24/07/2025
Tabia ya baadhi ya vijana kujisaidia haja ndogo kwenye chupa na kuzitupa ovyo mitaani imeibua hasira kwa wakazi wa mtaa wa Mpendae, Zanzibar.
Asam Online TV imeshuhudia mazingira hayo duni na kuzungumza na wananchi wakiwemo kina mama wa mtaa huo, wakiongozwa na Binti Amrani, ambao wamesema hali hiyo si tu ni uchafuzi wa mazingira bali pia ni tishio kwa afya ya jamii.