The slate news Updates

The slate news Updates Hii ni page kwa ajiri habari na matukio yakijamii na yakisiasa pia habari za burudani na michezo

06/12/2021

NAFASI ZA *WAUZAJI NA WASAMBAZAJI*
====================

D LIGHT TANZANIA LIMITED ni kampuni ya kuuza na kusambaza vifaa vya nishati jua (Solar Energy products), yenye ofisi zake zilizopo, mtaa wa 57 Haille Selassie, na Sanduku la Posta 1378 Arusha na tawi lake Katika mkoa wa Dodoma pia Iringa

D LIGHT TZ LTD Inayofuraha kutangaza nafasi za wauzaji na wasambazaji wa bidhaa kwa Malipo ya kamisheni katika mkoa wa Dodoma/Iringa na wilaya zake.

*Nafasi:* MUUZAJI (SEP)
*Kuripoti.* WAKALA (EC),
*Kituo ch kazi* DODOMA/IRINGA

*Majukumu*
```kupokea vifaa vya nishati jua kutoka kwa Duka la wakala (Experience Centre)

Kuwasiliana na Wateja kupokea oda wakati wote

Kufuatilia na kuhakikisha madeni ya Wateja yanalipwa kwa wakati.

Kuuza/kufanya biashara ya mauzo ya vifaa vya nishati jua kuzingatia na kuendana na mfumo wa mauzo atakaopangiwa

kufikia malengo ya uuzaji/biaashara aliyowekewa

kuhudhuria mafunzo na semina mbalimbali zitakazokuwa zikitolewa na mkufunzi/wakufunzi kutoka kwa

anapaswa kuwa nadhifu wakati wote wa kufanya biashara ya mauzo na kutumia lugha nzuri na ya ushawishi wa kibiashara.

*Sifa*
Mtanzania
Mkazi wa Dodoma/ Iringa
Mwenye umri wa miaka 18 au zaidi
Awe mwenye akili timamu
Awe na Elimu ya kidato cha nne na kuelendelea
Awe na taaluma ya biashara ambayo ni sifa ya Ziada.

*Ujuzi*
Awe na ujuzi na maarifa ya masoko na biashara.
Udereva wa pikipiki/Gari ni sifa ya Ziada
```

*Mahitaji*
Nakala kitambulisho Uraia (NIDA)
Barua ya utambulisho kutoka Serikali ya mtaa
Picha passport size mbili
Barua ya uthibitisho kutoka kitu cha polisi inayothibitishwa hujawahi kufanya makosa ya jinai
Barua za wadhamini wawili zilizoambatanishwa na picha zao ( passport size) mbili
Nakala za vyeti vya kuhitimu masomo

Tafadhali unaweza kuwasilisha Maombi yako kupitia
Email [email protected]
au wasap number 0655042287
```
Kwa maelezo zaidi piga simu namba
*0655042287*

Mwisho wa kupokea maombi ni ``` *saa 10:00 Jioni Jumatano Tarehe 01 july 2021*

05/20/2021

NAFASI ZA *WAUZAJI NA WASAMBAZAJI*
====================

D LIGHT TANZANIA LIMITED ni kampuni ya kuuza na kusambaza vifaa vya nishati jua (Solar Energy products), yenye ofisi zake zilizopo, mtaa wa 57 Haille Selassie, na Sanduku la Posta 1378 Arusha na tawi lake Katika mkoa wa Dodoma pia Iringa

D LIGHT TZ LTD Inayofuraha kutangaza nafasi za wauzaji na wasambazaji wa bidhaa kwa Malipo ya kamisheni katika mkoa wa Dodoma/Iringa na wilaya zake.

*Nafasi:* MUUZAJI (SEP)
*Kuripoti.* WAKALA (EC),
*Kituo ch kazi* DODOMA/IRINGA

*Majukumu*
```kupokea vifaa vya nishati jua kutoka kwa Duka la wakala (Experience Centre)

Kuwasiliana na Wateja kupokea oda wakati wote

Kufuatilia na kuhakikisha madeni ya Wateja yanalipwa kwa wakati.

Kuuza/kufanya biashara ya mauzo ya vifaa vya nishati jua kuzingatia na kuendana na mfumo wa mauzo atakaopangiwa

kufikia malengo ya uuzaji/biaashara aliyowekewa

kuhudhuria mafunzo na semina mbalimbali zitakazokuwa zikitolewa na mkufunzi/wakufunzi kutoka kwa

anapaswa kuwa nadhifu wakati wote wa kufanya biashara ya mauzo na kutumia lugha nzuri na ya ushawishi wa kibiashara.

*Sifa*
Mtanzania
Mkazi wa Dodoma/ Iringa
Mwenye umri wa miaka 18 au zaidi
Awe mwenye akili timamu
Awe na Elimu ya kidato cha nne na kuelendelea
Awe na taaluma ya biashara ambayo ni sifa ya Ziada.

*Ujuzi*
Awe na ujuzi na maarifa ya masoko na biashara.
Udereva wa pikipiki/Gari ni sifa ya Ziada
```

*Mahitaji*
Nakala kitambulisho Uraia (NIDA)
Barua ya utambulisho kutoka Serikali ya mtaa
Picha passport size mbili
Barua ya uthibitisho kutoka kitu cha polisi inayothibitishwa hujawahi kufanya makosa ya jinai
Barua za wadhamini wawili zilizoambatanishwa na picha zao ( passport size) mbili
Nakala za vyeti vya kuhitimu masomo

Tafadhali unaweza kuwasilisha Maombi yako kupitia
Email [email protected]
au wasap number 0655042287
```
Kwa maelezo zaidi piga simu namba
*0655042287*

Mwisho wa kupokea maombi ni ``` *saa 10:00 Jioni Jumatano Tarehe 01 june 2021*

Rais Mhe Samia Suluhu Hassan akijumuika chakula cha mchana na watoto wenye mahitaji maalum ikulu
04/04/2021

Rais Mhe Samia Suluhu Hassan akijumuika chakula cha mchana na watoto wenye mahitaji maalum ikulu

12/20/2020

MKOPO RAHISI Banc ABC

Ni mkopo kwa watumishi wa umma na ambao wameajiliwa kazi wizarani na baadhi ya watumishi wa Vyuo vikuu.

Sifa za mkopo rahisi.
Kwanza hautumii muda mrefu kuupata.
Hakuna gharama za kuuchakata mkopo.
Pia mkopo wetu unauwezo wa kufuta deni muda wowote mara tu baada yakuupata mkopo.
Na mengineyo tunaweza kuzungumza...

Piga simu 0715123013
Au [email protected]

12/17/2020

TIMIZENI WAJIBU WENU KWA WELEDI NA MAADILI

NA DANSON KAIJAGE,DODOMA

KATIBU Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Idara kuu ya Afya Prof. Mabula Mchembe amewataka Maafisa Afya ngazi zote kufanya kazi zao kwa weledi na kufuata maadili wakati watimizapo majukumu yao katika jamii.

Prof. Mchembe ameyasema hayo, wakati wa Mkutano wa Maafisa Afya mazingira wenye kauli mbiu ya "Zingatia mahitaji ya Jinsia kwa usafi wa mazingira endelevu " uliofanyika Jijini Dodoma.

"Tusimamie maadili sana, usitende kitu kwa kufikiria kwamba unamfanyia fulani, natambua changamoto zipo katika baadhi ya sehemu, lakini tunahitaji kutimiza wajibu wetu kwa maadili na uwaminifu wa hali ya juu" alisema Prof. Mchembe.

Pia, Prof. Mchembe amewataka Maafisa Afya mazingira kusimamia usafi katika maeneo ya huduma za vyoo katika jamii, hususan katika ofisi na vituo vya daladala ambavyo huudumia Jamii kwa kiasi kikubwa ili kuikinga Jamii dhidi ya magonjwa ya milipuko.

Aidha, Prof. Mchembe amewaagiza Maafisa Afya mazingira nchini kusimamia usafi na ubora wa vyakula katika maeneo yote yanayotoa huduma za vyakula, yakiwemo maeneo ya migahawa na hoteli ili kuikinga jamii na magonjwa ya tumbo na kuhara.

Mbali na hayo Prof. Mchembe ametoa wito kwa Maafisa afya mazingira kujiepusha na vitendo vya Rushwa wakati wa wakitimiza majukumu yao na kuhakikisha usafi wa mazingira unaendelea kufuatwa katika ngazi zote za Jamii.

"Tuachane na Rushwa, inawezekana baadhi ya sehemu unafika pale, unapewa 10,000 au unapewa bia mbili au tatu unaondoka zako, kitu ambacho hakina maana, sasa k**a wewe ni Mtaalamu wa Afya simama kwenye maadili yako" alisema Prof. Mchembe.

Hata hivyo, Prof. Mchembe amewaagiza Maafisa afya mazingira nchini, kusimamia udhibiti wa takataka zinazotokana na utoaji wa huduma za afya ili kuendelea kuikinga jamii dhidi ya maambukizi yatokanayo na taka hizo.

Naye Kaimu Mganga Mkuu wa Serikali, ambae pia ni Mkurugenzi wa huduma za Kinga Wizara ya Afya, Maendel

12/16/2020

WIZARA YA AFYA YAJIPANGA KUZINDUA MPANGO WA KITAIFA WA AFYA NA USAFI WA MAZINGIRA

NA DANSON KAIJAGE,DODOMA

WIZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto amepanga kuzindua Mpango Mkakati wa Kitaifa wa Afya na Usafi wa Mazingira kwa mwaka (2021-25) unaolenga kupunguza mlipuko wa magonjwa yanayotokana uchafuzi wa mazingira hasa kipindupindu na kuhara.
Mkakati huo unalenga kuboresha afya ya wananchi juu ya maswala ya afya ya mazingira na usafi wa mazingira kwa kuunda jukwaa la kuruhusu Wizara, taasisi na wadau kushiriki juhudi na kutoa utaalam katika kutatua vizuizi kadhaa vinavyosababisha uchafuzi wa mazingila na kutafuta ufumbuzi wa kuboresha hali ya afya ya mazingira na usafi wa mazingira nchini Tanzania.
Taasisi ambazo zinalengwa kushiriki katika mkakati huo wa kutoa elimu ya kimkakati kwa afya na usafi wa mazingira ambazo ni Wizara za Elimu, maji, Ofisi ya Waziri Mkuu (Serikali za Mitaa na Tawala za Mikoa), Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba Tanzania (TMDA,) Shirika la Viwango Tanzania (TBS) na Wakala wa Barabara Vijijini (TARURA).
Maelezo hayo yametolewa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Prof Mabula Mchemba wakati akizungumza na Maofisa Afya na Mazingira Tanzania bara 2020 katika mkutano mkuu wa mwaka uliofanyika Jijini Dodoma unaoendelea kwa siku nne.
Katika hotuba yake ya ufunguzi, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, amesema kuwa afya ya mazingira na usafi wa mazingira ni eneo nyeti kwani inahusika na afya ya kisaikolojia, afya ya akili ya binadamu.
Kutokana na hali hiyo Prof Mchemba amewataka watumishi wote wanaotoa huduma ya afya pamoja na usafi wa mazingira kuhakikishanwanafanya kazi kwa ueledi pamoja na kueshimiana wao kwa wao pamoja na kutoa huduma sahihi kwa wateja wao.
"Kumekuwepo na changamoto kubwa ya usafi hata kwenye taasisi zetu katika ofisi nyingi za Umma,mashuleni bado kuna tatizo la usafi wa mazingira unaweza kuingia katika ofisi hata kwenye hospitali lakini utashangaa kukutana na vyoo vikiwa vichafu.

FURSA FURSA FURSAKwako wewe Mtumish wa umma na ulie ajiriwa wizarani na shirika la umma.Habari! Karibu BancABC, upate Mk...
12/10/2020

FURSA FURSA FURSA
Kwako wewe Mtumish wa umma na ulie ajiriwa wizarani na shirika la umma.

Habari! Karibu BancABC, upate Mkopo Rahisi,
1-Hakuna gharama za kuchakata Mkopo.
2-Sio lazima uwe na Account bancABC, utapata fedha kupitia account yako.
3-Mteja ana Uhuru wa kurudia Mkopo (Top up)
4-Mteja anaruhusiwa kufuta Mkopo Muda wowote
5-Tuna nunua Madeni toka Benki zingine, Loan board, Sacco's,na Taasisi za FEDHA.
Pia unachukua muda mchache mpaka kuupara.
Karibu nasi tukuhudumie.
Dodoma - Fika Uhindindi Jirani na Chef Asili au Jengo la BIMA/NIDA.
KARIBU tukuhudumie,
Ikumbukwe kuwa mkopo tunaotoa unabima kabisa na pia utakushika mkono popote utakapo pata matatizo.
Piga 0715123013 au 0656439819 kwa maelezo zaidi.

Afisa Mikopo.
SELEMANI M. MUBARAKA.

11/01/2020

Amsterdam aomba Jumuiya ya Madola kuingilia Uchaguzi Mkuu wa Tanzania

Amsterdam aomba Jumuiya ya Madola kuingilia Uchaguzi Mkuu wa Tanzania
Wakili wa aliyekuwa mgombea Urais Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CHADEMA, Tundu Lissu, Robert Amsterdam ameiandikia barua jumuiya ya madola na kuiambia kuwa kuna ubadhilifu mkubwa umefanyika katika uchaguzi wa Tanzania hivyo ameomba Jumuiya ya Madola kuingilia Uchaguzi huo.
Barua Yenyewe Ilioandikwa kwa Kizungu hii hapa:
https://www.jamiiforums.com/attachments/2020-10-29-commonwealth-complaint-pdf.1615734/

JEREMY WISTEN AJIUA KWA MAWAZONA  SELEMANIMUBARAKAKINDA wa Man City, Jeremy Wisten (17), inadaiwa kuwa amejiua kutokana ...
10/28/2020

JEREMY WISTEN AJIUA KWA MAWAZO

NA SELEMANIMUBARAKA

KINDA wa Man City, Jeremy Wisten (17), inadaiwa kuwa amejiua kutokana na msongo wa mawazo baada ya kuachwa na klabu hiyo.
Jeremy ni mzaliwa wa Malawi ambaye alihamia England na familia yake wakati akiwa bado mdogo na baadaye kuanza maisha yake soka akiwa na Juniors FC na 2014 akajiunga na De la Salle FC.
Mwaka 2016 alisajiliwa na Man City katika kikosi cha U-13 na kuanza safari yake ya soka ambapo hakupata nafasi timu ya wakubwa, hata hivyo, vyanzo vya baadhi vinaripoti kuwa mchezaji huyo kajiua huku wengine wakiripoti kifo chake pasipo kutaja sababu.

10/27/2020

Uchaguzi Tanzania 2020: Kiongozi wa chama cha ACT Wazalendo Maalim Seif ak**atwa Zanzibar

Mwenyekiti wa chama cha ACT Wazalendo Maalim Seif amek**atwa kisiwani Zanzibar.
Maalim Seif alik**atwa na maafisa wa polisi mapema leo katika kituo cha kupigia kura cha Garagara hatua ambayo imeshutumiwa vikali na viongozi wa upinzani.
Taarifa zinaarifu kwamba barabara inayoelekea katika kituo hicho imefungwa huku vitoa machozi vikirushwa.
Hapo jana Tume ya uchaguzi kisiwani Zanzibar ilisema kwamba ni maafisa wa polisi na wale wa kusimamia uchaguzi watatakaoruhusiwa kupiga kura katika siku ya kwanza ya uchaguzi.
Ilisema kwamba hatua hiyo inalenga kuwapatia fursa maafisa hao ambao wamekuwa wakikumbwa na changamoto ya kushiriki katika uchaguzi huo.

10/26/2020

WAGOMBEA BK "V",BK MJINI WAFUNGA KAMPEINI RASM

NA MWANDISHI WETU

WAGOMBEA ubunge jimbo la Bukoba Vijini Conchesta Rwamlaza na Cheifu Kalumuna wote Chadema wamefunga kampeini zao za ubunge kwa kishindo.
Wakifunga mikutano ya Kampeini wagombea hao wamesema kuwa wanawashukuru wanachi kwa kuweza kuhudhuria mikutano yao na kusikiliza Sera zao kwa umakini mkubwa.
Licha ya kuwasgukuru wanachi ambao ni wapiga kura wamevishukuru vyambo vya ulinzi na usalama kwa kulinda mikutano yao ya kampeini na kusababisha mikutano yao kuwa salama.
"Tunawashukuru wananchi kwa kuwa waaminifu katika kufika katika mikutano yetu na mmeweza kutusikiliza vyema na hamkuweza kusababisha fujo bali mlisikiliza sera.
" Lakini pia tuchukue nafasi hii kuvishukuru vyombo vya ulinzi na usalama kwa kuweza kusimamia vyema mikutano yetu ya kampeini bila kuwa na mikwaluzano yoyote"amesema Conchesta.
Pamoja na mambo mengine Conchesta amewaomba wapiga kura kujitokeza kwa wingi kupiga kura na wasiwe na wasiwasi kwani katika uchaguzi huu mtu ambaye atashinda kwa halali lazima atatangazwa.
Conchesta amefunga kampeini zake katika kata ya Kemondo Jimbo la Bukoba vijijini huku akisisitiza vipaumbele vyake sita ambavyo ni miundombinu ya barabara, Afya,kilimo,uvuvi,Maji,Elimu huku akiomba kupewa ridhaa ya kuwa mbunge wa jimbo hilo kwa faida ya maendeleo ya wana Bukoba Vijijini.
Naye Cheifu Kalumuna mgombea ubunge Jimbo la Bukoba Mjini Chadema amefunga kampeini zake katika kata ya Kashai huku maelfu ya wananchi wakiwa wamefurika.
Chief Kalumuna ambaye amewahi kuwa Meya wa halmashauri ya Manispaa ya Bukoba mjini amewataka wapiga kura kuhakikisha wanajitokeza kupiga kura na kulinda kura zao.
Mwisho.

MATUKIO KATIKA PICHA Leo October 26, 2020 Mgombea Ubunge wa Jimbo la Mbeya Mjini kwa tiketi ya CCM Dr. Tulia Ackson ameh...
10/26/2020

MATUKIO KATIKA PICHA

Leo October 26, 2020 Mgombea Ubunge wa Jimbo la Mbeya Mjini kwa tiketi ya CCM Dr. Tulia Ackson amehitimisha ziara za kampeni zake za kata kwa kata kuelekea Uchaguzi mkuu wa October 28, 2020 katika Viwanja vya Airport ya zamani Mkoani Mbeya huku akisindikizwa na msanii wa kizazi kipya Rayvanny.

10/25/2020

GARI YA RWEIKIZA YAPOPOLEWA NA MAWE KYAITOKE

NA MWANDISHI WETU

GARI ya Mgombea ubunge kupitia tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Jimbo la Bukoba Jason Rweikiza imevamiwa na kupopolewa mawe na vijana wa Kata ya Kyaitoke ndani ya jimbo la Bukoba vijijini.
Taarifa kutoka katani hapo zinaeleza kuwa majira ya saa mbili usiku Rweikiza pamoja na Dereva wake walikuwa wakiendelea na harakati za kuonana na wapiga kura kwa ajili ya uchaguzi unaotarajiwa kufanyika 28 Oktoba Mwaka huu.
Chanzo cha kuhaminika kutoka katika eneo hilo kinasema kuwa shambulio lililomsibu mgombea ubunge wa CCM pamoja na Dereva wake,inasemekana walikuwa wamewakusanya baadhi ya watu kwa ajili ya kuwapatia chochote k**a sehemu ya kuwashawishi ili waweze kumpigia kura.
"Ilikuwa saa mbili usiku kuamkia leo(Jumapili) tuliona lilionekana gari la mheshimiwa Rweikiza likiwa limezingirwa na watu ambao inasadikiwa walikuwa wameahidiwa kupewa rushwa ili waweze kufanikisha kumchagua.
" Lakini wakati zoezi likiendelea lilitokea kundi la watu ambao walikuwa wakirusha mawe na kusababisha gari la mheshimiwa kuvunjwa vioo na baadeye Rweikiza na Dereva wake kukimbia"kimesema chanzo cha habari hizi kwa masharti ya kutotajwa majina.
Naye Juliasi Kashangaki amesema kuwa wakati tukio linatokea alikuwa anaelekea katika hospitali teule ya Izimbya kwa ajili ya kumwangalia mgonjwa wake.
"Kwa kuwa tayari kuligua kumeisha ingia giza na ilikuwa saa mbili usiku niliona watu wakikimbizana huku mawe yakirushwa kwenye gari na baadaye gari kukimbizwa nilipouliza wakasema Rweikiza alikuwa akigawa hela" amesema Kashangaki.
Alipotafutwa katibu wa mgombea Ubunge kwa Tiketi ya CCM,Jasson Lwankomezi alithibitisha kutokea kwa rabisha hiyo na kusema kuwa gari halikuharibika k**a inavyosemekana.
"Nikweli jambo hilo limetokea lakini gari halikupigwa kwa kiwango cha kuharibika bali ni sehemu ndogo tu ya uharibifu uliotokea.
" Katika mambo ya siasa hilo ni jambo la kawaida na si kweli kuwa alikuwa anagawa hela kwa wapiga kura kwani tunajua ...

10/25/2020

KAMPENI ZA CCM KUFUNGWA SAA TISA ALASIRI, MGOMBEA URAIS WA CCM KUHUTUBIA WANANCHI SAA KUMI ALASIRI

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt. Bashiru Ally Kakurwa, ametoa maelekezo kwa wanaCCM wote nchini, kufunga kampeni saa tisa alasiri, ili kutoa muda kwa wanachama na wananchi wote kumsikiliza Mgombea Urais wa CCM Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli kuanzia saa kumi alasiri tarehe 27 Oktoba, 2020 atakapokuwa akizungumza kupitia vyombo vya habari katika Ukumbi wa Jakaya Kikwete Convetion Center Jijini Dodoma.

Ameyasema hayo leo tarehe 24 Oktoba, 2020 wilayani Babati katika kikao cha mawakala wa CCM na viongozi mbalimbali wa Mashina, matawi, Kata, wilaya na mkoa.

"Kamati zote za ushindi wanaelekezwa na Mwenyekiti na Mgombea wetu wa Urais waendelee na kampeni bila kuchoka mpaka saa tisa alasiri tarehe 27 Oktoba. Saa kumi alasiri Mwenyekiti, Rais wetu na Mgombea wetu Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli atahutubia wanachama na wananchi wote akiwa Dodoma katika ukumbi wa Jakaya Kikwete, na hotuba hiyo yenye ujumbe mahususi ataitoa kupitia vyombo vyoote vya habari na itakuwa mubashara"

Aidha Katibu Mkuu, ametoa maelekezo kuwa wagombea wote wakiwemo waliopita bila kupingwa ngazi za Udiwani na Ubunge, kufanya mikutano mfululizo kuanzia sasa na siku ya tarehe 27 kuanzia saa mbili asubuhi mpaka saa tisa alasiri, wagombea wote wakiwemo waliopita bila kupingwa ni lazima wawe wamefanya mikutano ya kuhitimisha kampeni kabla ya kuanza kumsikiliza Mgombea wa Urais saa kumi alasiri.

Katika hatua nyingine, Katibu Mkuu ametumia fursa hiyo, kutoa elimu kwa wapiga kura ambapo amewataka wanachama wote siku ya tarehe 28 kutokuvaa sare za Chama, na kwa wale waliopoteza shahada zao za kupigia kura wanaweza kutumia Vitambulisho vya NIDA, leseni ya udereva na hati ya kusafiria.

Wakati huo huo, Katibu Mkuu amewahakikishia wanachama na wananchi wote, kuwepo na usalama wa kutosha siku ya kupiga kura na kutangazwa matokeo, hivyo amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi kupiga kura

10/24/2020

NA DANSON KAIJAGE,BUKOBA

MGOMBEA ubunge jimbo la Bukoba Vijijini Conchesta Rwamlaza (Chadema) amekemea vikali vitendo vya wanasiasa ambao wanatumia muda mwingi kutukana na kudhalilisha wagombea wengine wa k**e.

Akihutubia maelfu ya wapigakura wa kitongoji cha Bituntu Kijiji Kaironge Kata ya Rukoma Jimbo la Bukoba vijijini.

Rwamlaza amesema kwa sasa Mgombea mwenzake kutoka CCM ameshindwa kuwasaidia wapiga kura wa kata ya Rukoma katika jimbo la Bukoba vijijini licha ya kuwa mbunge wa jimbo kwa miaka 10.

"Mimi ni mgombea ubunge kutoka Chadema na tupo wagombea wanne na mimi ni mwanamke pekee lakini jambo la kushangaza wagombea hao badala ya kutoa agenda kwa wananchi wanakuwa na matusi.

" Matusi kwa wagombea hao kwangu ni unyanyasaji wa kijinsia na kwa kutukana kunawafanya hata akina dada ambao wanaumri mdogo wataogopa kugombea nafasi mbalimbali ya uongozi"amesema Conchesta.

Pamoja na mambo mengine Conchesta amesema Rweikiza ameaza kuunda magenge ya kuvuruga mikutano yake kutokana na kuwa na hofu ya kishindwa kutoa hoja ya utatuzi wa matatizo mbalimbali yanayowakabili wananchi.

"Rweikiza ameanzisha magenge ya wahuni ili kuvuruga mikutano yangu,mbaya zaidi kawapanga vijana wa kufanya kila kata ambapo naenda kufanya mkutano na taarifa ambazo tumezipata ameisha toa fedha kiasi cha milioni moja na ametoa kianzio sh.laki tano.

" Natuma ujumbe kwa Rweikiza sitotaka kufanya fujo wala kupigana ila hakitaka kufanya fujo mimi nitafanya fujo zaidi siwezi kushindwa kupambana na Rweikiza na naomba awe mstaarabu" amesema Conchesta.

Mwisho.

Vichwa vya habari  vya magazeti yalio toka LeoTarehe 21
10/21/2020

Vichwa vya habari vya magazeti yalio toka Leo
Tarehe 21

TAARUKI YATANDA BAADA YA KUBADILISHA VITUO VYA KUAPISHIA MAWAKALANA DANSON KAIJAGE, BUKOBA PAMOJA na Barua ya kiapo cha ...
10/20/2020

TAARUKI YATANDA BAADA YA KUBADILISHA VITUO VYA KUAPISHIA MAWAKALA

NA DANSON KAIJAGE, BUKOBA

PAMOJA na Barua ya kiapo cha Kutunza Siri cha mawakala iliyoandikwa Oktoba 11 mwaka huu kinachowataka mawakala kuapishwa tarehe 21/10/2020 saa nne asubuhi katika kata husika hali imebadilika ghafla na kuwataka mawakala kuapishiwa katika makao makuu ya tarafa.

Taarifa ambazo mawakala wamezipata mida ya saa kumi jioni leo 20/10/2020 zinawataka mawakala kuapishwa kwenye makao yao ya tarafa tofauti na maelekezo, iliyoandikwa kwa niaba ya msimamizi wa uchaguzi Dk.Themistocles Kaijage na kusambazwa katika halmashauri zote za uchaguzi.

Hali hiyo ya kubadilisha vituo vya kuapishwa kwa mawakala vimezua taaruki katika Jimbo la Bukoba Vijijini ambapo maafisa watendaji wa kata ambao ndio wanatakiwa kuwaapisha mawakala wa uchaguzi kutoa maelekezo ambayo yanapingana na maelekezo ya tume ya Uchaguzi NEC.

Maelekezo ya barua kwa mawakala katika Msimamizi wa Uchaguzi Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba Vijijini kipengere namba 4 kinasema"Kwa kuzingatia Jiografia ya jimbo letu la uchaguzi Msimamizi wa Uchaguzi ameelekezwa kuwa wagombea wote udiwani waape mbele ya Msimamizi Msaidizi Kata pamoja na mawakala wao katika maeneo yao ya kata tarehe 21/10/2020, saa nne Kamili Asubuhi.

"Wagombe ubunge pamoja na wakala wa kujumuisha kura za jimbo wanatakiwa kula kiapo cha kutunza siri mbele ya Msimamizi wa uchaguzi ofisini kwake Mubembe Kemondo tarehe 21/10/2020 saa tano Asubuhi" barua inaeleza.

Kwa maelezo hayo taarifa zinazotolewa na maofisa watendaji kata kuwa mawakala wanatakiwa kuapishwa katika makao makuu ya tarafa zinapingana kabisa na barua ya Msimamizi wa Uchaguzi.

Mwisho.

Address

Brooklyn, NY

Telephone

+255656439819

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when The slate news Updates posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to The slate news Updates:

Share