12/14/2025
Ibada ya Jumapili :
Somo: Madhara ya kuzoea madhabahu ya Mungu .
Key points: Andaa Safari yako kwa ajili ya kukutana na Mungu .
Je mahali ambapo Mungu amekuweka uwepo katika kanisa una simama katika utakatifu?
Mambo ya walawi 10:1-2
Unapokuwa unazoea madhabahu ya Mungu na kuona kawaida ni rahisi kufa kiroho , Roho ya mazoea Inauwa taratibu inasababisha Mungu kuondoka taratibu ndani yako .
Tunatakiwa kuwa na unyeyekevu , utii na kufuata maelekezo .
Kuzoea madhabahu ni kuipuuza , kufanya ya kawaida na kukosa hofu ya Mungu.
Angalia siku moja uliahidi nini katika madhabahu ya bwana , je maneno yako uliyatendea kazi . Tusidanganye madhabahu.
Kuna watu wa Mungu wamekufa kwa kuichafua na kuzoea madhabahu.
Madhabahu inauwa , inafedhehesha , inapiga ukiitumia vibaya .
Kuna Munganiko mkubwa Kati ya madhabahu na sadaka . K**a hutoi sadaka na fungu la kumi haujajiambatanisha!
Kuzoea madhabahu huleta kiburi!
Kuzoea madhabahu kunaleta kupungukiwa na nguvu za Mungu.
Kuzoea madhabahu kunaleta laana za maangamizi.
(Biblia inasema waliozoea madhabahu walikufa pale pale)
Preacher : Pastor Mariam PKE