
07/12/2025
Kwa mujibu wa taarifa za awali zinasema kuwa sababu zilizopelekea Ndege ya Air India kudondoka mwezi Juni 12, 2025 na kuua watu 260 ilitokana na kuzimwa kwa mafuta ya Injini zote mbili za Ndege.
Kwa mujibu wa sauti za Marubani wa Ndege hiyo zilizorekodiwa kwenye Black Box alisikika Rubani mmoja akimuuliza Rubani mwenzake kuwa, "Kwanini umezima mafuta kwenye Injini?, Rubani mwenzake akamjibu Sijafanya hivyo,". Sekunde kadhaa Ndege ikadondoka.