Western Nyota 87.8 Busia Fm

  • Home
  • Western Nyota 87.8 Busia Fm

Western Nyota 87.8 Busia Fm Western Nyota Busia Fm 87.8 Hits, is a leading in local languages Ateso and luhya in western kenya
(2)

K**a njia moja wapo  ya kupunguza ukosefu wa usalama, Mungano wa Vocal Afrika umejitokeza na kuandaa mashindano ya miche...
25/08/2026

K**a njia moja wapo ya kupunguza ukosefu wa usalama, Mungano wa Vocal Afrika umejitokeza na kuandaa mashindano ya michezo almaarufu tournaments kwa vijana wa county ya Busia eneo bunge la Butuula......

Zaidi ya miaka kumi tangu kuanzishwa kwa mfumo wa ugatuzi wa serikali nchini, wakazi wa kauti ya Busia bado hawajanufaik...
23/08/2026

Zaidi ya miaka kumi tangu kuanzishwa kwa mfumo wa ugatuzi wa serikali nchini, wakazi wa kauti ya Busia bado hawajanufaika kikamilifu na matunda ya ugatuzi huo, haya ni kwa mujibu wa mwaniaji wa kiti cha useneta wa kaunti ya Busia kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka wa 2027 wakili Victor Obuli Namenya

Kulingana na wakili huyo,anasema licha ya serikali ya kitaifa kutenga mabilioni ya fedha kwa ajili ya maendeleo ya kaunti, wakazi wa Busia bado wanakabiliwa na changamoto za umaskini, huduma duni za afya pamoja na miundombinu isiyoridhisha hali ambayo anasema imeendelea kujitokeza chini ya uongozi wa gavana wa zamani Sospeter Ojaamong na gavana wa sasa Paul Otuoma.

Victor Ambaye amezungumza na wanahabari mjini busia , amepuuzilia mbali madai kwamba Busia imekuwa nyuma
kimaendeleo kwa sababu ya kuwa eneo la upinzani kisiasa akisema kaunti hiyo imekuwa na viongozi mashuhuri waliowahi kuhudumu serikalini katika nyadhifa mbalimbali, akimtaja aliyekuwa makamu wa rais Moody Awori miongoni mwao na kusema kuwa licha ya kuwepo kwa viongozi hao kutoka Busia, ukosefu wa ajira miongoni mwa vijana bado ni changamoto kubwa katika kaunti hiyo.

19/08/2026

Salamu wafuasi wangu wapya! Nina furaha kuwa nanyi! Mutai Sylvester, Patrick Juma, Isaack Ouma, Kiboko Cha Nana Ward, Amaya Royal

19/08/2026

Odilo 7s Rugby Tournament

12/08/2026

Salamu za kipekee kwa mashabiki bora wageni! Otieno Rogers

PANA HAJA YA  KUFANYIKA KWA SIASA ZA AMANI KUELEKEA KWENYE UCHAGUZI MKUU WA MWAKA WA 2027 K**A MOJAWAPO YA NJIA ZA KUIMA...
12/08/2026

PANA HAJA YA KUFANYIKA KWA SIASA ZA AMANI KUELEKEA KWENYE UCHAGUZI MKUU WA MWAKA WA 2027 K**A MOJAWAPO YA NJIA ZA KUIMARISHA SEKTA YA BODABODA KATIKA KAUNTI YA BUSIA .

NI WITO WA MWENYEKITI WA KITAIFA WA WANABODABODA KEVIN MBADI AMBAYE AMESEMA KUWA SIASA ZA VURUGU INA ATHARI KUBWA KATIKA SEKTA HIYO YA BODABODA KWANI NI NJIA YA MAPATO KWA WENGI HUKU PIA AKIWATAKA VIJANA KUTOKUBALI KUTUMIWA NA WANASIASA KUZUA GHASIA KATIKA MIKUTANO YA KISIASA.

WAKATI UO HUO, MBADI AMESIFIA RUWAZA YA MWAKA WA 2060 ILIYOZINDULIWA NA RAIS WILLIAM RUTO AKISEMA INALENGA KUIMARISHA UCHUMI WA TAIFA AKIWAKASHIFU WANASIASA WANAOPINGA RUWAZA HIYO NA KUWATAJA K**A ADUI WA MAENDELEO YA TAIFA .

Uteuzi wa Kenya kuikaribisha Kituo cha Ubora cha Afrika cha Mtaji wa Watu na Maendeleo ya Kijamii na Kitaasisi unaashiri...
11/08/2026

Uteuzi wa Kenya kuikaribisha Kituo cha Ubora cha Afrika cha Mtaji wa Watu na Maendeleo ya Kijamii na Kitaasisi unaashiria hatua muhimu katika juhudi za nchi za kukuza maendeleo yanayoendeshwa na maarifa na kuimarisha uwezo wa Afrika wa kutoa mabadiliko endelevu ya kijamii na kiuchumi, sambamba na Ajenda ya Kenya ya Mabadiliko ya Kiuchumi ya bottom up.

Katibu mkuu kwenye wizara ya mipangilio ya kiuchumi nchini Dr Boniface makokha,ameweza kupokea Mkurugenzi Mtendaji wa Bara wa AUDA-NEPAD, Bi. Nardos Bekele Thomas, ambaye anaongoza ujumbe kutoka Sekretarieti ya Bara ya AUDA-NEPAD katika ziara yake nchini Kenya.

Kwa niaba ya Serikali ya Kenya, katibu huyo ameshukuru AUDA-NEPAD kwa kuchagua Kenya kuikaribisha Kituo cha Ubora, ambacho kimekuja katika wakati muhimu huku nchi ikiandaa kuanza awamu inayofuata ya mipango yake ya muda mrefu ya maendeleo.

Kituo hiki kitachukua jukumu kubwa katika kuimarisha mtaji wa watu, kujenga uwezo wa kitaasisi na kukuza uzalishaji na utumizi wa maarifa ili kuunga mkono maendeleo ya Afrika.

Waliokuwepo katika mkutano huo walikuwa Balozi Dkt. Samori Okwiya, Mkurugenzi Mtendaji wa Sekretarieti ya NEPAD/APRM Kenya, Dkt. Masini Ichwara, Mkurugenzi Mkuu wa Mipango ya Kiuchumi pamoja na maafisa wengine waandamizi kutoka Sekretarieti ya Bara ya AUDA-NEPAD na Serikali ya Kenya.

08/08/2026

Kwa Vivian Afuma – Nimetambuliwa sasa hivi k**a mmoja wa mashabiki wake bora!

Linda mwananchi western tour, Busia County # western nyota Busia #87.8 FM
07/08/2026

Linda mwananchi western tour, Busia County
# western nyota Busia
#87.8 FM

Address

Bulanda Checkpoint

P.OBOX450BUSIA

Telephone

+254723784848

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Western Nyota 87.8 Busia Fm posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Shortcuts

  • Want your business to be the top-listed Media Company?

Share

l="false"> Add listing
  • Login
  • Subscribe

    We will notify you when anything happens in Columbus.