
09/15/2025
K**A UMEZALIWA FAMILIA MASKINI SOMA UJUMBE HUU MPAKA MWISHO...
Usitazame ni familia gani umetokea fahamu kuwa una uwezo wa kutengeneza utajiri hata k**a umetoka kwenye familia ya hali ya chini namna gani,
_Fahamu njia za kuwa tajiri hata k**a umetoka kwenye familia masikini._
πAnza kuwekeza sasa.
Utajiri haujengwi kwa siku moja bali unatengezwa kwa siku nyingi,
Ili uweze kuwa tajiri lazima uanze kuwekeza sasa ili baadae uweze kumiliki huo utajiri,
Haijalishi ni kiasi gani unachowekeza, bali tabia ya uwekezaji ndiyo muhimu zaidi.
π Lazima ujifunze elimu ya fedha.
Lazima uwe na uelewa kuhusu pesa,
Usipo kuwa na uelewa kuhusu pesa utakuwa mtu wa kuingiza na kutoa pesa tu bila kufanya chochote,
Ili uweze kufanikiwa lazima ufahamu au ujifunze kuhusu elimu ya fedha kwa mwendelezo bila kuacha.
π Weka bajeti kwenye lengo lako.
Ishi kwa kupanga malengo na kuyaandalia bajeti yake.
Ili uweze kufanikiwa lazima uwe na bajeti kwenye lile lengo ambalo unataka kulikamilisha.
Ukitembea hivi hivi hauta weza kufanikiwa utaishia kuwa masikini k**a ulivyo toka kwenye familia yako.
Kumbuka bajeti ni kuiambia pesa yako iende wapi na si kujiuliza imeenda wapi unapokuwa huioni.
π Ishi maisha rahisi.
Usiishi juu ya kipato chako, jitahidi sana matumizi yasizidi kipato chako,
Acha kutumia pesa kifahari wakati ndo kwanza unajitafuta,
Tengeneza kwanza msingi wa pesa zako.
π Kuwa na vyanzo vingi vya mapato.
Kuwa na mgawanyo wa vyanzo vyako vya mapato,
Hii itakusaidia hata k**a chanzo kimoja kiki yumba basi vyanzo vingine vitaendelea kuleta mapato,
Hauta kaukiwa kabisa na mapato.
Note: Kuzaliwa kwenye familia masikini sio kosa ila kosa ni wewe kufa masikini, jitahidi sana uepuke kufa masikini kwa kisingizio cha familia yako.
Learn more to earn more
LEAVE THE GREAT LIFE
benjathekingofficial_new Benjaminlucipaofficial