The New Bohat Bollywood 102.9fm

The New Bohat Bollywood 102.9fm The new bohat Bollywood is about indian film,songs and news

BRAHMASTRA IS UNSTOPPABLE    Yaibuka BIGGEST WEEKEND OF ALL TIME FOR A HINDI FILM. Ijumaa - ₹ 37 cr Jumamosi- ₹ 42 cr Ju...
12/09/2022

BRAHMASTRA IS UNSTOPPABLE

Yaibuka BIGGEST WEEKEND OF ALL TIME FOR A HINDI FILM.

Ijumaa - ₹ 37 cr
Jumamosi- ₹ 42 cr
Jumapili- ₹ 45 cr

Weekend- ₹ 125 cr
LUGHA ZOTE INDIA

LUGHA YA KIHINDI BIZ
Ijumaa - ₹ 32 cr
Jumamosi- ₹ 37 cr ( 15.80 % ongezeko)
Jumapili- ₹ 41 cr ( 11 % ongezeko )

LUGHA ZA KUSINI - ₹ 15 cr .

NAMBA MOJA KWA FILAMU ZA KIHINDI KWA WEEKEND YA KWANZA MDA WOTE (All time):-
1. - ₹ 125 cr
2. - ₹ 120 cr
3. - ₹ 114.93 cr
4. - ₹ 105.55 cr ( 1st 3 days)
5. - ₹104.53 cr

ZINGATIA - & hazikutoka kwenye siku za sherehe (festivals).

CHAKDE PHATE BOLLYWOOD

Tunaambiwa kua JR NTR msanii nguli na mwenye sura ya mauzo atahudhuria (grace) ktk maonesho ya mwanzo (pre-release) ya f...
28/08/2022

Tunaambiwa kua JR NTR msanii nguli na mwenye sura ya mauzo atahudhuria (grace) ktk maonesho ya mwanzo (pre-release) ya filamu ya BRAHMASTRA ambayo yatafanyika ktk mji wa HYDERABAD unaopatikana katika jimbo la wasichana warembo TELANGANA.

Watengenezaji wa filamu ya BRAHMASTRA nahisi wameamua kumuhusisha bwana huyu ili waue upepo mbaya wa kisuli suli cha mauzo unaoendelea kundirima huko BOLLYWOOD.

BOLLYWOOD kwa sasa imekua ikiwasujudia wasanii wa kusini maana ndio wenye nyota zao.

BRAHMASTRA itatoka 9.9.2022 ikiwa staa wakubwa ni RANBIR KAPOOR na ALIA BHAT wakisaidiwa na AMITABH BACHCHAN , MOUNI ROY na NAGARJUNA.

Tukae mkao wetu wa kusibiri lolote litakalowakuta ila safari hii tunawatakiwa mafanikio ili wajawazito wasijepata uchungu kabla ya muda (ALIA BHAT) 😆

Haya njooni tugawane hasara (Disaster)😆hizi ni filamu 20  za BOLLYWOOD zilizoachiwa kwenye kumbi za sinema mwaka 2022 na...
27/08/2022

Haya njooni tugawane hasara (Disaster)😆

hizi ni filamu 20 za BOLLYWOOD zilizoachiwa kwenye kumbi za sinema mwaka 2022 na zikashindwa kujiuza.

Wenyewe tunasema zimelala yooo😆

Tutakuja zichambua moja badala ya moja ila hizi 3 yaani ANEK, OM na ATTACK ni mapacha wa mama tofaut 😂.

Hili ni pigo letu wote hakuna wa kumcheka mwenzake vile siku hazigandi. tuonane OTT.

Haya kati ya hizi 20 ipi unaihurumia zaidi 😂 mimi naihurumia RAKSHAK BANDHAN natamani isingekua miongoni mwao.

LAAL SINGH CHADHA baada ya kuiona nimegundua kua inastahili kuwepo kwenye hili kundi.

Can we take just a moment to look the beauty of this charming woman.😮 Miongoni mwa wadada watulivu kuwahi kutokea BOLLYW...
27/08/2022

Can we take just a moment to look the beauty of this charming woman.😮

Miongoni mwa wadada watulivu kuwahi kutokea BOLLYWOOD.

Ni mdogo kiumri kuliko wenzake ila mafanikio yake ni makubwa, tokea aolewe ni mtu wa furaha kila sekunde, she is really grateful.

upendo wetu kwake unazidi kumea, tunamtakia kila zuri ktk kipindi hiki kigumu cha ujauzito wake.

Our SUNSHINE GIRL 🌻.

ALIA BHATT KAPOOR.

FILAMU YA LAAL SINGH CHADHA YAIBUA JINA JIPYA SOKONI LA MAUZO MABOVU.Hakika usimtusi mamba kabla hujavuka mto, filamu am...
16/08/2022

FILAMU YA LAAL SINGH CHADHA YAIBUA JINA JIPYA SOKONI LA MAUZO MABOVU.

Hakika usimtusi mamba kabla hujavuka mto, filamu ambayo ilitarajiwa kurudisha haiba ya BOLLYWOOD katika ramani ya mauzo ambayo pia ni filamu ya msanii mkongwe, hodari, fundi na mtawala wa mauzo yaangukia komwe.

Filamu ya LAAL SINGH CHADHA ya kwake AMIR KHAN licha ya kuchukua muda mrefu kutengenezwa na kupambwa hatimae imezimwa kirahisi mno, filamu hii imeshindwa kabisa kurejesha hadhi ya BOLLYWOOD na badala yake imeingia katika shimo lile lile walilodumbukia wengine.

Licha ya filamu hii kupata siku 5 za holiday ila imeshindwa kujikwamua na kwa siku ya leo jumanne inasemekana imeingiza si zaidi ya 2Crore hivyo filamu hii rasmi imepewa jina la ELEPHANTINE DISASTER yaani hasara kimo cha tembo 😭.

Poleni sana washabiki wa Amir khan na poleni sana washabiki wa BOLLYWOOD na hili litapita.

MDADA WA MIAKA 40 AIGIZA MAMA WA MBABA WA MIAKA 57 WADAU WAJA JUU.Ikiwa ni wiki kadhaa zimepita za ukimya wa page yetu h...
15/08/2022

MDADA WA MIAKA 40 AIGIZA MAMA WA MBABA WA MIAKA 57 WADAU WAJA JUU.

Ikiwa ni wiki kadhaa zimepita za ukimya wa page yetu hii ni kutokana na majukumu mapya ya kimaisha yanayoibuka siku hadi siku na kutufanya kutumia muda mwingi kuyaweka sawa ili tusijeumiza uhalisia kwa kuweka sawa burudani. Lakini haimaanishi kua tumeacha na k**a hivi tunarudi tena kuendeleza moto 🔥

Kuna mengi tutayaleta kuhusiana na filamu ya LAAL SINGH CHADHA ila moja ya gumzo liloibuka ni baada ya Mwanamama MONA SINGH mwenye umri wa miaka 40 alipoonekana akiigiza mama wa AMIR KHAN mwenye miaka 57 kitu ambacho mtoto alimzidi miaka 17 mama yake.

Baada ya hadhira kukosoa jambo hili ndipo mwanamama huyu MONA SINGH alipojibu kua yeye hakuigiza mama wa AMIR KHAN bali aliigiza mama wa LAAL katika filamu hivyo maisha na umri wao wa kweli hauhusiani na wa kwenye filamu.

SISI K**A WAPENZI WA FILAMU MAONI YETU NI HAYA.
Siku zote ili filamu ibaki katika ubora inapaswa iepuke sintofahamu zinazoepukika na panapowezekana uhalisia upatikane sababu kwao wao waigizaji ni filamu kwetu sisi ni hadithi ya kweli na kwa vile tunawajua wote hatutokubali kudanganywa mama huyu wa miaka 40 aigize mama wa baba wa miaka 57 hii ni kuumiza uhalisia. Ingawa LAAL alipokua mdogo ndio lengo la huyu mama kuwepo ila alipokua mkubwa walishdwa kufikiria tutachukuliaje. Licha ya yote vile uigizaji ni mzuri basi wanastahili pongezi ila kuufunika ukweli ni ngumu.

NINI MAONI YAKO..? JEE UNAHISI NI SAHIHI WALIVYOFANYA..?

AKSHEY KUMAR NA RAKSHAK BANDHAAN Wiki inayofata tutaishuhudia hii filamu ikitupa karata yake katika majumba ya sinema hu...
01/08/2022

AKSHEY KUMAR NA RAKSHAK BANDHAAN

Wiki inayofata tutaishuhudia hii filamu ikitupa karata yake katika majumba ya sinema huku ikitarajiwa kuwa na clash (upinzani) mzito kutoka kwa AMIR KHAN na filamu yake ya LAAL SINGH CHADHA.

Binafsi hii filamu ya RAKSHAK BANDHAAN imetokea kutuvutia wengi nikowemo mimi, hii filamu nimejikuta natamani sana niione na katika miaka ya karibuni kwa filamu zote alizoachia AKSHAY naweza sema hii ndio nimekuta naitamani zaidi na zaidi.

Kitu kikubwa kilichonivutia ni baada ya kusikia nyimbo zake mbili zilizoachiwa ambazo ni.

1) Teri saathi hoon main - Hii nyimbo kaimba NIKHIL na ndio instrumental yake inayotumika k**a main theme ya hii filamu. Hii nyimbo imetulia sana ni aina ya nyimbo ambayo ukiisikia kwa mara ya kwanza unaweza sema ni ya miaka chini ya 2010 kwa melody yake na utulivu. Ni nyimbo ambayo hata bila kuijua maana unajikuta unaisikiliza maneno yanavotamkwa jinsi yalivopambwa na sauti ya NIKHIL inayopanda na kushuka kwenye chorus.

Nyimbo ya pili ni

2) Dhagoon se bandha - hii wameimba ARJIT SINGH na SHREYA GHOSHAL, ni nyimbo nyengine tamu sana sana sana , Shreya ameifungua hii nyimbo vizuri sana kwa sauti yake maridadi ya kusafisha masikio na kuibua mapigo ya moyo yaende haraka haraka, ARJIT baadae amekuja kuibeba hii nyimbo hadi mwisho hadi nakosa usemi, nyimbo ambazo tunazihitaji kabisa , hakika hii album ndio playlist yangu siku hizi.

Kazi mzuri sana sana kwa waandaaji wa music wa hii filamu.

FILAMU IPO MABEGANI MWA AKSHEY music tayari umekua na rate mzuri 4.5/5 ingawa udhaifu mdogo upo kwenye video za nyimbo hizi zote zimefanana hutofautishi.

UNAZIONAJE HIZI NYIMBO..?

Uliza swali lolote kwetu sisi page kuhusiana na  ishu za kihindi.Leo tunataka style mpya maswali yawe ya funny zaidi usi...
30/07/2022

Uliza swali lolote kwetu sisi page kuhusiana na ishu za kihindi.

Leo tunataka style mpya maswali yawe ya funny zaidi usiulize maswali kuhusu wasanii tuulize sisi tutoe maoni yetu kuhusu kitu chchte mfano (muigizaji tunaempenda, filamu bora 2022 au mwaka flani, nyimbo mzuri, filamu kufeli, yaani yawe maswali ambayo bado hayana jibu sip yale Salman ana movie ngapi, filamu flani kaigiza nani, tiger anaisha wapi aya tayari yana majibu)

NADHANI TUMEELEWANA, HAYS TUANZE KAZI TUULIZE KABLA HATUJASHUSHA MAHABARI MAPYA YA LEO...🤨

BIPASHA BASU NA KARAN SINGH GROVER NI WAZAZI WATARAJIWA.Mungu si athumani ile ndoa ya watu wazuri zaidi iliyotuvutia kwa...
29/07/2022

BIPASHA BASU NA KARAN SINGH GROVER NI WAZAZI WATARAJIWA.

Mungu si athumani ile ndoa ya watu wazuri zaidi iliyotuvutia kwa wengi hatimae imebarikiwa kupata ujauzito.

Bipasha na Karan walifunga ndoa mwaka 2016 baada ya miaka 7 sasa ndio wanabarikiwa ujauzito.

Pea yangu pendwa kabisaaaa, nawapenda mno hawa watu. Mungu awabariki wapate kizazi chema.

New parents to be👏👏

TIGER SHROF NA DISHA PATANI WAMWAGANA.Lile penzi refu k**a filamu ya ISIDINGO la wapendwa wetu DISHA PATANI na TIGER SHR...
29/07/2022

TIGER SHROF NA DISHA PATANI WAMWAGANA.

Lile penzi refu k**a filamu ya ISIDINGO la wapendwa wetu DISHA PATANI na TIGER SHROF hatimae lafikia mwisho baada ya miaka 6.

Wawili hawa walianza uhusiana wao mnamo mwaka 2017 walipokua ktk utengenezaji wa filamu ya BAAGHI 2 ndipo waliposhibana na ikawa ni moja ya couple zilizokua na utulivu zaidi.

Baada ya uhusiano wao huo watu wengi walisema hii couple ilikua ikilewa lewa kutokana na kua DISHA PATANI ni msichana wa bei ghali na TIGER ni mtu aliyepoa (mtulivu).

Kuna fununu zinadai TARA SUTARIA kaingilia kati penzi hili.

JEE UNADHANI NANI CHANZO CHA KUACHANA KWAO.

ALIA BHATT NA SRK WATUPIANA MESSAGE ZA MAHABA.Baada ya siku chache kuachiwa kionjo cha filamu mpya ya ALIA BHATT inayoit...
29/07/2022

ALIA BHATT NA SRK WATUPIANA MESSAGE ZA MAHABA.

Baada ya siku chache kuachiwa kionjo cha filamu mpya ya ALIA BHATT inayoitwa DARLINGS ambayo ndio filamu yake ya mwanzo ALIA kua k**a PRODUCER na inayomilikiwa na kampuni yake ya ETERNAL SUNSHINE PRODUCTION ikishirikiana kwa ukaribu na urafiki na kampuni ya SRK na GAURI KHAN ya RED CHILLS ENTERTAINMENT.

Baada ya kionjo hicho SRK na ALIA BHAT walianza kuchati huko twitter kwa kupeana maneno mazuri huku SRK akisema yupo na shauku na filamu hiyo na kila wakati anabaki kutafuna kucha zake tu akiifikiria.😆

ALIA alimjibu kua SRK ndio msanii wake pendwa na itabidi baada ya filamu kutoka waende saloon kutengeneza kucha zao maana zitakua zote zimeharibika kwa kutafunwa.😂.

Chati hii imetufarijisha mioyo yetu kuona kuna uhusiano mzuri kati ya wasanii hawa mashahuri.

OUR DARLINGS 🌻 ni mwendo wa njano tu.

SANJAY DUTT AMTIA MOYO RANBIR KAPOOR BAADA YA FILAMU YAO KUDONDOKEA USO.Muigizaji mkongwe SANJAY DUTT amempa maneno ya f...
29/07/2022

SANJAY DUTT AMTIA MOYO RANBIR KAPOOR BAADA YA FILAMU YAO KUDONDOKEA USO.

Muigizaji mkongwe SANJAY DUTT amempa maneno ya faraja muigizaji kinda RANBIR KAPOOR baada ya filamu yao ya SHAMSHERA kufanya vibaya sokoni.

SANJU amemwambia RANBIR haijalishi filamu yake itauza bei gani k**a ni mzuri itatafuta na kupata watazamaji hata baadae.

SANJU amesema sio kila kizuri kinakupa faida kuna vengine inabidi ujitoe sadaka na mafanikio ya filamu ni zaidi ya mauzo bali jinsi gani itadumu kwenye mioyo ya watu siku za usoni.

Muigizaji huyu mkongwe ametamka maneno hayo kutokana na uzoefu wa matukio k**a hayo ya kufeli filamu zake lakini bado akapata jina na upendo kutoka kwa watu.

JEE UNAKUBALIANA NA MANENO YA SANJU BABA...?

KAMPUNI YA YASH RAJ YALAANIWA KWA KUMTUMIA VIBAYA VAANI KAPOOR.Kampuni kongwe na mashuhuri ya filamu INDIA kwa kutoa fil...
29/07/2022

KAMPUNI YA YASH RAJ YALAANIWA KWA KUMTUMIA VIBAYA VAANI KAPOOR.

Kampuni kongwe na mashuhuri ya filamu INDIA kwa kutoa filamu mzuri na za kusisimua YASH RAJ COMPANY ambayo kwa mwaka 2022 imejikuta ikitumia kuni na kuingiza jivu (kupata hasara kubwa) kwa kufeli filamu zake kubwa zote k**a JJ, PRITHIVRAJ na SHAMSHERA imejikuta ikipokea laana za mashabiki baada ya matumizi mabaya ya mrembo VAANI KAPOOR.

Kampuni hii imeshtumiwa kwa kuwalaghai watazamaji kua filamu ya SHAMSHERA itakua na uhusika wa mrembo VAANI KAPOOR k**a ndio malkia wa filamu.

Baada ya kutoka filamu hii imeonekana kua VAANI KAPOOR alitumiwa katika kuitangaza tu filamu kwani uhusika wake ulikua ni mdogo kupitiliza usiokua na thamani.

VAANI KAPOOR alipewa nafasi ya kua mchumba wa RANBIR (love interest) ambae alionekana mara chache sana kwenye filamu mzima.

Wadau wa filamu wamelaani kitendo hiki na kusema wamedharau nafasi ya mwanamke badala yake wamemfanya ni sehem ya starehe tu.

JEE UNA MAONI GANI JUU YA MWANAMKE KUPEWA NAFASI NDOGO NAMNA HII..?

AMTAMANI MTOTO WA SHAH RUKH KHAN, ACHANWA KUA ANAFATA PESA.Muigizaji machachari ANANYA PANDEY mtoto wa mkongwe CHUNKY PA...
29/07/2022

AMTAMANI MTOTO WA SHAH RUKH KHAN, ACHANWA KUA ANAFATA PESA.

Muigizaji machachari ANANYA PANDEY mtoto wa mkongwe CHUNKY PANDEY ametoa donge zito la moyoni juu ya yeye kutamani kua na mahusiano na A***N KHAN mtoto wa SRK.

ANANYA ambae kwa sasa anatamba na ujio wa filamu yake ya LIGER ametoa kauli hiyo mara baada ya kuulizwa na KARAN JOHAR katika kipindi cha KOFFEE WITH KARAN.

ANANYA amesema A***N ni mzuri hivyo ndio crush wake (mtu anaemfukuzia).

Baada ya kuenea kwa mazungumzo haya watumiaji mitandao wameonekana kumshambulia ANANYA na kusema kua anafata utajiri wao A***N na sio penzi.

JEE UNAHISI WAWILI HAWA WANAENDANA..?

PATHAAN ON THE WAY.Angalia hii gaze ya DEEPIKA 😱 She is constantly amazing. YASH RAJ wasijetuangusha kwenye hii maana ca...
26/07/2022

PATHAAN ON THE WAY.

Angalia hii gaze ya DEEPIKA 😱 She is constantly amazing. YASH RAJ wasijetuangusha kwenye hii maana cast mzuri story ikiwa mbovu hatutowasamehe.

SRK looking promising, pozi lake namna alivyoshika bomba well well well.

DEEPIKA ni new avatar, our very own BOLLYWOOD wonder woman.

IVI KWANINI WANAWAKE WA KIHINDI WAKIIGIZA MOVIE ZA MAPIGANO AU ADUI LAZIMA WAPUNGUZE NYWELE 😆

APOKEA KICHAMBO KWA KULIZARAU SOMO LA HESABU.Muigizaji mrembo tishio kwa shepu yake machachari JANHVI KAPOOR amejikuta a...
26/07/2022

APOKEA KICHAMBO KWA KULIZARAU SOMO LA HESABU.

Muigizaji mrembo tishio kwa shepu yake machachari JANHVI KAPOOR amejikuta akipakaziwa baada ya kusema kua somo la hesabu halina msaada wowote ktk maisha yake.

JHANVI alisema ktk kipindi cha KOFFEE WITH KARAN kua hajawahi kuitumia hesabu ya ALJEBRA katika maisha yake ingawa hesabu hiyo ilimsumbua sana shuleni lakini History na maarifa ndio masomo yanayomsaidia kila siku.

Mashabiki walianza kumshambulia mitandaoni na kumuita akili mbovu baada ya maoni yake hayo.

JEE WEWE HESABU YA ALJEBRA INEKUSAIDIA 😆

ASHTAKIWA KWA KUUMIZA HISIA ZA WANAWAKE.Muigizaji RANVEER SINGH ambae alikua story ya mjini baada ya kusambaa picha zake...
26/07/2022

ASHTAKIWA KWA KUUMIZA HISIA ZA WANAWAKE.

Muigizaji RANVEER SINGH ambae alikua story ya mjini baada ya kusambaa picha zake za nusu utupu mitandaoni amejikuta akipokea lawama nyingi na zengine zikidaiwa kufikishwa mahak**ani.

Muigizaji huyo ambae ni mume wa mrembo DEEPIKA PADUKONE amefunguliwa kesi kwa kosa la kuziumiza hisia za wanawake kwa picha zake zilizoonesha jinsi mwili wake ulivyo umbika kitendo kilichowafanya wadada wengi kumtamani.

Hadi sasa hatujui ni nini kitaendelea baada ya kesi hii.

Tukumbuke picha hizo alipiga kwa ajili ya cover ya jarida.

KOSA LAKE AU LA WATAZAMAJI WANAO ZOOM 😆

BEAUTY WITH BRAIN.Miongoni mwa warembo wenye uwezo mkubwa wa kujieleza ni SAMANTHA RUTH PRABU.Mrembo kutokea TELUGU amba...
24/07/2022

BEAUTY WITH BRAIN.

Miongoni mwa warembo wenye uwezo mkubwa wa kujieleza ni SAMANTHA RUTH PRABU.

Mrembo kutokea TELUGU ambae karibuni aliingia ktk kashfa baada ya kuachana na mumewe NAGA CHAITANYA.

Nimetokea kumpenda sana huyu dada baada ya kuangalia interview zake, swala kubwa ni kua hamuangushi mtu ili aonekane mwema anatoa hoja zinazomlinda hadi ex wake. SAMANTHA amebariki upeo anajua kuongea na waandishi hana papara, wala hana ile excitement iliyopitiliza hadi akasahau asili yake.

KARAN JOHAR alimtwanga maswali magumu ila yote alichomoa na kila mmoja alimpenda hakika huyu dada kiboko.

Karibuni ataitwa kuigiza BOLLYWOOD huyu mrembo na natamani itokee ivyo ingawa ni ngumu sabab wadada wa BOLLYWOOD hawatoruhusu kilaini hiki chombo kitoboe BOLLYWOOD maana upeo wake umezidi kiwango.

Nampenda sana huyu dada 💙 usikose kuangalia Koffe with karan kwenye OTT ilikua episode ya 3 ndio alialikwa huyu dada akipea na AKSHAY KUMAR.

ENGLISH yake ni very grammatical, anaweza kuacha njiani unatafuta dictionary 😆

Address

Mbweni
Zanzibar

Telephone

+255718874223

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when The New Bohat Bollywood 102.9fm posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share

Category