Taarifa ZOTE

Taarifa ZOTE Hapa utapata habari za kila saa.Ila huruhusiwi kutupatia habari za Matusi.

Pia unaruhusiwa kutangaza biashara yako.Anayekiuka masharti ataondolewa kwenye kundi Karibuni sana ila vigezo na Masharti kuzingatiwa.

01/08/2025

Chama Cha Mapinduzi(CCM) kimemteua Mtoto wa Rais wa awamu ya tano Hayati John Pombe Magufuli Magufuli, Jessica Magufuli ( .jmagufuli ) na Wagombea wengine 30 kugombea Ubunge Viti Maalum kupitia kundi la UVCCM

Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Amos Makalla ametangaza majina hayo leo July 29,2025.

01/08/2025
01/08/2025

: Tume ya Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) imesema hakuna sheria inayoruhusu kura za mapema kupigwa kwa upande wa Tanzania bara katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 29 mwaka huu.

Kura hiyo ni ile ambayo itapigwa Zanzibar na baadhi ya watu, ambazo siku ya uchaguzi watakuwa na majukumu ya kusimamia uchaguzi mkuu huo.

Kauli hiyo meelezwa na Mwenyekiti wa INEC Jaji Mstaafu wa Mahak**a ya Rufaa Jackobs Mwambegele, wakati akizungumza na Wahariri wa vyombo vya Habari Jijini Dar es Salaam.

Amesema Zanzibar ilipitisha sheria ya kuruhusu upigwaji huo wa kura.

Mbali ya Hilo Jaji Mwambegele amesema raia wa Tanzania wanaoishi nje ya nchi hawataweza kupigakura kutokana na sheria kutaka zoezi kufanyika hapahapa nchini.

Tume huru ya taifa ya uchaguzi (INEC) inaendelea kukutana na makundi mbalimbali kuelezea maandalizi ya uchaguzi mkuu yalipofikia.


01/08/2025

Jeshi la Polisi Mkoani Mtwara limesema limemk**ata Anastanzia Exavery Mahatane (27), maarufu Ebitoke katika fukwe za Msanga Mkuu Mjini Mtwara akiwa katika hali inayoonekana kuwa amechanganyikiwa na wala hakuwa ametumbukizwa katika shimo wala kutekwa k**a ambavyo alivyokuwa ameeleza mitandaoni ambapo Polisi hao wamempeleka Ebitoke Hospitali ya Mkoa Mtwara kwa matibabu na limeomba Ndugu zake wafike Mtwara kumchukua.

Akiongea leo August 01,2025, Kamanda wa Polisi Mtwara Issa Suleiman amesema ““Mnamo July 30, 2025 Anastanzia Exavery Mahatane (27), maarufu Ebitoke ambaye ni Msanii wa comedy hapa Tanzania, Mkazi wa Dar es salaam, ambaye kwa sasa anaishi katika Kata na Kijiji cha Msanga Mkuu Wilaya ya Mtwara alichapisha taarifa katika akaunti zake za mitandao ya kijamii ikiwemo Instagram kuwa yeye kwa sasa yupo Mtwara na kwamba ametumbukizwa katika shimo huko katika fukwe za Msanga Mkuu na kwamba wapo Watu ambao aliwataja kwa majina kuwa wanataka kumuua”

“Kwakuwa Jeshi la Polisi jukumu lake la msingi ni kulinda raia na mali zao, Jeshi la Polisi Mkoa wa Mtwara lilianza uchunguzi wa haraka sana ilikujua ukweli wa taarifa iliyotolewa na Anastanzia Mahatane, katika uchunguzi wa awali Jeshi la Polisi Mkoa wa Mtwara limebaini kwamba Ebitoke alifika Mtwara tangu
Aprili 2025 na kufikia katika hoteli moja iliyopo Msanga Mkuu na kuomba hifadhi kwa Watu waliokuwa wanafahamiana kabla ya maisha yake kumuendea vibaya huko alikokuwa”

“July 31, 2025 saa 11:00 jioni Jeshi la Polisi Mtwara lilimk**ata Ebitoke huko katika fukwe za Msanga Mkuu akiwa katika hali inayoonekana kuwa amechanganyikiwa na wala hakuwa ametumbukizwa katika shimo wala kutekwa k**a ambavyo alivyokuwa ameeleza katika mitandao hiyo ya kijamii, Ebitoke amefikishwa katika Hospitali ya Mkoa wa Mtwara kwa ajili ya matibabu na Jeshi la Polisi Mtwara linawaomba ndugu na jamaa wa Ebitoke kufika Mkoa wa Mtwara kutoa msaada au kumchukua ndugu yao”

28/06/2025
28/06/2025

Address

Usa River

Telephone

+255752243648

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Taarifa ZOTE posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share