
14/09/2025
Viongozi wa dini nchini wametakiwa kuendelea kuiombea nchi amani na mshik**ano hasa katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika mwezi Oktoba mwaka huu.
Wito huo umetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Mhe Hamida M***a Khamis huko katika kanisa la Penticost Celebration Feroship Kidimni katika ibada maalum ya kuwaombea duwa Viongozi wakuu na Taifa kwa ujumla
Amesema jukumu la kuhakikisha nchi inabaki kuwa na utulivu ni la kila mwananchi, hivyo waumini wana wajibu wa kipekee kuendelea kuiombea nchi na viongozi wake walioko madarakani ili waweze kuendelea kuliongoza Taifa.
Ameelezakuwa Kila muumini anapaswa kuonyesha mfano wa upendo na kuvumiliana hata wanapokuwa na mitizamo tofauti ya kidini, kabila au siasa kwani Tanzania ni yetu sote hivyo tunawajibu wa kuhakikisha nchi inaendelea kubaki salama.
Akisalimia waumini wa kanisa hilo Mkuu wa Wilaya ya Kati Rajab Ali Rajab amewahimiza waumini kushiriki uchaguzi kwa amaniI na kutokubali kutumiwa k**a chombo cha kuchochea vurugu hususani katika kipindi cha Uchaguzi
Amesema jukumu la kuhakikisha nchi inabaki kuwa na utulivu ni la kila raia hivyo endapo atatokea mchungaji au waumini anahubiri maneno ya kuvunja amani basi waumini hawapaswi kumuunga Mkonoi
Awali akiongoza ibada ya sala Mwenyekiti wa Wachungaji Mkoa wa Kusini Unguja Bwana Edward Jackson Lenjima amesema atahakikisha waumini wao kutumia kipindi hiki kusimama katika maombi kwa kumuomba Mungu aendelee kuwalinda viongozi wakuu na nchi dhidi ya vurugu, migawanyiko na chuki za kisiasa.