Camp Nou News Tanzania

Camp Nou News Tanzania Hapa ni mahala pekee utakapopata habari zote zinazoihusu klabu ya FC Barcelona 🔵🔴

K**a nilivyoripoti mchana, Thierry Henry 🇫🇷 alikuwepo leo uwanjani kuishuhudia El Classico ambapo Real Madrid wamepasuka...
11/05/2025

K**a nilivyoripoti mchana, Thierry Henry 🇫🇷 alikuwepo leo uwanjani kuishuhudia El Classico ambapo Real Madrid wamepasuka mechi ya nne mfululizo msimu huu mbele ya FC.

Wawili hao wakibadilishana jezi zao baada ya mechi kumalizika.

Kylian Mbappe na Robert Lewandowsk ndio wafungaji wanaokimbizana kuwania kiatu cha ufungaji bora pale Laliga.Mbappe amea...
11/05/2025

Kylian Mbappe na Robert Lewandowsk ndio wafungaji wanaokimbizana kuwania kiatu cha ufungaji bora pale Laliga.

Mbappe ameanza kwenye kikosi cha kwanza huku Lewandowsk akianzia benchi hii leo.

Officially, kikosi cha kwanza cha FC Barcelona kitakachoanza leo hii dhidi ya Real Madrid.   🏟️ Estadio Olympic Lluis   ...
11/05/2025

Officially, kikosi cha kwanza cha FC Barcelona kitakachoanza leo hii dhidi ya Real Madrid.

🏟️ Estadio Olympic Lluis

⏰ 17:15 EAT

Head to head ya Real Madrid vs FC Barcelona.Barcelona wamebakisha mechi mbili pekee ili kuwa sawa na Real Madrid kwenye ...
11/05/2025

Head to head ya Real Madrid vs FC Barcelona.

Barcelona wamebakisha mechi mbili pekee ili kuwa sawa na Real Madrid kwenye mechi za ushindi katika historia baina yao wawili.

Kwa mujibu wa Victor Navarro ni kwamba kocha wa zamani wa klabu ya FC Barcelona ambaye kwa sasa anakinoa kikosi cha PSG ...
11/05/2025

Kwa mujibu wa Victor Navarro ni kwamba kocha wa zamani wa klabu ya FC Barcelona ambaye kwa sasa anakinoa kikosi cha PSG Luis Enrique, leo hii atakuwepo uwanjani Estadio Olympic Lluis kuishuhudia mechi ya El Classico.

Pia awali kocha huyo pia alitoa utabiri wake kuwa leo FC Barcelona ni rahisi kushinda goli 3-0 😅

Dimba la Estadio Olympic Lluis liko tayari kwa mpambano wa El Classico 🔥.Karibuni Los Blancos kwenye uwanja wa machinjio...
11/05/2025

Dimba la Estadio Olympic Lluis liko tayari kwa mpambano wa El Classico 🔥.

Karibuni Los Blancos kwenye uwanja wa machinjio🤘

Baada ya kuibuka na ushindi wa goli 9-0 Leo hii dhidi ya Real Betis (W), klabu ya FC Barcelona (W) wametwaa ubingwa wa l...
11/05/2025

Baada ya kuibuka na ushindi wa goli 9-0 Leo hii dhidi ya Real Betis (W), klabu ya FC Barcelona (W) wametwaa ubingwa wa laliga upande wa kina dada ikiwa ni mara ya sita (6) mfululizo.

Oya kwani hamuogopi🤩

Msimu huu tunaukamilisha kwa kushubudia mechi 4 za El Classico. Tayari mechi 3 zimeisha na Real Madrid kapasuka zote. Le...
11/05/2025

Msimu huu tunaukamilisha kwa kushubudia mechi 4 za El Classico. Tayari mechi 3 zimeisha na Real Madrid kapasuka zote. Leo ni El Classico ya 4 na ya mwisho kwa msimu huu, FC Barcelona watakuwa nyumbani kuwapokea Real Madrid kuanzia majira ya saa 11:15 jioni.

Nini utabiri wako kuelekea kwenye game ya leo?

Mshambuliaji wa zamani wa klabu ya FC Barcelona Thierry Henry 🇫🇷 leo hii atakuwepo uwanjani Estadio Olympic Lluis wakati...
11/05/2025

Mshambuliaji wa zamani wa klabu ya FC Barcelona Thierry Henry 🇫🇷 leo hii atakuwepo uwanjani Estadio Olympic Lluis wakati FC Barcelona watakuwa wakiwaalika Real Madrid kwenye mchezo wa ligi kuu nchini Spain.

Henry amemuomba Lamine Yamal jezi yake baada ya mechi kumalizika.

"Utabiri wangu leo kuelekea kwenye mechi ya El Classico? Ni rahisi kwa FC Barcelona kushinda 3-0. 😂"            🎙️ Luis ...
11/05/2025

"Utabiri wangu leo kuelekea kwenye mechi ya El Classico? Ni rahisi kwa FC Barcelona kushinda 3-0. 😂"

🎙️ Luis Enrique 🇪🇦

Eneo la kiungo la klabu ya FC Barcelona imesheheni vipaji haswa ambapo Hans Flick hana wasiwasi nalo. Anayetoka na anaye...
11/05/2025

Eneo la kiungo la klabu ya FC Barcelona imesheheni vipaji haswa ambapo Hans Flick hana wasiwasi nalo. Anayetoka na anayeingia wote wanakupa ubora wa daraja la juu.

Kuumia kwa Marc Cassado kumefanya wengi tuuone ubora wa Fermin Lopez japo huwa anapishana na Dani Olmo uwanjani. Atalinda mali mguuni, atatengeneza nafasi na atakimbia uwanjani kwa nguvu na nishati ileile.

Nafurahi sana kumuangalia Fermin Lopez akiwa uwanjani na leo ni siku yake kuzaliwa na ndio kwanza ana Miaka 22 tu.

Happy birthday Fermin Lopez 🧁

Barcelona wanakabiliwa na kipindi kigumu cha siku 15 ambapo watacheza mechi nne muhimu dhidi ya wapinzani wao wakuu: Rea...
18/04/2025

Barcelona wanakabiliwa na kipindi kigumu cha siku 15 ambapo watacheza mechi nne muhimu dhidi ya wapinzani wao wakuu: Real Madrid na Inter Milan.

🏆 Fainali ya Copa del Rey:
Barcelona vs Real Madrid
⌛️Jumamosi, 26 Aprili 2025
🏟 Estadio de La Cartuja, Sevilla

🏆Ligi ya Mabingwa Ulaya:
Barcelona vs Inter Milan
⌛️Jumatano, 30 Aprili 2025
🏟 San Siro, Milan

Mechi ya Marudiano:
⏰️Jumanne, 6 Mei 2025
🏟Estadi Olímpic Lluís Companys

🏆La Liga – El Clásico:
Barcelona vs Real Madrid
⌛️Jumapili, 11 Mei 2025
🏟Estadi Olímpic Lluís Companys

Vipi unaiona wapi FC Barcelona kwenye mechi hizi?

Address

Mapumulo

Telephone

+255719856594

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Camp Nou News Tanzania posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share