
09/29/2025
Polisi Wavunja Mtandao wa Usafirishaji Haramu wa Wakenya Kupelekwa Kupigana Nchini Ukraine
Polisi nchini Kenya wamewaokoa zaidi ya watu 20 kutoka kwa mtandao unaoshukiwa wa usafirishaji haramu wa binadamu, uliodaiwa kuwadanganya wakenya waliotafuta ajira kwa ahadi za kazi nchini Urusi, kisha kuwatuma kupigana vitani nchini Ukraine.
Operesheni hiyo ilifanyika kufuatia msako ulioongozwa na taarifa za kijasusi katika eneo la Athi River, viunga vya jiji la Nairobi, ambapo maafisa walik**ata nyaraka za usajili, hati za kusafiria na barua bandia za ofa za kazi.
Mshukiwa mmoja, anayedaiwa kuratibu safari za wahanga mwezi Septemba na Oktoba, amek**atwa na mahak**a ya Nairobi imeruhusu polisi kumzuilia kwa siku 10 ili kukamilisha uchunguzi.
Mamlaka zinasema mtandao huo umekuwa ukiwatoza wakenya fedha nyingi kwa ahadi za kazi zenye malipo makubwa jijini Moscow. Badala yake, wahanga walifichua kuwa walilazimishwa kusaini mikataba iliyowataka kulipa hadi dola 18,000 (takriban shilingi milioni 2.3) kwa ajili ya visa, usafiri, malazi na gharama nyingine. Baadhi yao walikuwa tayari wamelipa malipo ya awali ya dola 1,500.
Polisi walithibitisha kuwa jumla ya Wakenya 22 walipatikana katika nyumba moja eneo la Athi River “wakisubiri kusafirishwa kwenda Urusi.” Uchunguzi unaonyesha mpango wa mwisho ulikuwa ni kuwatuma vitani Ukraine kupigania upande wa Urusi.
Kumekuwa na ongezeko la wasiwasi kuhusu idadi kubwa ya Wakenya wanaosafirishwa nje kwa ahadi za uongo za ajira. Hivi karibuni, mwanariadha kijana wa Kenya alik**atwa nchini Ukraine, akidai alidanganywa kujiunga na jeshi la Urusi. “Mimi ni Mkenya, msinipige risasi,” alisema baada ya kudanganywa kuingia vitani.
Maafisa wanasema wengi wa wanaosafirishwa hurudi nyumbani wakiwa wamejeruhiwa, wameathirika kisaikolojia, au wengine hawarudi kabisa. Wakenya wawili wamerejeshwa hivi karibuni, mmoja wao akiwa amelazwa katika hospitali moja jijini Nairobi.
Wizara ya Mambo ya Nje imethibitisha kuwa inafuatilia taarifa za Wakenya kadhaa waliodaiwa kusafirishwa hadi Urusi na sasa wanashikiliwa k**a mateka wa vita nchini Ukraine.
Ripoti za kimataifa pia zinaonyesha kuwa raia wa Somalia, Sierra Leone, Togo, Cuba na Sri Lanka wako miongoni mwa walioko kwenye kambi za mateka wa vita nchini Ukraine. Msemaji wa Ukraine kuhusu masuala ya mateka wa vita, Petro Yatsenko, aliwahi kuiambia BBC kwamba “mataifa mengi ya Afrika hayaonyeshi nia ya kuwarudisha raia wao na hayapendi kuwapokea tena.”