Vwawa Fm Radio

Vwawa Fm Radio Tuna wakaribisha kwenye ukurasa rasmi wa vwawa fm radio
karibu kwa maoni na ushauri . tuambie unatusikia kutoka wapi
103.7

📰 MBEYA | MWENGE WA UHURU 2026 🇹🇿🔥Mwenge wa Uhuru unatarajiwa kuwasili mkoani Mbeya Septemba 28, 2026, na kukimbizwa kwa...
05/09/2026

📰 MBEYA | MWENGE WA UHURU 2026 🇹🇿🔥

Mwenge wa Uhuru unatarajiwa kuwasili mkoani Mbeya Septemba 28, 2026, na kukimbizwa kwa siku saba katika halmashauri mbalimbali za mkoa huo.

Kaulimbiu ya mwaka huu ni: “Tanzania ni yetu sote, tushik**ane kwa pamoja kuleta maendeleo.”

📍 Ratiba kwa ufupi:

Septemba 28: Chunya – Mapokezi Lupatingatinga

Septemba 29: Jiji la Mbeya

Septemba 30: Mbarali

Oktoba 1: Rungwe

Oktoba 2: Kyela

Oktoba 3: Busokelo

Oktoba 4: Mbeya DC

Oktoba 5: Mwenge utakabidhiwa Mkoa wa Songwe kupitia Mbozi.

🔥 Mwenge wa Uhuru 2026 — Tanzania ni yetu sote. Tushik**ane kwa pamoja kuleta maendeleo! 🇹🇿

02/09/2026

Wachekeshaji na wamejiandaa vilivyo kutumbuiza tarehe 12 September 2026 katika ukumbi wa uliopo Mlowo Stand Mpya

JE USHAPATA TIKETI YAKO?

CALL 0777 302 982 AU 0757444065

02/09/2026

Dkt Samia: Wakuu wa mikoa mkawatumikie wananchi

Rais Dkt Samia Suluhu Hassan, amewaambia wateuliwe wapya wa ukuu wa mkoa na katibu tawala kwamba hawajapeleka maeneo hayo, kuwa wafalme bali kuwa watumishi wa wananchi.

Dkt Samia ameeleza hayo Jumatano Septemba 2,2026 wakati wa akiwaapisha wakuu wa mikoa na katibu tawala aliowateua hivi karibuni. Uapisho huo umefanyika Ikulu Ndogo ya Tunguu, Kusini Unguja.

Amefafanua kuwa kwa mujibu wa Katiba, Rais amekasimu madaraka yake katika eneo lililokatwa la mkoa na kukabidiwa wakuu wa mikoa.

“Wewe jichukulie k**a rais wa eneo hilo, mkoa hauna fedha ni lako, umekumbwa na mazingira baada ya mvua kunyesha ni lako, kwa Rais ni msaada tu,” amesema na kuongeza kuwa;

“Unabeba dhamana ya mkoa, na unasema huu mkoa na watu wake ndio Taifa langu, hatuwapeleki pale mkale raha,” amesema Rais Dkt Samia.

02/09/2026

Dkt Samia awapa 'somo' wakuu wa mikoa

Rais Dkt Samia Suluhu Hassan, amesema kupata uzoefu na kuondoa dhana ya watendaji kujenga ‘falme’ katika maeneo wanayohudumu ni miongoni mwa sababu zilizomfanya kufanya mabadiliko na kuwahamisha baadhi ya wakuu wa mikoa.

Dkt Samia ameeleza hayo Jumatano Septemba 2,2026 wakati wa akiwaapisha wakuu wa mikoa na katibu tawala aliowateua hivi karibuni. Uapisho huo umefanyika Ikulu Ndogo ya Tunguu, Kusini Unguja.

“Moja ni kupata uzoefu kutoka mkoa mmoja kwenda mkoa mwingine. La pili, kutotengeneza ufalme pale ulipo, kwamba ndio kwangu na himaya ulizozijenga ndio za kwako. Hapana, wewe ni mtumishi wa umma, unaweza kutumika popote pale,” ameeleza.

Rais Samia amekumbusha kuwa katika mkutano wake wa mwisho na wakuu wa mikoa aliwaambia kuwa yeye anawachukulia k**a jeshi lake, hivyo hatarajii kuona jeshi hilo likichafuka.

“Huko mliko nimekuwa nikipata taarifa hizi, zile; huyu ana hivi, huyu ana lile. Sasa kuwabadilisha ni kuwaondosha katika matatizo yale ambayo nayapokea. Sasa k**a ulikuwa unajijua una tabia mbaya au yoyote, nenda kajirekebishe, tumikia wananchi k**a inavyotakiwa,” amesema Dkt Samia.

02/09/2026

Dkt Samia ataka usafi ufanywe kila kona

Rais Dkt Samia Suluhu Hassan, amewataka wakuu wa mikoa wote nchini kusimamia usafi wa mazingira katika maeneo yao, akieleza kwa sasa baadhi ya maeneo hali si nzuri.

Kwa mujibu wa Samia, kitendo cha kuwapa madiwani zabuni za usafi ndio kinachosababisha uchafu, kwa sababu hawana uwezo wa kusimamia suala hilo, hivyo halmashauri zinapaswa kubadilika na kuwapa wakandarasi wenye uwezo.

Dkt Samia ameeleza hayo Jumatano Septemba 2,2026 wakati wa akiwaapisha wakuu wa mikoa na katibu tawala aliowateua hivi karibuni. Uapisho huo umefanyika Ikulu Ndogo ya Tunguu, Kusini Unguja.

“Kuna watu wanaweza, wanaomba lakini mnawanyima.Mnawapa madiwani ili mkae nao vizuri, hawa uwezo, miji michafu, imeenea uchafu kila pembe aibu, hatuwezi kuendelea hivyo, nendeni mkasimie usafi, asiyeweza aondolewe,” amesema.

Katika uapisho huo, Rais Samia aliutaja Mkoa wa Dar es Salaam (uso wa Tanzania) akisema hajaridhika na suala la usafi, hasa katika mitaa yake, akiahidi kukaa nao kikao na watendaji wao mkoa huo.

“Lazima tuimarishe usafi wa nchi yetu, tuondoe uchafu. Tunapovutia watalii, mtalii hana kikomo, anapenya penya, kuna wengine wataka kuona tu Dar es Salaam ipoje,” amesema Dkt Samia.

Kampuni ya mbegu Namburi yawataka wakulima  kununua mbegu za mahindi asili ya Mbozi.KAMPUNI ya kuzalisha mbegu ya Nambur...
31/08/2026

Kampuni ya mbegu Namburi yawataka wakulima kununua mbegu za mahindi asili ya Mbozi.

KAMPUNI ya kuzalisha mbegu ya Namburi Agricultural Company imesema mpaka sasa ina zaidi ya tani 500 za mbegu ya mahindi na zingine 30 za mtama bora zikisubiri wanunuzi.

Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo, Dk Mary Mgonja amesema hayo leo Agosti 31 alipozungumza na Vwawa Fm kwa njia ya simu akiwa Dar es Salaam.

Dk Mary ambaye ni miongoni mwa wanawake wachache wanazolisha mbegu mkoani Songwe amesema mbegu ipo kwenye maghala yaliyopo Kijiji cha Hanseketwa na Vwawa wilayani Mbozi na kwamba mbegu zote ni za asili ya mkoa wa Songwe.
Amesema tani 300 ni za mahindi aina ya haibrid na tani 200 ni za mahindi yanayojichavusha huku tani 30 zikiwa za mtama bora na zingine tani nane za alizeti ya mafuta mengi.

Ametoa wito kwa wakulima mkoani Songwe kufika kununua mbegu zenye asili ya mkoa wao na kwamba amepunguza bei ili wakulima wengi wapate.

Nkunyuntila Siwale aipongeza Mahak**a Kuu mkoa wa Songwe kwa usafi wa mazingiraMDAU wa Maendeleo Mkoa wa Songwe ambaye p...
30/08/2026

Nkunyuntila Siwale aipongeza Mahak**a Kuu mkoa wa Songwe kwa usafi wa mazingira

MDAU wa Maendeleo Mkoa wa Songwe ambaye pia ni mfuasi wa taasisi ya Mwalimu Nyerere Nkunyuntila Siwale ameupongeza uongozi wa Mahak**a Kuu ya Mkoa wa Songwe kwa kusimamia vizuri suala la usafi wa mazingira.

Siwale ambaye ni mwanachama mwandamizi wa Chama cha CUF na mkazi wa Mlowo amesema amepita kwenye mahak**a hiyo hivi karibuni ambapo amejionea mazingira safi na yanayopendeza kwa macho na akili za binadamu.

Amesema hayo Agosti 30 alipozungumza na Vwawa Fm kwa njia ya simu akiwa nyumbani kwake Mlowo Wilaya ya Mbozi.

Mdau huyo ametoa kauli hiyo wakati tayari amelipia tangazo kwa mwezi Agosti 2026 akihimiza ofisi za umma, taasisi za uma na binafsi kutengeneza mazingira na kwamba baada ya miezi sita ataviomba vyombo vya dola kukagua usafi mkoa mzima wa Songwe.

Siwale amesema ofisi za mahak**a kuu mkoa wa Songwe zinafaa kupongezwa kwa usafi, lakini pia amedokeza kwamba wafanyakazi wa TARURA wajitathimini kwa uchafu wa barabara nyingi.

Mdau huyo wa maendeleo na mazingira bora Nkunyuntila Siwale amesema yeye anasisitiza usafi kwenye maeneo ya majengo yote yanayotoa huduma za kijamii yakiwamo majengo ya ibada, ofisi za serikali mkoa hadi kijiji, huduma za afya, elimu na maeneo ya vyombo vya habari.

Mwaka 2025 Nkunyuntila Siwale ameonesha nia ya kutaka kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha CUF, lakini hakuteuliwa kwenye chama hicho.

30/08/2026

*Rais Samia: Ndejembi ukakue akili, usiharibikiwe*

Rais Samia Suluhu Hassan, amemtaka Makamu wa Rais, Deogratius Ndejembi kuhakikisha anatumia wadhifa aliopewa kukua kiakili badala ya kuharibikiwa.

Mkuu huyo wa nchi, ameyasema hayo leo, Agosti 29, 2026 wakati wa hotuba yake baada ya uapisho wa Ndejembi uliofanyika Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma.

Amerejea kauli ya Rais mstaafu wa Zanzibar, Amani Abeid Karume, aliyewahi kuwasihi vijana wasiwe k**a samaki kwa kadiri anavyokua na akili inaharibika.

Rais Samia, amesema pamoja na kumpa majukumu makubwa, anaamini atayamudu.

Address

297 Mbozi
Vwawa

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Vwawa Fm Radio posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to Vwawa Fm Radio:

Shortcuts

Share