21/02/2025
RC KITWANA AWATAKA WAFANYABIASHARA KUACHA KUBIASHARA PEMBEZONI MWA BARABARA
Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Idrissa Kitwana Mustafa amewataka wafanya biashara kuacha kufanya biashara katika maeneo ya pembezoni mwa barabara na badala yake kufanya biashara zao katika maeneo maalum yaliyotewekwa na Serikali.
Akizungumza na wafanyabiashara wa maduka , mitumba na bidhaa nyengine walio nje ya masoko ya Mwanakwerekwe na Jumbi Mhe Kitwana amesema Serikali imekuwa ikiendelea kuimarisha mazingira bora kwa wafanya biashara hivyo si jambo jema kuendelea kufanya biashara katika njia wapita kwa miguu na maeneo ya akiba ya barabara.
Ameleza kuwa kumekuwa na kawaida wauza maduka kuweka bidhaa za nje ya maduka jambo ambalo limekuwa likipoteza haiba nzuri ya mji na kusababisha msongamano wa watu jambo ambalo ni magari kinyume na utaratibu wa sheria .
Aidha amewasisitiza wafanyabiashara kufanya biashara kwa mashirikiano na kuacha kubaguana kwa upande mtu anaotoka na badala yake kufanya kazi kwa pamoja huku wakijua watanzania wote ni wamoja.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Magharibi B Hamida M***a Khamis ameahidi kusimamia maagizo yaliotolewa kwa kufanya oparation maalum pamoja na kuwataka wafanyabiashara hususani wauza mitumba ambao bado hawajaingia katika maeneo waliyotengewa ndani ya masoko kwenda kufanya biashara zao katika maeneo waliopangiwa.
Oparation hiyo ya kuwaondoa wafanya biashara katika maeneo yasio rasmi ikmekuja kufuatia ongezeka la wafannyabiashara kufanya biashara katika maeneo yasio rasmi jambo linalopoteza haiba nzuri ya mji.
Mwisho.