Zamzam news.

MAREKANI YAINGIA TENA MWILINI AFRIKA KUSINI. Marekani imeanzisha mzozo mpya na Afrika Kusini na kupelekea kuzuka majibiz...
07/10/2026

MAREKANI YAINGIA TENA MWILINI AFRIKA KUSINI.

Marekani imeanzisha mzozo mpya na Afrika Kusini na kupelekea kuzuka majibizano makali ya hadharani kati ya Waziri wa Afrika Kusini wa Masuala ya Uhusiano wa Kimataifa na Ushirikiano, Ronald Lamola, na Balozi wa Marekani nchini Afrika Kusini, Brent Bozell.

Waziri huyo wa Afrika Kusini amelazimika kujibu vitendo na kauli za huko nyuma za balozi wa Marekani na kusema kuwa balozi huyo anapaswa "kuondoka jikoni" k**a amechoshwa na mazungumzo na hana imani tena na ushirikiano wa kidiplomasia na Pretoria.
Akijifanya mtu aliyedhulumiwa licha ya kwamba yeye ndiye aliyeanzisha ugomvi, balozi wa Marekani ameandika kwenye mtandao ya kijamii kwamba: "Haya tena. Tusi jingine hilo binafsi kutoka kwa Waziri Lamola dhidi ya kiongozi wa Marekani (safari hii ni dhidi yangu mimi)."
Kauli za Waziri Lamola alizozitoa baada ya kushindwa kuvumilia ubeberu wa Marekani, zilichapishwa na gazeti la "Sunday Times" la Afrika Kusini siku ya Jumapili, ikiwa ni siku chache baada ya Afrika Kusini kuwasilisha malalamiko rasmi ya dhdi ya balozi wa Marekani nchini humo ambaye anafanya uchochezi na vitendo visivyo vya kidiplomasia.
Waziri Lamola alisema ameshangazwa na kauli za Bozell zilizodokeza kuwa Washington imechoshwa na mazungumzo ya mara kwa mara na Pretoria.
Waziri Lamola pia amesema: "Huwezi kuwa na mwanadiplomasia anayesema muda wa mazungumzo umekwisha. Kazi yetu ni kuzungumza."
Pia alimlaumu vikali balozi huyo wa Marekani kwa kuingilia masuala ya ndani ya Afrika Kusini tena kwa kauli na vitendo vya hadharani.
Tarehe 29 Septemba 2026, Idara ya Uhusiano wa Kimataifa na Ushirikiano ya Afrika Kusini ilimwita Bozell kwenda kutoa maelezo kuhusu tabia zake zisizo za kidiplomasia. Hayo yalikuwa ni malalamiko rasmi ya tatu yaliyowasilishwa kwa balozi huyo wa Marekani tangu alipowasili Pretoria mwezi Februari kutokana na uchochezi wake na kuingilia masuala yasiyomuhusu.
Popote pale dola la kibeberu la Marekani linapotia mguu wake huwa hapabaki salama. Viongozi wa juu hadi wa chini wa Marekani ni maarufu kwa kutoheshimu sheria za kimataifa wala haki za kujitawala mataifa ya dunia na kujiamulia mambo yao kwa uhuru.

Kwa haya na mengine

Unakaribishwa kwenye kituo chako kupitia :
https://www.facebook.com/profile.php?id=100063744357288

Vilevile https://whatsapp.com/channel/0029Va9jawz3rZZeo2Wmdo3R

Karibuni

KIONGOZI WA SOMALIA AAPA KUZUIA UWEPO WA JESHI LA ISRAEL MJINI BERBERA Rais Hassan Sheikh Mohamud anasema kuwa Israel in...
04/10/2026

KIONGOZI WA SOMALIA AAPA KUZUIA UWEPO WA JESHI LA ISRAEL MJINI BERBERA


Rais Hassan Sheikh Mohamud anasema kuwa Israel inataka kituo cha jeshi la wanamaji na fursa ya kutumia uwanja wa ndege huko Berbera, ndani ya Somaliland, ili kukaribia Iran na mataifa ya Ghuba

Rais wa Somalia, Hassan Sheikh Mohamud, ametangaza kuwa Somalia haitakubali uwepo wa jeshi la Israel katika ardhi yake "chini ya hali yoyote ile", huku akionya kuwa Tel Aviv ina mpango wa kuanzisha kituo cha kijeshi cha majini katika eneo la Somaliland lililojitenga.

Katika mahojiano na shirika la habari la Al Jazeera yatakayorushwa hewani siku ya Jumapili, ambayo sehemu zake zimechapishwa kwenye tovuti ya shirika hilo, Mohamud alisema kuwa Israel ina mpango wa kujenga kituo cha kijeshi cha majini katika mji wa bandari wenye umuhimu wa kimkakati wa Berbera na kutumia uwanja wa ndege wa mji huo.

Alisema lengo halisi la mpango huo ni kupata ukaribu zaidi wa kijiografia na nchi za Ghuba pamoja na Iran.

Mohamud alisisitiza kuwa majaribio ya nje ya kuivuta Somalia katika migogoro mipana ya Mashariki ya Kati hayatafanikiwa, akiongeza kuwa serikali yake itashinda changamoto za kiusalama na kidiplomasia zinazotokana na hatua hizo za Israel.

Rais huyo alisisitiza kuwa hata wakazi wa eneo la Somaliland, ambalo limejitangazia uhuru, nao pia wanapinga vikali uwepo wowote wa Israel katika eneo hilo.

Mzozo wa mamlaka

Somaliland, ambayo ilitangaza uhuru wake yenyewe mwaka 1991, hatua ambayo haikutambuliwa na karibu nchi zote wanachama wa Umoja wa Mataifa, ilipata utambuzi rasmi kutoka kwa Israel mwishoni mwa mwezi wa Desemba 2025.

Umoja wa Mataifa unashikilia msimamo thabiti kwamba Somaliland ni sehemu isiyotenganishwa na Somalia.

Kiongozi wa taifa la Somalia pia alisisitiza tena kuwa Mogadishu haijawahi kuanzisha uhusiano wa kidiplomasia na Israel, akionyesha kuwa serikali yake inaichukulia Israel k**a taifa linalofanya uchokozi dhidi ya watu wa Palestina, huku ikikataa kuruhusu ardhi ya Somalia kutumika k**a kituo cha ushindani wa kijeshi wa mataifa ya Mashariki ya Kati.

Kwa haya na mengine

Unakaribishwa kwenye kituo chako kupitia :
https://www.facebook.com/profile.php?id=100063744357288

Vilevile https://whatsapp.com/channel/0029Va9jawz3rZZeo2Wmdo3R

Karibuni

WIMBI KUBWA LA HASIRA ZA WALIMWENGU DHIDI YA ISRAEL LAMLIZA NDULI WA GHAZA. Nduli wa Ghaza, waziri mkuu wa utawala wa Ki...
04/10/2026

WIMBI KUBWA LA HASIRA ZA WALIMWENGU DHIDI YA ISRAEL LAMLIZA NDULI WA GHAZA.

Nduli wa Ghaza, waziri mkuu wa utawala wa Kizayuni, Benjamin Netanyahu, amekiri kuwa hivi sasa kuna wimbi kubwa la hasira za walimwengu dhidi ya utawala huo pandikizi unaofanya mauaji ya umati dhidi ya watoto wasio na hatia.

Hayo yameandikwa na gazeti la Uingereza la "Daily Mail" ambalo limemnukuu nduli wa Sabra na Shatila, Benjamin Netanyahu akikiri kuwa, chuki na hasira za walimwengu dhidi ya utawala wa Kizayuni zinazidi kuongezeka. Hapo hapo amedai kuwa mzingiro uliowekwa na rais wa marekani dhidi ya Iran eti umeidhoofisha sana nchi hiyo.

Akiendelea na bwabwaja zake bila ya kutaja jinai kubwa zinazofanywa na utawala wa Kizayuni ambazo ndicho chanzo kikuu cha kuongezeka hasira za walimwengu dhidi ya Israel, na bila ya kutaja pia uchokozi na jinai zilizofanywa na Wazayni na Marekani za kuivamia kijeshi Iran bila ya sababu yoyote, Netanyahu amedai kuwa Iran inalenga kusambaratisha uchumi wa nchi za Magharibi kwa kuvuruga njia za usafirishaji wa nishati na njia za maji za kimataifa.

Nduli huyo wa Ghaza ametoa madai hayo bila ya hata kugusia jinsi Marekani inavyoendesha mzingiro wa baharini dhidi ya Iran na anataraji kuwa Jamhuri ya Kiislamu itatulia tuli bila ya kutumia turufu yake ya Lango-Bahari la Hormuz.

Ukweli ni kuwa, hivi sasa Netanyahu ana hali ngumu sana ndani ya ardhi za Palestina zilizopachikwa jina bandia la Israel. Amerejea ndoto zake za mchana akidai kuwa, mfumo wa utawala wa Iran hatimaye utaanguka, ingawa itachukua muda.

Netanyahu ambaye duniani ni maarufu kwa jina la nduli wa Ghaza kutokana na jinai za kuchupa mipaka anazozifanya dhidi ya wananchi wasio na hatia wa ukanda huo, amedai bila ya aibu kwamba eti Israel inatetea ustaarabu na haipaswi kukasirikiwa kiasi chote hicho na walimwengu. Madai hayo yanahesabiwa kuwa ni aina fulani ya kuwatukana walimwengu na kuwafanya vipofu wasioona jinai za kupindukia zinazofanywa na Israel dhidi ya watu wasio na hatia.

Kwa haya na mengine

Unakaribishwa kwenye kituo chako kupitia :
https://www.facebook.com/profile.php?id=100063744357288

Vilevile https://whatsapp.com/channel/0029Va9jawz3rZZeo2Wmdo3R

Karibuni

UFARANSA YAITISHA MKUTANO WA DHARURA SHULE ZAJIANDAA KUFUNDISHA KWA NJIA YA MTANDAO KUTOKANA NA KUSHADIDI MAANDAMANO YA ...
03/10/2026

UFARANSA YAITISHA MKUTANO WA DHARURA SHULE ZAJIANDAA KUFUNDISHA KWA NJIA YA MTANDAO KUTOKANA NA KUSHADIDI MAANDAMANO YA WANAFUNZI

Shule nchini Ufaransa zinajiandaa kuhamishia baadhi ya masomo kwenye mfumo wa kufundisha kwa njia ya mtandao, huku vuguvugu la maandamano ya wanafunzi likiendelea kuenea kwa kasi nchini humo.

Wanafunzi wanaandamana kupinga msongamano wanafunzi madarasani, uhaba wa walimu na kuzorota kwa hali ya majengo ya shule. Hali hiyo imeifanya serikali kuitisha mkutano wa dharura.

Hatua hiyo imekuja wakati maandamano yakizidi kupamba moto na kugeuka kuwa makabiliano pamoja na vitendo vya uharibifu katika miji kadhaa. Wakati huohuo, kupanda kwa gharama za maisha kumeongeza mvutano wa kijamii nchini humo kuelekea uchaguzi wa rais wa Ufaransa.

Waziri Mkuu Sébastien Lecornu aliitisha mkutano wa dharura wa baraza la mawaziri siku ya Alhamisi na kuwaagiza mawaziri kufuta mipango yao ya safari, baada ya maandamano yaliyoanza Paris wiki iliyopita kuenea katika maeneo mbalimbali ya nchi hiyo ya Ulaya

Waziri wa Elimu, Édouard Geffray, alitarajiwa kukutana na wawakilishi wa wanafunzi siku ya Ijumaa.

Polisi wanasema kuwa takribani maandamano, vizuizi na matukio mengine yanayohusiana na maandamano 900 yalikuwa yakiendelea katika maeneo ya nje ya shule za sekondari kote nchini Ufaransa. Zaidi ya shule 160 zilikuwa zimefungwa. Aidha, njia za kuingia katika takribani kampasi 30 za vyuo vikuu zilikuwa zimezuiwa, zikiwemo kampasi zilizopo Paris na Marseille.

Kwa mujibu wa Wizara ya Mambo ya Ndani, karibu wanafunzi 3,000 wa shule za sekondari za juu, wenye umri wa miaka 15 hadi 18, wamek**atwa tangu maandamano hayo yalipoanza. Kati yao, wanafunzi 1,949 walik**atwa siku ya Alhamisi pekee.

Zaidi ya maafisa 300 wa polisi pamoja na makumi ya wazima moto, walimu na wanafunzi wamejeruhiwa. Maandamano hayo yamechochewa na malalamiko kuhusu ratiba ndefu na zilizosheheni masomo kupita kiasi, msongamano wa wanafunzi madarasani, uhaba wa walimu na kuzorota kwa majengo ya shule. Wanafunzi pia wamelalamikia joto lisilovumilika madarasani wakati wa mawimbi ya joto yaliyotokea mapema mwaka huu.

Kwa haya na mengine

Unakaribishwa kwenye kituo chako kupitia :
https://www.facebook.com/profile.php?id=100063744357288

Vilevile https://whatsapp.com/channel/0029Va9jawz3rZZeo2Wmdo3R

Karibuni

ERITREA YAKATA MAHUSIANO YOTE YA KIDIPLOMASIA NA ETHIOPIA. Eritrea imetangaza kukata mahusiano yote ya kidiplomasia na n...
01/10/2026

ERITREA YAKATA MAHUSIANO YOTE YA KIDIPLOMASIA NA ETHIOPIA.

Eritrea imetangaza kukata mahusiano yote ya kidiplomasia na nchi jirani ya Ethiopia, baada ya Ethiopia kuwafukuza wanadiplomasia 10 wa Eritrea siku ya Alhamisi.

Wizara ya Mambo ya Nje ya Eritrea ilisema hatua ya kukata mahusiano imechukuliwa kwa kujibu hatua ya Ethiopia kuwafukuza wanadiplomasia hao kutoka Addis Ababa.

Katika taarifa iliyowekwa kwenye mtandao wa X, wizara hiyo ilisema Eritrea “haina chaguo jingine isipokuwa kujibu kwa hatua k**a hiyo na kukata mahusiano yote ya kidiplomasia na Ethiopia, pamoja na madhara yote yanayoweza kutokana na hatua hiyo.”

Awali, Ethiopia ilitangaza kuwafukuza wanadiplomasia 10 wa Eritrea, ikidai kuwa walihusika katika shughuli ambazo zilikuwa “tishio la moja kwa moja” kwausalama wa taifa wa Ethiopia

Katika taarifa iliyochapishwa kwenye Facebook, Wizara ya Mambo ya Nje ya Ethiopia ilisema imewatangaza wanadiplomasia hao 10 waliokuwa Addis Ababa kuwa watu wasiotakiwa —yaani watu wasioruhusiwa kuendelea kubaki nchini—kwa madai ya kujihusisha na shughuli zinazotishia moja kwa moja usalama wa taifa wa Ethiopia.

Wizara hiyo pia ilisema imeamua kuifunga Ubalozi wa Ethiopia mjini Asmara, mji mkuu wa Eritrea, ikitaja hatua hiyo kuwa ni majibu kwa kile ilichokiita “vitendo vya uhasama na uchochezi wa moja kwa moja na usio wa moja kwa moja” kutoka Eritrea kuelekea Ethiopia.

Kwa haya na mengine

Unakaribishwa kwenye kituo chako kupitia :
https://www.facebook.com/profile.php?id=100063744357288

Vilevile https://whatsapp.com/channel/0029Va9jawz3rZZeo2Wmdo3R

Karibuni

RUSSIA YATISHIA KUWASHAMBULIA KWA BOMU LA NYUKLIA WANACHAMA WA NATO. Moscow imeionya NATO kwamba inaweza kutumia silaha ...
01/10/2026

RUSSIA YATISHIA KUWASHAMBULIA KWA BOMU LA NYUKLIA WANACHAMA WA NATO.

Moscow imeionya NATO kwamba inaweza kutumia silaha za nyuklia kuwashambulia wanachama wa jeshi hilo la nchi za Marekani iwapo muungano huo utajaribu kukata mawasiliano kati ya Kaliningrad na eneo kuu la Russia.

Shirika la habari la Mehr limeripoti habari hiyo kupitia Reuters na kusema kuwa, Russia imetuma waraka kwa jeshi la nchi za Magharibi NATO ikilaani chokochoko za muungano huo na kuzitaja kuwa ni hatari kubwa. Imeonya kuhusu uwezekano wa kutokea vita vya moja kwa moja baina ya Russia na NATO na kusema kuwa, ikilazimika, Moscow haitosita kutumia silaha za nyuklia dhidi ya wanachama wa NATO.



Waraka huo umeeleza kuwa, iwapo nchi wanachama wa NATO zitajaribu kulitenga jimbo la Kaliningrad na kukata mawasiliano baina ya jimbo hilo na maeneo mengine ya Russia, basi Moscow nayo haitosita kutumia uwezo wake wote zikiwemo silaha za nyuklia kulinda eneo hilo na kujihami mbele ya wanachama wa NATO.



Msemaji wa Kremlin, Dmitry Peskov, vilevile amesema kuwa, maonyo ya hivi karibuni yaliyotolewa na balozi za Russia katika nchi kadhaa za Ulaya kuhusu jimbo la Kaliningrad la Russia la kuzitaka nchi hizo za Ulaya ziache chokochoko zao za kujaribu kulitenga eneo hilo na maeneo mengine ya Russia, yalikuwa ni k**a njia ya kuwakumbusha "watu wenye misimamo mikali barani Ulaya" kuhusu msimamo rasmi wa Moscow.

Kaliningrad ni eneo la Russia lililoko kati ya Poland na Lithuania kwenye pwani ya Bahari ya Baltic.

Katika kujibu onyo hilo la Russia, jeshi la nchi za Magharibi NATO limesema kuwa shughuli na mazoezi yake ya kijeshi si tishio la aina yoyote ile kwa Russia.

Kwa haya na mengine

Unakaribishwa kwenye kituo chako kupitia :
https://www.facebook.com/profile.php?id=100063744357288

Vilevile https://whatsapp.com/channel/0029Va9jawz3rZZeo2Wmdo3R

Karibuni

POLISI AFRIKA KUSINI WAKABIANA KWA NGUVU NA UCHIMBAJI HARAMU WA MADINI. Polisi nchini Afrika Kusini wamewatia mbaroni za...
01/10/2026

POLISI AFRIKA KUSINI WAKABIANA KWA NGUVU NA UCHIMBAJI HARAMU WA MADINI.

Polisi nchini Afrika Kusini wamewatia mbaroni zaidi ya washukiwa 100 wanaohusishwa na vikundi haramu vya uchimbaji madini ambavyo pia vinahusishwa na ufyatuaji risasi katika mikahawa, hivi karibuni, katika jimbo la Gauteng.

Operesheni kubwa ya usalama imeimarisha uchunguzi wa vitendo vinavyoendelea vya vurugu, upatikanaji wa silaha nzito na vitendo vya uhalifu vinavyofanywa na magenge yenye mitandao mipana haramu ya uchimbaji madini yaliyoenea kila mahali nchini humo.



Operesheni ya kutiwa mbaroni watu hao ilianza baada ya kutokea shambulio la mauaji Jumamosi usiku huko Wedela, mji ulioko karibu na kitovu cha uchimbaji dhahabu cha Carletonville, yapata kilomita 80 kusini magharibi mwa Johannesburg. Watu kumi na nane waliuawa baada ya watu wenye silaha nzito kuvamia mkahawa mmoja wa eneo hilo karibu saa 3:30 usiku na kuwafyatulia risasi ovyo watu waliokuwemo kwenye mkahawa huo.



Polisi wana wasiwasi kwamba tukio hilo lilikuwa ni shambulio la kulipiza kisasi lililohusishwa na ugomvi wa kimaeneo kati ya vikundi haramu vya uchimbaji madini, kwa sababu mwezi uliopita pia kulikuwa na ufyatuaji risasi k**a huo katika mkahawa huo huo.



Katika kukabiliana na tishio hilo, polisi wa Gauteng walitangaza Jumanne kwamba vikosi vya usalama vya mashirika mengi viliwatia mbaroni watu 121 wanaotuhumiwa kuendesha operesheni haramu za kuchimba madini kinyume cha sheria. Polisi hao walik**ata pia silaha tano, ikiwa ni pamoja na bunduki ya AK-47 na bunduki tatu za mkononi, pamoja na mitungi ya gesi na vifaa maalumu vya uchimbaji madini wakati wa msako wa pamoja uliopewa jina la "Operesheni Prosper."



Brigeri Brenda Muridili, msemaji wa Jeshi la Polisi la Afrika Kusini huko Gauteng, amesema kwamba, tangu mwezi Machi, kikosi kazi cha pamoja kinachojumuisha polisi, timu maalumu za kukabiliana na uhalifu kimkakati na Jeshi la Ulinzi wa Taifa la Afrika Kusini kimetumwa kwenda kulinda usalama katika wilaya zenye hatari kubwa kutokana na shughuli nyingine za uchimbaji madini.

Kwa haya na mengine

Unakaribishwa kwenye kituo chako kupitia :
https://www.facebook.com/profile.php?id=100063744357288

Vilevile https://whatsapp.com/channel/0029Va9jawz3rZZeo2Wmdo3R

Karibuni

BAADA YA KUJITOA 2016 UINGEREZA YAFIKIRA KUJIUNGA TENA NA UMOJA WA ULAYA. Waziri Mkuu wa Uingereza Andy Burnham, amesema...
01/10/2026

BAADA YA KUJITOA 2016 UINGEREZA YAFIKIRA KUJIUNGA TENA NA UMOJA WA ULAYA.

Waziri Mkuu wa Uingereza Andy Burnham, amesema, uamuzi wa nchi hiyo wa kujiunga tena na Umoja wa Ulaya, EU utasaidia katika kukuza mahusiano na mataifa mengine ndani ya umoja huo.

Akizungumza jana Jumatano, Burnham alisema, anatumaini kwamba, Uingereza itarudi tena kwenye umoja huo.

"Kwa sasa, tunaangalia namna mbalimbali za kurudi ndani ya Umoja wa Ulaya, kwa kuzingatia faida na hasara zake,” ameeleza waziri mkuu huyo wa Uingereza.

Kwa mujibu wa Burnham, ambaye alishika wadhifa wa uwaziri mkuu kuanzia mwezi Julai mwaka huu, mchakato wa kujiondoa ndani ya Umoja wa Ulaya, maarufu k**a ‘Brexit’, umeathiri nchi hiyo kwa kiasi kikubwa.

Uingereza ilipiga kura ya kujiondoa ndani ya Umoja wa Ulaya, kupitia kura ya maoni ya mwaka 2016.

Katika kura hiyo ya maoni, asilimia 52 ya Waingereza waliunga mkono kujitoa katika Umoja wa Ulaya mkabala wa 48% waliopinga uamuzi huo.

Waingereza wengi wa England na Wales walipiga kura kuunga mkono Brexit, lakini wakazi wengi wa Scotland na Ireland ya Kaskazini walipinga uamuzi huo na kutaka nchi hiyo iendelee kubakia katika EU.

Kufuatia tamko hilo la waziri mkuu wa Uingereza, Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amesema itakuwa "habari njema sana" iwapo Uingereza itataka kujiunga tena na Umoja wa Ulaya, huku Waziri Mkuu wa Uhispania Pedro Sanchez naye pia akisema nchi yake itaikaribisha tena Uingereza "kwa mikono miwili" katika umoja huo.

Kwa haya na mengine

Unakaribishwa kwenye kituo chako kupitia :
https://www.facebook.com/profile.php?id=100063744357288

Vilevile https://whatsapp.com/channel/0029Va9jawz3rZZeo2Wmdo3R

Karibuni

RAIS WA AFRIKA KUSINI ATAKA HATUA ZICHUKULIWE KUWALINDA WANAWAKE BAADA YA KUPATIKANA MIILI YAO 11 ILIYOTUOWA. Rais Cyril...
30/09/2026

RAIS WA AFRIKA KUSINI ATAKA HATUA ZICHUKULIWE KUWALINDA WANAWAKE BAADA YA KUPATIKANA MIILI YAO 11 ILIYOTUOWA.

Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini amesema ametoa agizo la kufanyika operesheni ya kusafisha maeneo ya manispaa yenye hatari kubwa na kuchukuliwa hatua kali dhidi ya matumizi mabaya ya pombe ili kuwalinda wanawake, kufuatia mfululizo wa mauaji uliosababisha malalamiko na hasira nchi nzima.

Kupatikana miili ya wanawake 11 iliyotupwa katika eneo la Ekurhuleni, mashariki mwa Johannesburg, kuanzia katikati mwa Julai, kumeibua tena wasiwasi kuhusu viwango vya juu vinavyoendelea vya ukatili wa kijinsia nchini humo.

“Taifa la Afrika Kusini limekasirika. Wanawake wa Afrika Kusini wamekasirika. Hasira yao ina msingi wa kueleweka. Nami pia nimekasirika,” alieleza Ramaphosa katika hotuba kwa taifa aliyotoa jana Jumanne.

Alisema serikali imeanzisha operesheni ya dharura ya kitaifa inayohusisha wataalamu kutoka nyanja mbalimbali ili kuchunguza mauaji hayo ya Ekurhuleni. Watu wanne wako chini ya ulinzi wa polisi kuhusiana na tukio hilo.

“Kumekuwa na hofu kubwa kwamba kugunduliwa kwa miili ya wanawake hao katika maeneo yaliyo karibu kunaweza kuashiria kwamba mauaji hayo yalifanywa na mhusika mmoja,” alieleza Rais wa Afrika Kusini na kuongezea kwa kusema: “hata hivyo, kwa sasa polisi hawajapata ushahidi unaothibitisha kwamba mauaji hayo yalifanywa na mhusika mmoja.”

Mwili wa mwisho ulipatikana siku ya Jumapili katika eneo la wazi. Siku moja kabla yake, mwili wa mwanamke aliyekuwa karibu bila nguo ulipatikana karibu na makaburi katika manispaa hiyo hiyo.

Waathiriwa wengi walikuwa katika umri wa miaka kati ya 20 na 30. Baadhi yao walikuwa wamevuliwa nguo na walionyesha dalili za kufanyiwa udhalilishaji wa kingono.

Japokuwa ukatili wa kijinsia ulitangazwa mwaka jana janga la kitaifa nchini Afrika Kusini, rais Ramaphosa amesema serikali imeshindwa kuwakinga wanawake ipasavyo. Ametangaza hatua mpya kadhaa za serikali, zikiwa na muda maalumu wa utekelezaji.

“Ni lazima tukabiliane na ukweli. Tulichofanya hadi sasa hakijatosha. Tunahitaji kufanya mengi zaidi,” ameeleza kiongozi huyo na kusisitiza:

“Ni lazima kila manispaa ianze mara moja kuimarisha usalama wa wanawake. Maeneo hatarishi lazima yatambuliwe” na kuchukuliwa hatua.

Ramaphosa amesema, ukaguzi huo unapaswa kubaini taa za barabarani zilizoharibika, maeneo ya umma yaliyoota nyasi na vichaka kupita kiasi, majengo yaliyotelekezwa, njia na vituo vya usafiri visivyo salama, bustani zisizolindwa vya kutosha, pamoja na hali nyingine zinazowaweka wanawake katika hatari.

Ameamuru pia kutekelezwa kwa “mpango wa utekelezaji wa sheria” wenye lengo la kupunguza vurugu zinazohusishwa na matumizi ya pombe.

Polisi na waendesha mashtaka wameagizwa kufungua upya kesi ambazo hazijatatuliwa zinazohusu wanawake na watoto, pamoja na kuharakisha kesi zinazoendelea, huku kipaumbele kikitolewa kwa kesi za ukatili wa kijinsia na mauaji ya wanawake kwa sababu ya jinsia yao

Kwa haya na mengine

Unakaribishwa kwenye kituo chako kupitia :
https://www.facebook.com/profile.php?id=100063744357288

Vilevile https://whatsapp.com/channel/0029Va9jawz3rZZeo2Wmdo3R

Karibuni

Address

KwaZulu Natal
Pietermaritzburg

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Zamzam news. posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to Zamzam news.:

Shortcuts

Share