa zaidi kwa Nabii Ya‘qub, alihisi huzuni kwa kukosa mtoto kwa muda mrefu. Akaamua kujielekeza kwa mwenyezi Mungu kwa unyenyekevu, maombi na machozi, akimwomba amruzuku mtoto mwema.
Allah, Mwingi wa Rehema, akamjibu dua yake. Baada ya muda, Raheli akapata ujauzito, na akamzaa mtoto wa kiume aliyeitwa:
Yusuf (a.s) mtoto mcha Mungu, mrembo kwa sura na tabia, na baadaye akawa miongoni mwa Manabii wakubwa wa Bani Israil.
Huu ulikuwa ni ujira mkubwa kwa subira na maombi ya Raheli.
Baada ya Yusuf:
Baadaye Raheli alipata mtoto mwingine aitwaye Binyamin Lakini wakati wa kujifungua kwake Bin'yamin Raheli alipata matatizo na akafariki dunia.
Hili lilimvunja moyo sana Nabii Ya‘qub, kwani alimpenda sana Raheli kuliko wake wengine.
Mtoto wa Upendo:
Yusuf na Bin'yamiin walikua wakiwa ni watoto waliopendwa sana na baba yao Yaaqub, hasa Yusuf kutokana na tabia yake njema, heshima, na maono aliyopewa na Allah tangu akiwa mdogo.
Lakini upendo huu ulisababisha wivu mkubwa kwa kaka zake Yusuf waliotokana na wake wengine, hasa kutoka kwa watoto wa Lia na watoto wa mjakazi wake.
Wivu huo ndio ulipelekea kisa mashuhuri cha Yusuf kutupwa kisimani, ambacho kimeelezewa kwa kina katika Surat Yusuf (Surah ya 12) ya Qur’an Tukufu.
Hitimisho: Hekima kubwa katika hadithi hii ni kwamba:
Subira na dua huzaa matunda.
Upendo wa kweli hujaribiwa na wakati.
Na kwamba mipango ya Mwenyezi Mungu daima ni bora hata k**a mwanzo wake unaonekana kuwa mgumu
Sufian Mzimbiri .