
15/07/2025
Nasikia kuongea na mtu mmoja siku ya leo, sijui unapitia jaribu gani, sijui unapita kwenye changamoto gani, sijui kiwango cha maumivu ulichonacho moyoni
Bwana amenipa Neno kwa ajili yako siku ya leo kwamba hakuna hali ambayo huwa inadumu katika maisha, hakuna uadui ambao huwa unadumu kila chenye mwanzo huwa kina mwisho
Nimetumwa kukwambia acha kujipa stress juu ya hali unayoipitia amini tu kwamba hata hilo utalishinda tu kwasababu unae mtetezi ambae ni Yesu Kristo atakutetea na kukushindia
Biblia inasema
Zaburi 23:4
Naam, nijapopita kati ya bonde la uvuli wa mauti
Sitaogopa mabaya
Kwa maana Wewe upo pamoja nami,
Gongo lako na fimbo yako vyanifariji.
Kila mwanadamu kuna wakati ambao lazima anapenda hapendi atapita kwenye bonde la uvuli wa mauti. Mahali ambapo tumaini linapotea, giza linatanda kila mahali
Lakini cha kutia moyo ni hiki kwamba kwenye bonde la uvuli wa mauti sio mahali tunakaa ni mahali tunapita. Nimetumwa kukwambia unapita tu wala hutakaa kwenye hiyo hali
Lakini pia pia Biblia inasema sitaogopa mabaya kwa maana Bwana yupo pamoja na wewe . Hata iweje, hata vita yako iwe kubwa kiasi gani, hata pito lako liwe kubwa kiasi gani hakikisha hauogopi
Sio kwamba maumivu hayatakuwepo yatakuwepo ila hakikisha hauogopi kwa maana Bwana yupo pamoja na wewe, Gongo lake na fimbo yake vitakufariji