06/02/2024
AFANDE MWAKATOBE
Sehemu ya I
Na. LD Mtunzi
“Kimbieniiiiiii! Afande mwakatobe huyo anakuja!”
Sauti hiyo ilisikika ikitoka katika jumba moja ambalo halikuwa limekamirika, mala vijana sita walitoka ndani ya pagara hilo kwa kupitia njia zisizo lasimi yaani madirishani, kisha wakatoka nje na kutokomea vichochoroni, mala sauti nzito yenye mamlaka kwa ujzo wa besi yake tena kwa kujiamini ikasikika kusema:-
“Hao wachumba tuu; akina Zuchu hao! Wangelibaki nikawapelekea motooo! Yaone komwe ka! Basi, ona! Ona na haya maaskari simuwafuate muwak**ate (wanaondoka) yaone chogo ka! Mwiko w aMwajuma”
Ilikuwa sauti kari ya mwakaotobe sauti ambayo kila iliposikika, waarifu wote walikimbia kwa kumuogopa, mji ulikuw umesafishika kiasi majabazi na wezi wote walitoweka kwani walimuogopa huyo askari aliyejulikana k**a afande Mwakatobe k**a ukoma.
Mwakatobe alijitwaria umaarufu nchi nzima kila aliyesikia jina hilo alisema kuwa afenda huyo alikuwa akipambana ela yote kupoteza utumiaji wa madawa ya kurevya na wizi mtaani.
One day Mwakatobe akiwa kituoni kwake, mala alipokea barua ya kuhamishwa kituo, na kuamriwa kuwa anatakiwa aende katika kijiji kinchoitwa Emangushi Village (kijiji cha Emanugshi) alipokea ile barua kisha kukubari agizo hilo.
Kijiji hiki kinapatikana Kusini Mashariki mwa nchi ya Tanzania, kijiji hiki hakina mchezo na maaskari viherehere wa Amani, askari akijifanya kuwapinga vijana wahuni wa humo kijijini, basi angeambulia kipigo huku akiwa amevaa gwanda zake.
Mwakatobe alipozipata habari za huko hofu ikaanza kumuingia, akatamani kukataa agizo hilo ila hakufanikiwa, maana ahakua na usemi wowote mbele ya amri hiyo, basi akawa amepatiwa siku ya kuwasiri katika kijiji hicho ili aweke Amani sawa, na apoteze magenge yote ya wahuni.
Hatimaye siku ya yeye kuwasiri kwenye kijiji hicho iliwadia, alipanda gari mchana juoni akafanikiwa kukanyagisha unyayo wake kwenye kijiji hicho.
Alishuka gari kisha taratibu akaelekea kwenye kituo alichopangiwa, ili aweze kukisimamia na kukom