Pemba News Media

Pemba News Media Kwa habari za ndani na nje ya nchi na matukio mbalimbali ya kijamii tafadhali tembelea ukurasa wetu

05/11/2024
05/11/2024

Kilimo, kilimo, kilimo.

Kuna fursa nyingi zitokanazo na kilimo, fikiria na chukua hatua.

05/11/2024

Karibuni Mabiyani Kusini Pemba.

Munapajua hapa?

Moja kati malengo yangu tokea kuchaguliwa kuwa Rais wa wachafunzi wa chuo cha ICPS - Zanzibar ni kuleta maendeleo ya har...
02/09/2024

Moja kati malengo yangu tokea kuchaguliwa kuwa Rais wa wachafunzi wa chuo cha ICPS - Zanzibar ni kuleta maendeleo ya haraka katika kila sekta na jana Alhamdulillah ndoto zangu zimeanza kufanikiwa katika sekta ya michezo baada ya kupata Ubingwa na kubeba kombe la ligi ya Elimu bila ya Malipo kwa vyuo vya Amali Zanzibar, hii ni baada ya kuichapa 3 bila timu ya Microtech katika dimba la Mau. Hongereni sana wachezaji, hongereni sana Uongozi wote wa ICPS hakika hiki ndio chuo bora zaidi Zanzibar karibuni sana.

Video na picha za ushindi zitafuata baadae ila nazidi kuwaahidi, k**a tulivyochukua ubingwa kimichezo pia tutakua mabingwa katika sekta zote nyengine Inshallah. Serikali yenu imejipanga zaidi kuhakikisha ufaulu unakua bora, tunazalisha wanafunzi wenye viwango na wenye uwezo wa kupambana na maisha mara wanapomaliza chuo, tunatarajia kutoa wanafunzi ambao watakua na uwezo wa kuague mambo tofauti kimaisha nk. Ukihitaji ubora katika elimu njoo ujiunge ICPS

https://forms.gle/yX3MzDF2Nax819K26Habari yako. Naitwa *SALMIN JUMA SALMIN* naomba unipigie kura ili kuniwezesha kushind...
23/08/2024

https://forms.gle/yX3MzDF2Nax819K26

Habari yako. Naitwa *SALMIN JUMA SALMIN* naomba unipigie kura ili kuniwezesha kushinda katika *tuzo* za Wanavyuo Tanzania.

Nimeshindana katika nafasi ya Watangazaji bora vyuo Vikuu kupitia chuo changu cha *ICPS*.

*JINSI YA KUPIGA KURA.*

Fungua link hii https://forms.gle/yX3MzDF2Nax819K26
utaona email yako, *iguse* itajitik, baadae shusha chini utaona neno *BEST MALE PRESENTER* nitafute mimi *SALMIN JUMA SALMIN* kuna picha yangu pia, kisha gusa picha hiyo, shusha tena chini utaona neno *submit* ikiligusa itakua umenipigia kura.

Naiwakilisha *Zanzibar* katia hili, naomba Sapot yako pls. Pia nisaidie kuwasambazia na wengine. Allah atakulipa kheri Inshallah.

Voting for nominees in uni awards 2024 (hakuna kusupp)

Karibu sana katika chuo cha ICPS Chukwani Zanzibar.
23/07/2024

Karibu sana katika chuo cha ICPS Chukwani Zanzibar.

16/07/2024

Nimeoendekezwa kugombea Nafasi ya Kiongozi bora kijana mwenye ushawishi katika jamii yake, naomba nipigie kura, fungua link ya hapo chini.

https://www.instagram.com/p/C9ZOECgtLy8/?igsh=MXg3czZpeTh5M3IzYw==

Habari zenu wadau wangu.

Naomba nipigieni kura km ifuatavyo. Tafadhali tizama video hii kisha Fungua link hii. Nenda sehemu ya Comments shusha kidogo utakua neno limeandikwa Yes Win liguse heno hilo itakua umenipigia kura.

Nipigie ili kuzidi kuipa nguvu jamii.

Shukran sana

Imeandikwa na Mwandishi wetu - ZanzibarMwenyekiti wa “Tume Huru ya Uchaguzi ya Serikali ya Wanafunzi” wa Chuo cha Instit...
07/06/2024

Imeandikwa na Mwandishi wetu - Zanzibar

Mwenyekiti wa “Tume Huru ya Uchaguzi ya Serikali ya Wanafunzi” wa Chuo cha Institute Of Continuing and Professional Studies (ICPS) Ndug Hassan Haji Mwadini amesema, tume imekalisha jukumu la kusimamia matakwa ya wanafunzi ya kupata raisi wa awamu ya kumi (10) wa chuo na kilichobakia ni kusubiri kuapishwa kwa raisi huyo mteule na kuanza utekelezaji wa majukumu yake.

Kauli hiyo ameitoa jana alikupokua akizungumza na mwandishi wa habri hizi aliyetaka kufahamu kuhusu mchakato wa uchaguzi ulivyokua na jinsi alivyopakana raisi mteule chuoni hapo, ambapo amesema, uchaguzi ulikua huru na wa haki na kila mgombea alipata haki yake na hakukua na masikitiko yoyote.

Akiendelea kueleza amesema, uchaguzi ulitanguliwa na kampeni za kujinadi kwa wagombea wote wa urais na kila mmoja alitoa ahadi zake na ushawishi wake, hatimae mmoja ameibuka mshindi na anatarajiwa kuapishwa rasmi tarehe 08 June 2024 saa 4 asubuhi hapohapo chuoni kwao Chukwani Zanzibar

“ uchaguzi haukua na chembe ya wasiwasi wala ghushi, mambo yalikua waziwazi kwa kila mtu, na wanafunzi ambao ndio wapiga kura walijitokeza kwa wingi, na tulipohesabu kura hizo, sisi na mawakala wa wanafunzi wa wagombea, kwapamoja tulidhirika kuwa Nd Salmin Juma Salmin amekua rais mteule kwa kuwashinda wagembea wenzake wawili katika kinyang’anyiro hicho cha uraisi wa chuo” alisema Mweyekitu huyo.

Sabah Salum Mohd wakala wa mgombea urais ndg Abrahman Rashid (Mhasibu) amesema, uchaguzi ulikwenda vizuri na hakukua na changamoto kubwa ambazo zingeathiri uchaguzi huo “ukweli tuuseme, asiekubali kushindwa si mshindani, mambo yalikwenda waziwazi na mgembea wangu alishindwa nikiwa naona, sikua na jinsi zaidi ya kukubaliana na matokeo, alisema Sabah.

Nae Nassra Savor, wakala wa mgembea ndg Salmin Juma amefahamisha “nyota njema huonekana asubuhi, nilisimama katika uwakala wangu kwa uhakika wa ushindi, mgembea wangu alikua ana kila sababu, mtanashati, mtimiza ahadi na ana mawazo makubwa ya kimaendeleo ya kuwasaidia wanafunzi, kwa wote waliyomsikiliza hawakuacha kumpa kura, mana si rahisi kumsikiliza kisha usimuunge mkono, na kura alizozikosa pengine wanafunzi hao hawakuwepo siku ya kampeni” alisema Savor.

Kwaupande wake Mlezi wa Wanafunzi chuoni hapo ambae pia ni Mkufunzi katika fani ya Manunuzi (Procurement) Mr Khamis Othman Hamad amesema, wao k**a chuo wameridhika na mchakato wote wa uchaguzi huku akimtakia kheri raisi mteule “kimsingi, tunamtakia kila la kheri mteule , kushinda ni jambo moja na kupiga kazi ni jambo jengine, tunamsihi akawasaidie wenzake na chuo kwa ujumla, kwakua ameshapita nasi tunamuamini” mwisho wa kunukuu.

Jumamosi ya tarehe 08 June mwaka huu, katika viunga vya chuo cha ICPS ndio siku inayoratajiwa kufanyika sherehe za kuapishwa kwa rais mteule Nd Salmin Juma Salmin baada ya kushinda kwa ushindi wa 64% dhidi ya wapinzani wake ndg Ibrahim Mohd Haji aliyepata 6% ya kura na Ndugu Abrahman Rashid Mhasibu ambae alipata 28% ya kura hizo, jumla ya kura zote zilizopigwa na 348

Sherehe za kuapishwa raisi wa serikali ya wanafunzi wa chuo hicho zitahudhuriwa na wageni waalikwa mbalimbali wakiwamo kutoka Serikalini (SMZ) taasisi binafsi na wananchi wa kawaida.

Chuo cha Institute Of Continuing and Professional Studies (ICPS) kipo Chukwani Zanzibar na kinasomesha masomo tofauti kwa ngazi mambali mbali kuanzia cheti na kuendelea na kozi zinazosomeshwa ni pamoja na Project Planning and Management, recording and achieve management, human resource management, information Communication technology, accountancy , procurement and supply , early childhood and primary education, na business operations assistant –BOA

ICPS CONTACT

+255776767494 or +255654585060

Karibuni Sana ICPS chuo bora, chenye hadhi ya juu na chenye ubora wa Wakufunzi na mazingira ya ufundishaji. Tunajambo le...
06/06/2024

Karibuni Sana ICPS chuo bora, chenye hadhi ya juu na chenye ubora wa Wakufunzi na mazingira ya ufundishaji. Tunajambo letu keshokutwa Inshallah, nawaalika wote wafuasi wangu mtandaoni, sasa ni wakati wa ICPS, karibuni sana Post inajieleza.

Chuo kipo Chukwani njia ya kuelekea TCRA

Taarifa kuhusu kukosekana Petrol Zanzibar
16/04/2024

Taarifa kuhusu kukosekana Petrol Zanzibar

Jumuiya ya KPDO inatangaza kifo cha Bi Najma Khalfan ambae ni mtu wa Kinyasini Wete Pemba.Bi Najima amefikwa na umauti l...
12/04/2024

Jumuiya ya KPDO inatangaza kifo cha Bi Najma Khalfan ambae ni mtu wa Kinyasini Wete Pemba.

Bi Najima amefikwa na umauti leo katika hospitali ya Mnazi Mmoja na Maziko yanatarajiwa kua leo baada ya Alaasiri Kijichi Unguja Inshallah.

Bi Najma aliwahi kuwa mtangazaji wa STZ (ZBC) baadae Radio Swahiba pamoja na nafasi nyengine za Uongozi.

Poleni sana wanafamilia, poleni sana watu wote wa Kinyasini Wete Pemba, poleni Wanahabari, poleni wawakilishi nk

Inna lillahi Wainna Ilyhirajiun.

Address

KISAUNI
Zanzibar City

Telephone

+255772997018

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Pemba News Media posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share