07/09/2025
بِسْمِ اللهِ الرَّحْمَنِ الرَّحِيمِ
*KUPATWA KWA JUA NA MWEZI*
*Hukmu, Sayansi na Mafunzo.*
(*The Eclipse of the Sun and Moon: Rulings, Science & Reflections*)
*الكُسوف والخُسوف: الأحكام والعِلم والعِبَر*
---
*1. MAAANA YA KUPATWA* :
- *كُسُوف الشمس*: Ni Hali ambapo mwezi unazuia mwanga wa jua kwa muda.
- *خُسُوف القمر*:
Ni Hali ambapo mwezi hauonekani kwa sababu ya kuingia kwenye kivuli cha dunia.
---
*2. SABABU YA KISAYANSI*
- Kupatwa kwa jua (Solar Eclipse) hutokea mwezi unapopita kati ya dunia na jua.
- Kupatwa kwa mwezi (Lunar Eclipse) hutokea dunia inapopita kati ya jua na mwezi.
Haya yote ni mzunguko wa kiasili uliowekwa na Allah, si tukio la kishetani wala la bahati mbaya.
---
*3. DALILI ZA KISHARIA*
*QUR’ĀN:*
وَمَا نُرْسِلُ بِالْآيَاتِ إِلَّا تَخْوِيفًا
*“Wala hatutumi Ishara isipokuwa kwa ajili ya kuwatia watu khofu.”*
(Sūrat Al-Isrā: 59)
*وَمِنْ آيَاتِهِ ٱلَّيْلُ وَٱلنَّهَارُ وَٱلشَّمْسُ وَٱلْقَمَرُ ۚ لَا تَسْجُدُوا۟ لِلشَّمْسِ وَلَا لِلْقَمَرِ وَٱسْجُدُوا۟ لِلَّهِ ٱلَّذِى خَلَقَهُنَّ إِن كُنتُمْ إِيَّاهُ تَعْبُدُونَ*
(فصلت: 37)
*Maana:* *Na miongoni mwa ishara zake ni usiku, mchana, jua na mwezi. Msisujudie jua wala mwezi bali msujudieni Allah aliyeviumba k**a kweli mnamuabudu.*
(Surah Fuswilat)
*HADĪTH SAHIHI:*
إِنَّ الشَّمْسَ وَالْقَمَرَ آيَتَانِ مِنْ آيَاتِ اللَّهِ، لَا يَنْخَسِفَانِ لِمَوْتِ أَحَدٍ وَلَا لِحَيَاتِهِ، فَإِذَا رَأَيْتُمُوهُمَا فَصَلُّوا وَادْعُوا حَتَّى يَنْجَلِيَ مَا بِكُمْ. مسلم
*“Hakika jua na mwezi ni miongoni mwa alama za Allah. Havipatwi kwa sababu ya kufa kwa mtu au kuzaliwa kwake. Basi mnapoviona vikipatwa, salini, ombeni, hadi yakae sawa.”*
(Imam Muslim)
---
*4. HUKUMU YA SWALA YA KUPATWA*:
- Ni *Sunnah Mu’akkadah*.
- Haiswaliwi kwa adhana wala iqaamah.
- Inaswaliwa kwa jamaa au mtu mmoja.
- Raka’a mbili tu, kila raka’a ina kusoma mara mbili na rukuu mbili.
- Muda wake huendelea hadi kupatwa kumalizike.
*NAMNA YA KUSWALI*:
- Raka’a mbili
- Kila raka’a ina rukuu mbili (rukuu ya kwanza ndefu, ya pili fupi)
- Kila raka’a ina kusoma mara mbili (baada ya qiyām).
*5. TOFAUTI KATI YA SWALA YA KUSUUF NA KHUSUUF* :
- Kusūf (kupatwa kwa jua) huswaliwa mchana kwa *sauti ya siri* (sirriyah), na kuna *khutba* baada ya swala.
- Khusūf (kupatwa kwa mwezi) huswaliwa usiku kwa *sauti ya juu* (jahr), na *hakuna khutba*.
---
*6. NANI HASWALI, NA AFANYE NINI?*:
- Mwanamke aliye hedhi au nifās: Hataswali, lakini atajishughulisha na *dhikr, istighfār, na dua*.
- Wagonjwa au walio safarini: Waswali kwa hali waliyo nayo– kwa kukaa au kulala.
- Watoto: Inafaa kuwahusisha kwa kujifunza na mazoezi ya dini.
---
*7. MAMBO YA KUFANYA WAKATI WA KUPATWA*:
Mtume صلى الله عليه وسلم alisema:
فَافْزَعُوا إِلَى الصَّلَاةِ
*"Kimbilieni swala!"*
(Sahih Muslim)
Mambo ya kuamrishwa:
- Swala
- Dua na istighfār
- Kutoa sadaka
- Kuhimiza toba na kurudi kwa Allah
---
*8. MAFUNZO TUNAYO PATA*
- Kupatwa ni onyo na ukumbusho wa *siku ya Qiyāmah*.
- Hufundisha kuwa uweza wote ni wa *Allāh سبحانه وتعالى*.
- Sayansi haipingani na dini, bali huthibitisha *ukuu wa Muumba*.
- Muumini wa kweli hubadilika na kuongeza ibada kwa kuona aya k**a hizi.
---
*9. HUKUMU KWA WALIO DHARURA*
- Mwanamke aliye kwenye udhuru halazimiki kuswali, lakini *asikose dua na kumkumbuka Allah*.
- Ikiwa kupatwa kutatokea na hawezi kushiriki kwa jamaa, *anaruhusiwa kuswali peke yake*.
- Aliyeshindwa hata kuswali, anaweza *kumuomba Allah kwa moyo, machozi, na dua.*
---
*10. HITIMISHO*
Kupatwa kwa jua au mwezi ni aya na alama kubwa ya uwepo wa Allah. Tusichukulie kwa mzaha wala k**a tukio la kawaida. Bali tuswali, tuombe rehema ya Allah, turejee kwa toba, na tusahihishe hali zetu kwa ajili ya Akhera.
Ameandaa
📚🖋️ *Sheikh*
*Abdurrahmani M***a*
(Allah amlipe kheri)
_______