01/18/2026
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, M***a Azzan Zungu ametangaza kifo cha mbunge wa Viti maalum Halima Idd Nassor kilichotokea hii leo Januari 18, 2026 katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) alipokuwa akipatiwa matibabu.
"Kwa masikitiko makubwa, natangaza kifo cha Mbunge wa Viti Mheshimiwa Halima Idd Nassoro kilichotokea leo 18 Januari, 2026 Jijini Dar es Salaam.
Jamaa na marafiki, Mwenyezi Mungu awape katika kipindi hiki kigumu," "Ofisi ya Bunge kwa kushirikiana na familia ya Marehemu inaratibu mipango ya mazishi na taarifa zaidi zitaendelea kutolewa. "Inna lillahi wa inna ilayhi rajl'un"
Amina."
Imeeleza taarifa rasmi kutoka Ofisi ya Bunge.