
18/10/2022
WATANI KAZI WANAYO,.,.,.aibu nyingne inakujaππ€£π€ππ€£ππ€.
ππππππππππ
Ratiba ya Kombe la Shirikisho barani Afrika imetangazwa ambapo mabingwa wa Ligi Kuu ya NBC kutoka Tanzania, Yanga wamepangwa kucheza na timu ya Club Africain ya nchini Tunisia.
Yanga wamepangwa na klabu hiyo baada ya kutolewa na Klabu ya Al Hilal ya Sudan kwa jumla ya mabao 2-1, wakitoa suluhu ya 1-1 katika mchezo wa kwanza uliochezwa katika Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam na kupoteza kwa bao 1-0 katika maechi ya marudiano iliyochezwa jijini Kharthoum.
Club Africain inakutana na Yanga, ikiwa na rekodi ya kuitoa Klabu ya Kipanga ya visiwani Zanzibar kwa jumla ya mabao 7-0, wakitoka suluhu katika mchezo wa kwanza uliochezwa nchini Tanzania na kuifunga 7-0 katika mchezo wa marudiano uliopigwa nchini Tunisia.